wawakilishi wa TANZANIA NA MALAWI kukutana MZUZU tarehe August 20 2012

Ziwa Nyasa lote ni mali ya Malawi huo ni ukweli usiopingika.

Usipende majibu rahisi kwenye maswali magumu, kwa bahati mbaya conclusion yako haina mashiko katika kumaliza tatizo lililopo mbele yetu!

Tafadhali substantiate sababu zako za kuamini hivyo?!
 
kama hii nayo ni hoja, nitawashangaa sana wamalawi na uwezo wao wa kufikiri...

3. Zoezi ili lilikuwepo kitambo kwanini baada ya kuchaguliwa raisi mwanamke ndo Tanzania inapeleka majeshi na si kipindi cha mihula ya viongozi wanaume?

na kwa hoja ya namna hii, tanzania ina haki zote ya kuwapiga..... hata idd amini alisema kagera ni yake....na kama kweli wameleta hoja ya namna hii inadhihirisha jinsi gani walivyo waroho....
2. Sababu za Kamuzu banda ; kudai Mbeya na Nyasa ni mali ya Malawi
 
yaani mi nina wasiwasi kama roundtape technique itafanikiwa.... yaani dispute ya namna hii uwa inakuwa resolved by win-win method:israel:. ila kwa namna na nature ya mgogoro huu ulivyo sio kama kuna nchi itakubali kuachia kipande cha ziwa..

lawama zangu ni kwa K.B wa malawi na J.KM wa tanzania ambao waliweka kiporo hili swala, nadhani this time will pay it with profit , nawasiwasi vita inakuja

Nyerere sio wa kulaumiwa kwa suala hili hakuwa na mtazamo mmoja na Banda katika masuala matatu.

1. Kamuzu Banda alikuwa na uhusiano wa kibalozi na Afrika kusini enzi za ubaguzi wa rangi wakati wenzake wakiwa katika harakati ya kuikomboa Afrika.

2. Mawaziri wa Banda walimuasi 1964 walikimbilia Tanzania na Banda alimsusa Mwalimu kwamba anawatumia kutaka kumpindua.

3. Mgogoro wa mpaka.

Haya mambo matatu yalisababisha mgogo wa mpaka kutofikia suluhisho la kudumu enzi za Mwalimu na Banda.
 
Usipende majibu rahisi kwenye maswali magumu, kwa bahati mbaya conclusion yako haina mashiko katika kumaliza tatizo lililopo mbele yetu!

Tafadhali substantiate sababu zako za kuamini hivyo?!

LAKENYASA.jpg
 
Malawi and Tanzania representatives are scheduled to meet in Mzuzu on August 20 2012 ;

Malawi wana hoja 3 za msingi.

.1. Anglo-Germany treaty 1890 Boundary inayoonesha Tanganyika mpk hupo kwenye beach (coast)

2. Sababu za Kamuzu banda ; kudai Mbeya na Nyasa ni mali ya Malawi

3. Zoezi ili lilikuwepo kitambo kwanini baada ya kuchaguliwa raisi mwanamke ndo Tanzania inapeleka majeshi na si kipindi cha mihula ya viongozi wanaume?

Hoja yako ya tatu usiombe Bisimba akaisikia....unawadhalilisha wanawake. Kwani wanapigana ngumi kwamba akiwa mwanamke Malawi na mwanaume TZ ulingoni atashinda mwanaume? Ngoja tusubiri waje wenyewe
 
ziwa victoria lilikuwa linaitwa ziwa nyanza likabadilishwa jina kuwa ziwa victoria kwa heshima yake dada wa malikia wa Uingereza wakati huo Afrika Mashariki ilikuwa koloni la Waingereza..... je ziwa victoria ni la waingereza? je ni la dada yake Malakia wa Uingereza.
 
Nyerere sio wa kulaumiwa kwa suala hili hakuwa na mtazamo mmoja na Banda katika masuala matatu.

1. Kamuzu Banda alikuwa na uhusiano wa kibalozi na Afrika kusini enzi za ubaguzi wa rangi wakati wenzake wakiwa katika harakati ya kuikomboa Afrika.

