Bungeni Dodoma: Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akosa Mbunge wa kumuuliza swali la papo hapo

WINGER_TEREZA

JF-Expert Member
Jul 31, 2015
242
450
Habari wanajukwaa, ni utaratibu wa kawaida wa kila Alhamisi Wabunge hupata nafasi ya kuuliza maswali kwa Waziri Mkuu na kupatiwa majibu ya moja kwa moja hasa kuhusu mambo nyeti yanayopaswa kupatiwa majibu ya haraka toka serikalini.

Ila hali imekuwa tofauti katika Bunge hili na hali hiyo imedhihilika leo wakati wa kuanza kwa kipindi cha maswali na majibu nimemsikia naibu Spika, Dr Tulia, akitangaza kuwa leo hakutakuwa na kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu kwa sababu hakuna Mbunge hata mmoja aliyejiandikisha kumuuliza swali Waziri Mkuu, makubwa haya!

Nikikumbuka Bunge lililopita, nilikuwa naisubiria kwa hamu sana siku ya Alhamisi kumuona kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni, Freeman Mbowe wakati huo, kupata wasaa wa kumuuliza Waziri Mkuu juu ya sensitive essues. Pia kulikuwa na Wabunge wengine wakina Heche, Mnyika, Msigwa na n.k (mnisamehe kwa kumention waliokuwa Wabunge wa CDM tu kwa sababu hao ndio waliokuwa wanauliza sana maswali - so lirahisi kuwakumbuka) nao walikuwa "Wanamshambulia" Waziri Mkuu kama nyuki kwa maswali ya kina.

Bunge hili hali ni tofauti, yani katika Wabunge wote wale zaidi ya 300 eti wamekosekana hata watatu wakumuuliza waziri Mkuu kuhusu ata ule uchunguzi alioagiza mh. Raisi, Mh. Samia, ufanywe pale BOT katika pesa zilizotoka kuanzia mwezi January hadi March umefikia wapi?. Au kuuliza serikali inampango gani kuwashawishi "waliokimbia" nchini wakati wa utawala wa Mwendazake warudi waje kujenga nchi sasa kwa kuwa mambo ni "swali", kweli jamani?. Hii imenisikitisha sana kwa kweli!, Je nini kimepelekea kuwepo kwa hali hii?

Walasam.
 
Leo hii ikiwa ni Alhamisi kama tulivyozoea kuwa ni siku ya wabunge kumuuliza kiongozi wa shughuli za bunge mh Waziri Mkuu.

Naibu Spika, Dkt. Tulia Ackson amesema, leo Alhamisi kulikuwa na kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, lakini "hakuna mbunge aliyejiandikisha kwa ajili ya kumuuliza Waziri Mkuu."

Ktk hali ya kuangaza hakuna mbunge aliyekuwa tayari kujiandikisha ili amuulize mwaswali ya papo kwa papo mh waziri mkuu.

Bunge kukosa wabunge wa upinzani kunalifanya kulala usingizi wa pono.

Haya ndiyo madhara ambayo waliyo panga huu mpango wa kuwakwamisha wapinzani wasishinde basi yatawatafuna maishani mwao milele.

bungeni.jpg
 
Wapinzani walikuwa wanaleta maswali kwa kuibua mawazo mapya, Sasa mtu mmoja hayupo lakini akasema nileteeni huyu mtapata maendeleo,
Saizi Ni mwenda wa mawazo mgando tu mana wote Wana ilani moja, ambayo wameitengeneza wao.

Wakina mdee wakiuliza maswali wanajobolewa kwa sababu hawana chama.
 
Back
Top Bottom