Wawekezaji China wazidi kumiminika Tanzania

esther mashiker

JF-Expert Member
May 29, 2018
616
552
1552049840380.png

CHINA na Tanzania zimezidi kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji baada ya makampuni 13 toka nchi hiyo ya Asia ya Mashariki kutembele Tanzania na kusema wanataka kuanzisha uwekezaji mpya wenye dola za kimarekani milioni 167.

Maeneo watakayowekeza ni pamoja na kuanzisha kiwanda cha mabehewa ya treni, betri za magari na kiwanda cha vifungashio. Wawakilishi wa makampuni hayo 13 ya China wamezuru katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki ikiwa ni miezi michache imepita baada ya wengine 17 kutembelea Tanzania na kufanya mazungumzo na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) juu ya namna bora ya kuanzisha na kuendeleza uwekezaji katika sekta mbalimbali.

Kwa mujibu wa taarifa za TIC, China inaendelea kuongoza kwa kuweka mitaji mikubwa nchini kwa zaidi ya dola bilioni 5.8 katika uwekezaji kuanzia mwaka 1990 mpaka 2017. Ushirikiano wa Tanzania na China katika sekta mbalimbali unazidi kuimarika kila mwaka katika kuhakikisha nchi hizo mbili kila moja inanufaika. Kwa mujibu wa takwimu za karibuni, uwekezaji wa China hapa nchini umeongezeka mara kumi katika kipindi cha miaka sita kutoka dola za Kimarekani 672.6 milioni hadi dola bilioni 6.7.

Wawakilishi wa makampuni hayo 13 wamekutana na Kituo Cha Uwekezaji Tanzania pamoja na uongozi wa Mkoa wa Pwani ambapo wanataka kuanzisha uwekezaji huo unaotarajiwa kuongeza ajira kwa Watanzania na kufanikisha azma ya Rais John Magufuli ya kuimarisha uchumi wa viwanda. Uwekezaji huo utafanyika katika eneo la uwekezaji la Kiluwa Free Processing Zone, mkoani Pwani, nje kidogo ya jijini la kibiashara la Dar es Salaam.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Evarist Ndikilo aliwahikishia wawekezaji hao walioletwa nchini na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni za Kiluwa Group, Bw Mohamed Kiluwa kuwa uongozi wake utashirikiana na wafanyabiashara hao kuhakikisha shughuli zao mkoani humo zinafanyika vizuri kwa maslahi ya Tanzania na China.

“Kwa kuzingatia fursa zilizopo hapa nchini hususan hapa mkoani, wameamua kuja kuwekeza hapa na wapo tayari kufanya hivyo muda wowote baada ya kupata ardhi. Wana mtaji na teknolojia ya kutosha. Baada ya wiki moja au mbili tutakuwa tumeshawapa majibu juu ya upatikanaji wa eneo ili waanze shughuli zao mara moja,” alisema Mkuu wa Mkoa wa Pwana Bw. Ndikilo.

Aliongeza kuwa kati ya wawekezaji hao 13, sita tayari wameshaingizia nchini vifaa na mashine mbalimbali kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa shughuli hizo za uwekezaji. “Lazima tuwape ushirikiano wa hali ya juu wawekezaji wanaokuja kuunga mkono jitihada za nchi yetu kufikia Uchumi wa Viwanda,” alisisitiza.

Kwa upande wake, Bw. Kiluwa alishukuru Kituo Cha Uwekezaji Tanzania kwa kuweka mifumo na namna bora ya kuhimiza na kulete wawekezaji, hali iliyomsaidia kufanya mazungumzo na makampuni hayo ya China na hatimae kukubali kuingia nchini kufanya makubaliano ya kuanza uwekezaji.

Aliongeza kuwa tayari ameshaweka kila kitu sawa ikiwepo miundombinu muhimu kwa ajili ya shughuli hizo huku akiomba serikali iharakishe taraibu za kuwakabidhi ardhi kwa wawekezaji hao. Bw. Lu Xiaoqiang, Naibu Meneja Mkuu wa Kampuni ya Sinoma East Africa Limited, akizungumza kwa niaba ya wawekezaji hao, alisema wanataka kushirikiana na Tanzania kufanya shughuli mbalimbali za uwekezaji. Alisema kampuni yake itawekeza katika viwanda vya plastiki na betri za magari. “Tuna mipango mikubwa kwa siku za baadae, tunataka kuendeleza mambo mengi na wazawa wa hapa kwa faida ya pande zote mbili,” alisema Lu
 
View attachment 1040883

Baba Naima anakulipa bei gani kumpa promo mkuu, hayo ya china na kilua tumeanza kuyasikia tangu 2013 mpaka leo hakuna hata kiwanda kimoja kimezinduliwa ni hadithi tu, fanyeki kitu kionrkane kijitangaze sio mnaanza kujitangaza with empy hands, am sure kiluwa bado hajapewa kibali cha kujenga hicho kiwanda cha mabehewa na bado hana makubaliano na TRC, hauoni kama mnaharibu mnapoanza kuweka mambo wazi wakati hata makubaliano hayajasainiwa zaidi tu kiluwa amesign na mwekezaji wa kiwanda cha mabehewa ambae ni jambo group ila bado hajasaini makubaliano yoyote na TRC au serikali na kwa maana hiyo hicho kiwanda kitabaki kuwa ndoto mpaka atakapopewa kibali na serikali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi hawa hawasumbuliwi work permit kama wengine? Naona kama ni tofauti kwao.
Wachina sawa na mti wa kisamvu, unachuma then unasubili uchanue tena ili baadae uchume.

