Wawekezaji Uchwara wanapaswa kupuuzwa, Rais Magufuli songa mbele

mdhalendo

JF-Expert Member
Dec 14, 2011
282
273
Siku za hivi karibuni kumekuwa na kawaida ya wawekezaji uchwara kuongea mambo yenye kuwatishia na kuwavunja moyo wawekezaji wengine. Mfano ni Dangote ambaye ameonekana kwenda kinyume na anapambana na sera za Magufuli waziwazi mpaka kwenye majukwaa ya kimataifa.

Ningependa kuishauri serikali kuwapuuza kabisa wawekezaji wa aina hii kwasababu wanatumiwa na maadui zetu kuturudisha nyuma kwenye safari yetu ya kuelekea Tanzania ya Viwanda, Uchumi wa Kiviwanda, Mapinduzi ya Viwanda na Tanzania mpya.

Baba yetu Magufuli songa mbele usisikilize kelele za chura wala kelele za watetezi wa mabepari. Kumbuka kwamba kundi kubwa la watanzania wanyonge tunakuunga mkono kwa juhudi zako kubwa unazozifanya kutetea rasilimali za wanyonge na makabwela, umerejesha nidhamu katika utumishi wa umma, leo hii tuna watumishi vijana na wachapakazi kama Ndugu Paul Makonda ambaye ukuu wake wa mkoa nia aina ya utendaji wenye kuacha alama kwa wakaazi wa Jiji la Dar es Salaam.

Mungu akubariki sana mkuu. Wanaosema hali ya maisha imekuwa ngumu ni waliozoea kuishi kiujanja ujanja. Wewe umetumwa kwa kazi maalumu ya kutufikisha kaanani. Songa mbele baba

maguu.jpg
 
Tinga tinga haliangalii sura...ni kufagia tuu...wanaochonga sana linawafagia tu hakuna namna nyingine
 
Siku za hivi karibuni kumekuwa na kawaida ya wawekezaji uchwara kuongea mambo yenye kuwatishia na kuwavunja moyo wawekezaji wengine. Mfano ni Dangote ambaye ameonekana kwenda kinyume na anapambana na sera za Magufuli waziwazi mpaka kwenye majukwaa ya kimataifa.
Ningependa kuishauri serikali kuwapuuza kabisa wawekezaji wa aina hii kwasababu wanatumiwa na maadui zetu kuturudisha nyuma kwenye safari yetu ya kuelekea Tanzania ya Viwanda, Uchumi wa Kiviwanda, Mapinduzi ya Viwanda na Tanzania mpya. Baba yetu Magufuli songa mbele usisikilize kelele za chura wala kelele za watetezi wa mabepari. Kumbuka kwamba kundi kubwa la watanzania wanyonge tunakuunga mkono kwa juhudi zako kubwa unazozifanya kutetea rasilimali za wanyonge na makabwela, umerejesha nidhamu katika utumishi wa umma, leo hii tuna watumishi vijana na wachapakazi kama Ndugu Paul Makonda ambaye ukuu wake wa mkoa nia aina ya utendaji wenye kuacha alama kwa wakaazi wa Jiji la Dar es Salaam. Mungu akubariki sana mkuu. Wanaosema hali ya maisha imekuwa ngumu ni waliozoea kuishi kiujanja ujanja. Wewe umetumwa kwa kazi maalumu ya kutufikisha kaanani. Songa mbele baba

View attachment 618771
Aluta Continua.......
 
Back
Top Bottom