2. Mawaziri wa Banda walimuasi 1964 walikimbilia Tanzania na Banda alimsusa Mwalimu kwamba anawatumia kutaka kumpindua.

3. Mgogoro wa mpaka.

Haya mambo matatu yalisababisha mgogo wa mpaka kutofikia suluhisho la kudumu enzi za Mwalimu na Banda.

nakubalia na wewe kiasi MAMA POROJO ,JK.Nyerere na banda walikuwa hawaendani kimtazamo, kiitikadi nafilosofia, but tukiwa focal kwenye hii dispute ya mpaka, swali linalohumiza kichwa ni kuwa, :

kwanini hawakufikia muafaka ??? whiy this dispute remained domant for all those year ??? je , unafikiri mazingira ya mwaka 2012 ni mazuri zaidi kwa kusolve hii issue diplomatically ukilinganisha na mazingira ya 1964 ???

kwa nini naisi vita ipo mlangoni:

1. viongozi wetu wa kisiasa wanaochulia hili suala kwa advantage ili kufanikisha azma yao ya kuwa successor wa JK-ilaza
2.pressure toka kwa wananchi wa malawi kwa raisi wao, kwamba yeye ni mwanamke dhaifu, ambaye ameshindwa hata kusema neno katika huu mgogoro wakati viongozi wake wa chini wakiongea nonsense
3.greed ya wawekezaji, hasa kwa upande wa malawi kwani ni vibaraka
4. kuna loop holes nyingi katika madai ya kila upande kuhusu umiliki wa ziwa. hili loop holes ndo zinafanya kila upande uamini kuwa hawa kwenye mahakama za kimataifa zitashinda
5. K.B na JK-Nyerere legacy kwa wananchi wao...ofcourse toka tupo chekechea tunajua mpaka upo katikati ya ziwa, je wamalawi wamekuwa wakifundishwa nini ? wamefundishwa mpaka upo kwenye shore of the lake....

UDHANI NI UPANDE GANI KATI YA TZ- & MALAWI utakao sacrifice madai yake kugrant WIN-WIN resolution na akaeleweka??? JK-ilaza dhaifu , mama banda dhaifu ... nguvu ya watu walio nyuma inatupeleka vitani
 
Mimi nilivyokuwa shule ya msingi miaka ya 80 nilikuwa nachora ramani kwa kupitisha mpaka katikati ya ziwa. Iweje leo iweje tofauti? Au niwaonyeshe Wamalawi nilivyokuwa nachora na tulivyofundishwa? Huwezi kudai kitu chako mpaka ukiona unadhulumiwa.
 
Wamalawi: Wanatumia Helgoland treaty ya 1890 " Ziwa sehemu ya Tanzania ni lao"
Tanzania : Wanatumia UN convection ya 1982 " nusu ya ziwa upande wa Tanzania ni eneo la Tanzania"

haya sasa wakienda kwenye Internationa law sijui nani atashinda
 
Ziwa Nyasa lote ni mali ya Malawi huo ni ukweli usiopingika.

mbona huzungumzii Msumbiji ktk kile kipande? Raman gn unayotumia ww,hii ni sawa na kusema ziwa tanganyika na victoria yote yapo Tz.
 
Alafu izi ramani zilichorwa na wazungu msiwape kichwa kwa kuzisadiki
Sisi waafrica ndo twajua mipaka ya nchi yetu iweje mgeni aje kutuwekea mipaka tutaonekana brainless
 
Si bora ningechora mimi, hiyo ni mipaka iliyowekwa toka enzi za wakoloni. hatuna ujanja katika hili suala. Tutashindwa na malawi kisheria. Malawi hawataki vita na wala hawana haja na vita, bali sheria itafuata mkondo wake.

kwa hiyo kwako wanachosema wakoloni ndio sahihi???? you must be kiding>>>>

Wakoloni ni watu ambao wanaweza kufanya madudu au kufanya jambo kwa interest zao??? binadamu ni yuleyule duniani kote.
 
