OLS
JF-Expert Member
- Oct 12, 2019
- 419
- 670
Uturuki yaingiza dola milioni 9.7 sawa na Tsh bilioni 22.3 katika biashara ya dagaa mwaka 2019. Mauzo ya nje ya dagaa kutoka nchini Uturuki yameongezeka kwa asilimia 1 ikilinganishwa na mwaka uliopita kwa kuuza tani 1996.
Mwaka 2019 tani takribani 1973 za dagaa zimeuzwa kutoka Uturuki na kuingiza dola milioni 9.7 katika uchumi wa Uturuki
Kiwango kikubwa cha dagaa wameuzwa nchini Ukraina, Somalia na Syria. Iko haja ya watanzania kujifunza kitu kwa wizara ya kilimo na uvuvi kujifunza kitu ili Tanzania ianze kusafirisha mazao yanayotokana na uvuvi kwa tija.
Na isiwe kama ilivyo hivi sasa kuwa hata samaki vibua walio wengi tunaingiza kutoka Japan, ilhali tuna mito, mabwawa, maziwa na bahari za kutosha
Kila kitu ni fursa ili tusipofikiri kwa upana, tutakuwa masikini mbali na kuwa na rasilimali za kutosha katika nchi yetu
Hali hiyo kiuchumi inaonyesha kuwa masoko yapo, ni kiasi cha sisi kuwa na tija katika uvunaji wa mazao yanayotokana na mito na bahari. Tuna taasisi nyingi ambazo zinaweza fanya tafiti na mikakati ya kuweza kukuza sekta ya uvuvi, kwa kuwa tuna idara ya uvuvi kwenye kila halmashauri, tuna TAFIRI(Tanzania Fisheries Research Institute) tuna FETA nk
Kama hizo taasisi tunaanzisha ili kuwapa ukurugenzi baadhi ya watu wetu, basi haina tija wala maana lakini kama tuna hizo taasisi, idara na mashirika kwa ajili ya kukuza uchumi basi ni muhimu kuwa na malengo na mikakati ya kukuza uchumi kupitia hivi tulivyo navyo.
Uturuki ni nchi ndogo sana ukilinganisha na Tanzania, ina zungukwa na bahari mbili tu, Mediteranian sea na Black sea, huku ikiwa na maziwa kadhaa ndani yake, lakini njoo kwetu uangalie Indian Ocean ilivyotamalaki ukanda wa pwani kuanzia Mtwara, Dar, Pwani, na Tanga, liko ziwa Victoria, Tanganyika, Nyasa, na mengine madogo mengi, tunashindwaje kuproduce zaidi ya uturuki.
Sio kesi, lakini ni wakati wa vijana kujivika uzalendo ambao haupo kwenye maandamani wala fujo bali kufanya mabadiliko kwenye nafsi zetu ili kuangalia uendelevu wa tunayoyafanya
Signed
Oedipus