Wawakilishi wahoji uhalali wa kuhojiwa na vyama vyao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wawakilishi wahoji uhalali wa kuhojiwa na vyama vyao

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by abdulahsaf, Aug 6, 2012.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Aug 6, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  [h=2][/h][​IMG]Mwakilishi wa jimbo la Chakechake Omar Ali Shehe

  Mwakilishi wa jimbo la Chakechake Omar Ali Sheikh amehoji uhalali wa vyama vya siasa kuwahoji wajumbe wa baraza la wawakilishi kufuatia hoja wanazozitoa katika vikao vya baraza hilo zinazokwenda kinyume na sera za vyama hivyo.
  Akizungumza katika semina ya elimu ya katiba amesema chombo hicho cha wananchi sasa kinaelekea kujali zaidi maslahi ya nchi badala ya vyama vya siasa, lakini amedai kuna watu wachache wasiojali uzalendo na kutaka kuwayumbisha wananchi.
  Shehe amesema katika mjadala wa bajeti unaondelea baadhi ya wawakilishi wamejaribu kuitwa na vyama vyao ili kuhojiwa juu ya msimamo wao wa mfumo wa muungano walioutoa ndani ya baraza hilo.
  Amesema kitendo hicho kinakwenda kinyume na sheria namba nne ya mwaka 2007 kuhusu kinga na fursa za wajumbe wa baraza hilo wanapokuwa ndani vikao vya baraza…
  Nae waziri wa sheria na katiba Zanzibar Abubakary Khamis Bakar ameshauri utowaji wa maoni hayo, sera za vyama vya siasa havina budi kuwekwa pembeni wakati wa kujadili maslahi ya Zanzibar
   
Loading...