Wamalawi: Wanatumia Helgoland treaty ya 1890 " Ziwa sehemu ya Tanzania ni lao"
Tanzania : Wanatumia UN convection ya 1982 " nusu ya ziwa upande wa Tanzania ni eneo la Tanzania"

haya sasa wakienda kwenye Internationa law sijui nani atashinda

Umesahau na Belin conference nao ni mkataba ulio upande wa tanzania.
 
Huu ni usanii mtupu.ziwa vicktoria linamilikiwa na nchi 3 na mipaka inaonyesha kuwa imepita kwenye maji.tz wanakipande chao uganda wanakipande chao na kenya wanakipande chao.vilevile nyasa kunanchi 3.baadhi ya ramani zinaonyesha kuwa mpaka umepita katikati ya ziwa kwamba kipande kimoja ni cha tz,mlw na msumbiji.ramani zingine zinaonyesha kuwa mpaka upo katika ya maji kuanzia msumbiji unapo karibia tz umekata kona na kuingia tz.hivyo tz kuonekana kuwa haina kitu chochote hapa.pia maelezo mingine yanaonyesha kuwa kuna wakati ziwa hilo lilikuwa huru bila kuwa na mwenyewe.utata wote huu unaonyesha kuwa ni maalumu kwa ajili ya kuikosesha tz haki yake.tunaambiwa kuwa mpaka uko kwenye pwani ya tz.binafsi sijawahi kuona mpaka unakuwa ndani ya nchi nyingine.tunaelezwa kuwa kulikuwa na makubaliano ya kila nchi kuheshim mipaka ilio wekwa na wakoloni. Lkn sijasikia maelezo yanayokataza kurekebisha makosa yaliofanywa na wakoloni kwenye mipaka.hapa iko namna mezani likishindikana hatunabudi kutumia mabom kudai haki yetu.
 
Acheni porojo.tupeni data kama amendments za mipaka baada ya treaty ya mwaka 1890 kama alivyokuwa anaelezea Waziri Membe mwaka 1947...........bungeni, na maazimio ya umoja wa mataifa kuhusu mipika ya kwenye maji,milima,mito n.k.tuone kama tuna hoja vinginevyo hawa wamalawi watatuzidi kwa hoja yao.tutapoteza ziwa lote,wavuvi wetu watatozwa kodi na mengineyo,ni sawa na kuuza baraza ya nyumba yako wakati bado unaishi ndani ya nyumba.
 
wasiwasi wangu ni hii staili ya maisha ya ubinafsi walio nao viongozi wetu na kama tunvyojua kuna tetesi kuwa kuna gesi, je hawa wadanganyika wakienda wakahakikishiwa rushwa kwa kupewa share kwenye mradi hawawezi kutuchinjia viwani kwenyewe? sina uhakika kama tukichagua viraza hapa tunaweza kutoswa
 
Malawi and Tanzania representatives are scheduled to meet in Mzuzu on August 20 2012 ;

Malawi wana hoja 3 za msingi.

.1. Anglo-Germany treaty 1890 Boundary inayoonesha Tanganyika mpk hupo kwenye beach (coast)

2. Sababu za Kamuzu banda ; kudai Mbeya na Nyasa ni mali ya Malawi

3. Zoezi ili lilikuwepo kitambo kwanini baada ya kuchaguliwa raisi mwanamke ndo Tanzania inapeleka majeshi na si kipindi cha mihula ya viongozi wanaume?

Kama kuna höja kama hii basi ni dhahiri kuwa Rais huyo mwanaharakati wa masuala ya jinsia hajiamini kabisa. Suala hili limeibuka sasa hivi kwa sababu Malawi wameipa kampuni ya kigeni kibali cha kufanya utafiti katika ziwa nzima wakati sehemu yao ni nusu tu. Hata angekuwa Ng'wazi bado yuko madarakani na akawaleta watu waingia kwenye eneo la mpaka wa Tanzania tusingemuachia. Wanatakiwa wajiulize kwanini Rais mwanamke ndio ameruhusu wageni kuchochea ugomvi kati yetu sio kuuliza kwa nini Tanzania inalinda mipaka yake inayovamiwa na Rais mwanamke. Hapa uanamke wa rais siyo hoja.
 
Back
Top Bottom