mamayoyo1
JF-Expert Member
- Jul 25, 2018
- 1,011
- 1,019
Afisa mwandamizi wa Ubalozi wa Austria wenye makazi yake Nairobi, Kenya. Bw. Kurt Muellauer akifungua Kongamano la Biashara lililoandaliwa kwa ushirikiano kati ya Chama cha Wafanyabiashara, Wakulima na Wenyeviwanda Tanzania (TCCIA) na Ubalozi wa Austria.
Kongamano hilo nimwendelezo wa jitihada za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini Ujerumani ambao unawakilisha pia nchini Austria na wadau mbalimbali katika kutekeleza diplomasia ya uchumi. Pamoja na mambo mengine kampuni 8 kati 16 zinatarajiwa kufanya ziara jijini Dodoma tarehe 29 Januari kwa lengo la kukutana na Mawaziri wa Kilimo; Nishati; Fedha na Mipango; Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Watoto na Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Kongamano hilo limefanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.