Wazee wa uhamiaji wanajua chines wanavoishi so wanatumia technic kana hiyo ya mti wa kisamvu.
 
Kila ninapoona neno Kiluwa basi lazima nikutane na neno Ardhi, huyu jamaa ni dalali wa mashamba au?
 
Uza migodi uza misitu uza mashirika ya umma ata mambo ya ndani uza uza tu lakini Roho tuachieni.
View attachment 1040883

CHINA na Tanzania zimezidi kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji baada ya makampuni 13 toka nchi hiyo ya Asia ya Mashariki kutembele Tanzania na kusema wanataka kuanzisha uwekezaji mpya wenye dola za kimarekani milioni 167.

Maeneo watakayowekeza ni pamoja na kuanzisha kiwanda cha mabehewa ya treni, betri za magari na kiwanda cha vifungashio. Wawakilishi wa makampuni hayo 13 ya China wamezuru katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki ikiwa ni miezi michache imepita baada ya wengine 17 kutembelea Tanzania na kufanya mazungumzo na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) juu ya namna bora ya kuanzisha na kuendeleza uwekezaji katika sekta mbalimbali.

Kwa mujibu wa taarifa za TIC, China inaendelea kuongoza kwa kuweka mitaji mikubwa nchini kwa zaidi ya dola bilioni 5.8 katika uwekezaji kuanzia mwaka 1990 mpaka 2017. Ushirikiano wa Tanzania na China katika sekta mbalimbali unazidi kuimarika kila mwaka katika kuhakikisha nchi hizo mbili kila moja inanufaika. Kwa mujibu wa takwimu za karibuni, uwekezaji wa China hapa nchini umeongezeka mara kumi katika kipindi cha miaka sita kutoka dola za Kimarekani 672.6 milioni hadi dola bilioni 6.7.

Wawakilishi wa makampuni hayo 13 wamekutana na Kituo Cha Uwekezaji Tanzania pamoja na uongozi wa Mkoa wa Pwani ambapo wanataka kuanzisha uwekezaji huo unaotarajiwa kuongeza ajira kwa Watanzania na kufanikisha azma ya Rais John Magufuli ya kuimarisha uchumi wa viwanda. Uwekezaji huo utafanyika katika eneo la uwekezaji la Kiluwa Free Processing Zone, mkoani Pwani, nje kidogo ya jijini la kibiashara la Dar es Salaam.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Evarist Ndikilo aliwahikishia wawekezaji hao walioletwa nchini na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni za Kiluwa Group, Bw Mohamed Kiluwa kuwa uongozi wake utashirikiana na wafanyabiashara hao kuhakikisha shughuli zao mkoani humo zinafanyika vizuri kwa maslahi ya Tanzania na China.

“Kwa kuzingatia fursa zilizopo hapa nchini hususan hapa mkoani, wameamua kuja kuwekeza hapa na wapo tayari kufanya hivyo muda wowote baada ya kupata ardhi. Wana mtaji na teknolojia ya kutosha. Baada ya wiki moja au mbili tutakuwa tumeshawapa majibu juu ya upatikanaji wa eneo ili waanze shughuli zao mara moja,” alisema Mkuu wa Mkoa wa Pwana Bw. Ndikilo.

Aliongeza kuwa kati ya wawekezaji hao 13, sita tayari wameshaingizia nchini vifaa na mashine mbalimbali kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa shughuli hizo za uwekezaji. “Lazima tuwape ushirikiano wa hali ya juu wawekezaji wanaokuja kuunga mkono jitihada za nchi yetu kufikia Uchumi wa Viwanda,” alisisitiza.

Kwa upande wake, Bw. Kiluwa alishukuru Kituo Cha Uwekezaji Tanzania kwa kuweka mifumo na namna bora ya kuhimiza na kulete wawekezaji, hali iliyomsaidia kufanya mazungumzo na makampuni hayo ya China na hatimae kukubali kuingia nchini kufanya makubaliano ya kuanza uwekezaji.

Aliongeza kuwa tayari ameshaweka kila kitu sawa ikiwepo miundombinu muhimu kwa ajili ya shughuli hizo huku akiomba serikali iharakishe taraibu za kuwakabidhi ardhi kwa wawekezaji hao. Bw. Lu Xiaoqiang, Naibu Meneja Mkuu wa Kampuni ya Sinoma East Africa Limited, akizungumza kwa niaba ya wawekezaji hao, alisema wanataka kushirikiana na Tanzania kufanya shughuli mbalimbali za uwekezaji. Alisema kampuni yake itawekeza katika viwanda vya plastiki na betri za magari. “Tuna mipango mikubwa kwa siku za baadae, tunataka kuendeleza mambo mengi na wazawa wa hapa kwa faida ya pande zote mbili,” alisema Lu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahah eti auze hata mambo ya ndani, shida huyu Kilua ni kujitangaza tu wakati hamna anachofanya anatumia mgongo wa viwanda kukwapua ardhi ya watanzania wanyonge

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwahiyo unataka kuniambia mkuu wa mkoa akishawapa ardhi hawatafanya huo uwekezaji? Kwahiyo anabaki kuhodhi ardhi tu? Halafu waziri akidai hati azifute anasema anazo mwenzake yupo nje ya nchi na kisha anapeleka rushwa? Na waziri akikataa rushwa na kumripoti polosi mahakamani anadai yeye ndie alikabwa na anaachiwa huru, si ndio?
 
Huyo mtu ni shida sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom