Wavuvi(majangili) wazidi kuuawa hifadhi ya kisiwa cha Rubondo

Lipijema

JF-Expert Member
Mar 8, 2015
809
1,193
Hili si jambo la kuficha. Yapata aidha kipindi cha miezi minne sasa wavuvi wanaoingia kwenye hifadhi ya Rubondo kwa kujipatia kitoweo wanapigwa risasi na kupoteza maisha kila kukicha. Sehemu hizi zinazokizunguka kisiwa hiki cha Rubondo ambazo ni: Izumacheli, Maisome, Ikuza na Mganza, Sasa kumetawaliwa na vijana wengi kupoteza maisha na maiti zao nyingi kutoonekana, wahifadhi doria (gem) hapo mwanzo kabla ya kuanza kampeni ya kuua walikuwa wakiwakamata wavuvi na kuwapeleka mahakamani Geita na hatimaye kufunguliwa mashtaka ya kuingia hifadhi bila kibali na walikuwa wakifugwa kati ya miezi sita hadi miaka mitatu,ila baada ya kuona hiyo adhabu haitoshi kwa sasa ni kupigwa risasi na kupoteza maisha!

Yasemekana ni maiti nyingi mno zilizotapakaa mule ndani ya hifadhi na katu hawaruhusu kuchukua maiti ya nduguyo yeyote yule!

Hapa kisiwani nilipo kuna zaidi ya wavuvi kumi na tano wametoweka kwa jinsi hiyo ikiwa majirani zangu kiasi cha watu wanne hivi ninaowatambua vilivyo, bado maeneo mengineo pia uchache wao awapungui watu mia na ushee!

Tafadhalini sana wavuvi wenzangu tuepuke kuingia ndani ya hifadhi ya Rubondo kwenda kuvua humo eti kwa kufata vilivyo vingi! Tufuate sheria tuvue kwenye uziwa wetu wa uraiani kwa kidogo tupatacho maisha yataenda vyema tu. Kumbuka hii ni awamu ya tano hakuna wa kutusemea!
 
Duh Nimeumia saaana aiseee!! Siku hizi ni mwendo wa risasi Tu
 
Kuingia ndani ya hifadhi kinyume cha sheria ni ujangili na this time hakuna ujangili
 
Uhai wa mtu una thamani hata kama ni jambazi au jangili. Ndio maana tuna katiba na sheria tanzania.
Hebu fanya mawasiliano chap na bbc au dw swahili ili walipe airtime ya kutosha swala hili.
 
Uhai wa mtu una thamani hata kama ni jambazi au jangili. Ndio maana tuna katiba na sheria tanzania.
Hebu fanya mawasiliano chap na bbc au dw swahili ili walipe airtime ya kutosha swala hili.
Tatizo ni maisha ya timing
 
JPM alikua MHALIFU sana, Rais katili kabisa kupata kutokea
Majangali wakishughulikiwa na serikali mnapiga kelele mitandaoni,,

Juzi Boda boda wamevamia ofisi ya serikali ya mtaa na kumchukuwa mwizi wa Boda boda(BONGE) na kutokomea nae kusikojulikana na kumuua,,

Mkawapongeza Boda boda ..

Kweli hasidi hana sababu ya kukuchukia.
 
Raia analipa kodi ambayo inaenda kununua risasi inayokuja kumuua.

Nchi hii, aliye salama ni maiti pekee
 
Back
Top Bottom