Wawekezaji wakubwa ni watu wema na waaminifu; dr. Kafumu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wawekezaji wakubwa ni watu wema na waaminifu; dr. Kafumu

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Babu Lao, Mar 25, 2011.

 1. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #1
  Mar 25, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Wakati Wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), wameitaka Serikali kufunga viwanja vya ndege vilivyojengwa katika maeneo ya migodi kwa kuwa vinatumiwa na wawekezaji kutorosha dhahabu nje ya nchi bila kulipa mapato; Kamishna wa Madini wa Wizara ya Nishati na Madini, Dk. Peter Kafumu, alipingana na hoja hizo na kusema wawekezaji wakubwa ni watu wema na waaminifu, bali wanaoweza kufanya uhuni ni wachimbaji wadogowadogo, ambao ni wazawa kwa kugopa kufungiwa biashara zao kwenye soko la hisa.

  Akichangia katika kikao kati ya Wizara ya Nishati na Madini na wajumbe wa kamati hiyo, kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam, Mbunge wa Shinyanga Mjini, Stephen Masele, alisema ana ushahidi kwamba, wawekezaji wanatorosha dhahabu nje ya nchi kwa kutumia viwanja wanavyomiliki maeneo ya migodini. “Mheshimiwa Mwenyekiti, hili sio jambo la siri. Hawa wawekezaji wanatumia viwanja hivi kuvusha dhahabu kwa kutumia ndege zao, ambazo hazipiti kwenye viwanja vya kawaida,” alisema.

  Alisema Serikali wamekuwa wepesi kufanya ukaguzi katika mazao ya pamba, ambayo yanasafirishwa nje ya nchi kwa kukagua kontena moja baada ya lingine, lakini kwenye madini wameshindwa kufanya hivyo ingawa huko ndiko kwenye fedha nyingi.

  Masele alisema pia ana mfano hai kwamba, mgodi wa Mwadui, mkoani Shinyanga ingawa hivi sasa umefungwa, wawekezaji wanafanya uzalishaji kinyemela, huku wakikwepa kulipa mapato ya Serikali.

  Mbunge wa Chwaka, Yahya Kassim Issa, akichangia katika kikao hicho, alisema wawekezaji ni watu waliokuja kuchuma, hivyo sio watu wa kuaminiwa, wafanye kazi nwenyewe bila kusimamiwa na kisha waweze kulipa mapato sahihi.

  Dk. Kafumu alipingana na hoja za Wabunge hao na kusema kuwa ndege zote zinazochukua vifurushi vya dhahabu zinapitia kwenye Viwanja vya Ndege vya Kimataifa vya Kilimanjaro (KIA) na Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es Salaam na kwamba katika viwanja hivyo, kuna maofisa wa TRA na wa madini, ambao wanahakikisha mzigo wote umekaguliwa kabla ya kuondoka nchini.

  ANGALIZO: Hivi huyu bwana antaka kutuambia kuwa haoni hata mantiki ya posibility kuwa hawa jamaa na ndege zao wanavusha hayo madini isivyo halali au ndio anawalinda sababu wanamlinda? Sijawahi ona mtanzania mpu***vu kama huyu!!!
   
Loading...