Wawekezaji wa migodi wazidi kuitafuna serikali...tazama hii!

Mkeshaji

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
4,262
1,416
Wakuu poleni na mapumziko ya sikukuu ya mapinduzi ya Zanzibar.
Jana kwenye taarifa ya habari ya ITV saa mbili usiku nilimuona Waziri wa Nishati na Madini Bw. William Ngeleja akifungua mradi wa maji ambao upo katika mgodi wa GGM.

Katika maelezo yao (Mkurugenzi wa wilaya ya Geita na mwakilishi wa GGM) walidai kuwa pindi utakapokamilika, mradi huo wa maji utakuwa na uwezo wa kutoa mita za ujazo 500 kwa siku ambapo mgodi wa Geita utakuwa unatumia mita za ujazo 300 na kiwango kitakachobaki (mita za ujazo 200) watapelekewa wananchi wa Geita.

Gharama ya mradi huo ni sh. 15bn ambapo GGM watatoa 6bn na kiasi kitakachobaki 9bn kitagharamiwa na serikali.
Nilijaribu kufanya analysis ndogo ya haraka haraka ambapo niligundua kuwa:

1. GGM watatumia 60% ya maji yote yatakayozalishwa na wananchi wa Geita watapelekewa 40% ya kiasi kinachobaki (hatukuelezwa kama mita za ujazo 200 ndiyo mahitaji ya wananchi wa Geita kwa siku).

2. Katika kuchangia, GGM wao watachangia 40% wakati serikali kwa niaba ya wananchi wake itachangia 60% ya mradi wote.

Swali linakuja:
Inakuwaje mgodi ambao utatumia maji zaidi ya mara moja na nusu ya wananchi uchangie mradi huo mara moja na nusu chini ya kiwango ambacho serikali itachanga?
Nilitarajia kuwa mtu anayetumia zaidi ndiye anastahili kulipa zaidi, lakini vilevile nilitarajia kuwa hii ilikuwa nafasi nzuri kwa mgodi kurudisha japo kiasi kidogo cha faida yao kwa wananchi.
Napata picha (na hii ni kwa mtu yeyote mwenye akili) kwamba mradi huo ni kwa manufaa ya mgodi isipokuwa kuna hila imefanyika ili serikali igharamie mradi huo kwa manufaa ya GGM.

IWAPI SASA FAIDA YA UWEKEZAJI KATIKA MIGODI KAMA KILA KITU TUNAWAGHARAMIA KILA KITU HALI WAO HAWALIPI CHOCHOTE SERIKALINI?

Zinduka!.
 
Mkeshaji tatizo ni kuwa sisi ndio tunaona hivyo lakini wao wanaona vinginevyo.
 
Watanzania wenyewe mmeamua hivyo.
Na bei ya umeme imepandishwa ili kuilipa dowans, na bado mtakaa kimya tu.
Kulalamikia kwenye keyboard hakutasaidia kitu.
Angalieni wenzenu Nigeria wanachokifanya sasa.
 
FYI hata mradi wa maji wa ziwa Victoria to Shinyanga and Kahama lenogo kuu ilikuwa kupeleka mradi ili mgodi wa Buzwagi uweze kufunguliwa,pamoja na majigambo ya waasisi wa mradi huo kuwa wamewasaidia wananchi wa kanda ya ziwa,sio kweli lengo ni kwa wawekezaji wa Buzwagi Gold mine,na si ajabu walikula cha juu,wanachi wananufaika kama spill over effect lakini hawakuwa walengwa.The same story na hiyo ya GGM kwani mradi huu uligharamiwa na serikali kwa asilimia 100 lakini kwa manufaa ya wawekezaji,mnaofanya researches mashuleni fanyeni utafiti mtagundu nalolisema kuwa watumiaji wakubwa na wenye priority kwenye mradi wa ziwa Victoia ni wawekezaji wa Buzwagi na ndio walipaji wakubwa wa bill kuliko bill zote za wanachi wa kanda ya ziwa ukizichanganya.
 
FYI hata mradi wa maji wa ziwa Victoria to Shinyanga and Kahama lenogo kuu ilikuwa kupeleka mradi ili mgodi wa Buzwagi uweze kufunguliwa,pamoja na majigambo ya waasisi wa mradi huo kuwa wamewasaidia wananchi wa kanda ya ziwa,sio kweli lengo ni kwa wawekezaji wa Buzwagi Gold mine,na si ajabu walikula cha juu,wanachi wananufaika kama spill over effect lakini hawakuwa walengwa.The same story na hiyo ya GGM kwani mradi huu uligharamiwa na serikali kwa asilimia 100 lakini kwa manufaa ya wawekezaji,mnaofanya researches mashuleni fanyeni utafiti mtagundu nalolisema kuwa watumiaji wakubwa na wenye priority kwenye mradi wa ziwa Victoia ni wawekezaji wa Buzwagi na ndio walipaji wakubwa wa bill kuliko bill zote za wanachi wa kanda ya ziwa ukizichanganya
 
Huo mradi wa Geita wananchi waliahidiwa kuwa ifikapo november 2011 wangekuwa wanatumia maji ya mferejini lakini mpaka sasa hakuna kinachoendelea huko wala dalili ya kuwa watapata maji hivi karibuni.
 
tatizo wenyeji wa maeneo ya madini ni wadanganyika sana.Chama Cha Magamba kinawadanganya sana
 
Kama mwekezaji anakopeshwa pesa na Serikali ili alipe mishahara ya wafanyakzai, hata hili sishangai.
Serikali imenunuliwa na wenye pesa. Inaendeshwa kama gari bovu.
 
Wakuu poleni na mapumziko ya sikukuu ya mapinduzi ya Zanzibar.
Jana kwenye taarifa ya habari ya ITV saa mbili usiku nilimuona Waziri wa Nishati na Madini Bw. William Ngeleja akifungua mradi wa maji ambao upo katika mgodi wa GGM.

Katika maelezo yao (Mkurugenzi wa wilaya ya Geita na mwakilishi wa GGM) walidai kuwa pindi utakapokamilika, mradi huo wa maji utakuwa na uwezo wa kutoa mita za ujazo 500 kwa siku ambapo mgodi wa Geita utakuwa unatumia mita za ujazo 300 na kiwango kitakachobaki (mita za ujazo 200) watapelekewa wananchi wa Geita.

Gharama ya mradi huo ni sh. 15bn ambapo GGM watatoa 6bn na kiasi kitakachobaki 9bn kitagharamiwa na serikali.
Nilijaribu kufanya analysis ndogo ya haraka haraka ambapo niligundua kuwa:

1. GGM watatumia 60% ya maji yote yatakayozalishwa na wananchi wa Geita watapelekewa 40% ya kiasi kinachobaki (hatukuelezwa kama mita za ujazo 200 ndiyo mahitaji ya wananchi wa Geita kwa siku).

2. Katika kuchangia, GGM wao watachangia 40% wakati serikali kwa niaba ya wananchi wake itachangia 60% ya mradi wote.

Swali linakuja:
Inakuwaje mgodi ambao utatumia maji zaidi ya mara moja na nusu ya wananchi uchangie mradi huo mara moja na nusu chini ya kiwango ambacho serikali itachanga?
Nilitarajia kuwa mtu anayetumia zaidi ndiye anastahili kulipa zaidi, lakini vilevile nilitarajia kuwa hii ilikuwa nafasi nzuri kwa mgodi kurudisha japo kiasi kidogo cha faida yao kwa wananchi.
Napata picha (na hii ni kwa mtu yeyote mwenye akili) kwamba mradi huo ni kwa manufaa ya mgodi isipokuwa kuna hila imefanyika ili serikali igharamie mradi huo kwa manufaa ya GGM.

IWAPI SASA FAIDA YA UWEKEZAJI KATIKA MIGODI KAMA KILA KITU TUNAWAGHARAMIA KILA KITU HALI WAO HAWALIPI CHOCHOTE SERIKALINI?

Zinduka!.

Mkuu Zinduka napenda kuchangia kwenye analysis yako kama ifuatavyo:
1. Nikweli mwakilishi wa GGM alisema mradi huo utakuwa na uwezo wa kuzalisha mita za ujazo 500
2. Jamaa aliendelea kusema kwasasa hivi uwezo wa uzalishaji ni mita za ujazo 250 ( the existing infrastructures has a capacity of pumping 250 meter cubic).
3. Kutokana na point No 1 & 2, mradi unaotegemewa ni upgrade ya existing infrastructure na mchanganuo ni wa 60% ya 50% au 40% ya 50% kwani tayari uwezo wa uzalishaji mpaka sasa ni 250 mita za ujazo ambayo ni 50% ya 500 mita za ujazo.
Kitu chakujiuliza ambacho nadhani hata uongozi wa wiliya kupitia kwa mkulugezi wao hajajiuliza ni ile running cost inakuwaje, wasije kubebeshwa zigo la kupampu maji kutoka Nungwe wao wenyewe na kuwabebesha wananchi wa Geita huo mzigo na kujikuta bill za maji zikawa hazikamatikiti.
Kama kunauwezekano wakupata agreement ya huo mradi basi ni vizuri iwekwe hapa ili wadau waweze kusaidia kuonyesha mapungufu ya mkataba huo na uendeshaji wa huo mradi.
 
.............GGM watatumia 60% ya maji yote yatakayozalishwa na wananchi wa Geita watapelekewa 40% ya kiasi kinachobaki ..............

Serikali inatakiwa kuandaa mazingira mazuri ya kuvutia wawekezaji!!!
 
Wewe umechelewa sana kugundua utata miongoni mwa irregularities nyingi kwenye mikataba ya wawekezaji wa migodi. Je umewahi kuwajulisha wananchi kuwa zaidi ya GOLD inayochimbwa pia huwa wanachimba PLATINIUM. Kama ukiwafahamisha wananchi labda watafungua macho na kudai mikataba yote ibatilishwe na ifanyike mipya kwa maslahi ya taifa. Wananchi wenzangu hembu tengeni muda mdogo kila siku ili mjiulize: KWA NINI UDONGO WENYE DHAHABU SIKU ZOTE UNAPELEKWA NJE YA NCHI KWA KISINGIZIO UNAPELEKWA KUSAFISHWA NA KWA NINI HAPAJAJENGWA MTAMBO WA KUUSAFISHA UDONGO HUO HAPA NCHINI HATA AKIPATINA MWEKEZAJI WA KUUJENGA.

What does a fish know about the water in which it swims all its life?
 
FYI hata mradi wa maji wa ziwa Victoria to Shinyanga and Kahama lenogo kuu ilikuwa kupeleka mradi ili mgodi wa Buzwagi uweze kufunguliwa,pamoja na majigambo ya waasisi wa mradi huo kuwa wamewasaidia wananchi wa kanda ya ziwa,sio kweli lengo ni kwa wawekezaji wa Buzwagi Gold mine,na si ajabu walikula cha juu,wanachi wananufaika kama spill over effect lakini hawakuwa walengwa.The same story na hiyo ya GGM kwani mradi huu uligharamiwa na serikali kwa asilimia 100 lakini kwa manufaa ya wawekezaji,mnaofanya researches mashuleni fanyeni utafiti mtagundu nalolisema kuwa watumiaji wakubwa na wenye priority kwenye mradi wa ziwa Victoia ni wawekezaji wa Buzwagi na ndio walipaji wakubwa wa bill kuliko bill zote za wanachi wa kanda ya ziwa ukizichanganya.
Uliloandika ni fact
 
Back
Top Bottom