Wavulana vinara darasa la Saba

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,072
1,250
WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, imetangaza matokeo ya mitihani ya darasa la saba ambapo jumla ya wanafunzi 478,912 sawa na asilimia 53.51 ya waliofanya mitihani wamefaulu wakiwamo wasichana 222,094 sawa na asilimia 48.29 ya waliofanya mitihani na wavulana ni 256,818 sawa na asilimia 59.02.

Akitangaza matokeo hayo jana, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa alisema, ufaulu wa mwaka 2010 umepanda kwa asilimia 4.1 kutoka 49.41 mwaka 2009 hadi asilimia 53.51 mwaka huu.

Kawambwa alisema, jumla ya wanafunzi 456,350 sawa na asilimia 95.3 ya wanafunzi waliofaulu mitihani ya darasa la saba wamechaguliwa kuingia kidato cha kwanza katika shule za sekondari za serikali ambapo wasichana ni 211,696 na wavulana na 244,654.

Alisema, idadi ya waliochaguliwa kuingia kidato cha kwanza mwaka 2011 ni ongezeko la asilimia 2.3 kutoka wanafunzi 445,954 wa mwaka 2009.

Kwa mujibu wa Kawambwa, wanafunzi 572 wenye ulemavu walifanya mitihani wa kumaliza elimu ya msingi na kati yao 292 wamefaulu wakiwamo wasichana 108 na wavulana 184.

Alifahamisha kuwa watahiniwa 124 kati ya waliofanya mtihani sawa na asilimia 0.01 wakiwamo wasichana 77 na wavulana 47, matokeo yao yamezuiliwa kutokana na tuhuma za kujihusisha na udanganyifu katika mitihani.

Akichambua matokeo ya mitihani kimasomo, Waziri Kawambwa alisema ufaulu katika somo la Kiswahili umeongezeka kutoka asilimia 69.08 mwaka 2009 hadi asilimia 71.02 mwaka huu.

Ufaulu katika somo la Maarifa umepanda kutoka asilimia 59.46 mwaka 2009 hadi asilimia 68.01 mwaka huu, ufaulu wa somo la Kiingereza umepanda kutoka asilimia 35.44 mwaka jana hadi asilimia 36.47 mwaka huu.

Ufaulu katika somo la Hisabati umepanda kutoka asilimia 20.96 mwaka 2009 hadi asilimia 24.70 mwaka 2010 na ufaulu wa somo la sayansi umepanda kutoka asilimia 53.41 mwaka 2009 hadi asilimia 56.05 mwaka huu.

Alisema, ufaulu katika masomo ya hisabati na kiingereza bado hauridhishi hivyo Serikali imeweka mikakati ya kuimarisha ufundishaji wa masomo hayo kwa kutumia mbinu mpya na za kisasa.

Alitaja baadhi ya mikakati hiyo kuwa ni pamoja na kutoa mafunzo ya ualimu sehemu za kazi, kuajiri wataalamu na kubadilisha mfumo wa kufundisha kwa kutumia mbinu za kisasa.

Kawambwa amezihimiza Halmashauri kushirikiana na wadau wa elimu kuandaa mazingira ya kuwapokea wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2011.

Mitihani ya Taifa ya kuhitimu elimu ya msingi ilifanyika Septemba sita na saba mwaka huu ambapo jumla ya wanafunzi 919, 260 wa darasa la saba waliandikishwa kufanya mtihani huo.

Kati yao wasichana 469,846 sawa na asilimia 51.11 na wavulana 449,414 sawa na asilimia 48.89.

Kati ya wanafunzi walioandikishwa watahiniwa 895,013 wakiwamo wasichana 459,889 na wavulana 435,124 sawa na asilimia 97.36 walifanya mtihani huo.
 

Gaijin

JF-Expert Member
Aug 21, 2007
11,817
0
Ina maana kuna watoto 419,305 ambao hawakufaulu kwa mwaka huu. Na kwa kila mwaka tukisema kwa wastani kuwa kuna wanafunzi 400,000 hawafaulu mitihani yao ya darasa la saba. Kwa miaka mitatu tu tayari tunao zaidi ya laki moja waliofeli.

Tuna mpango gani na vijana hawa?
 

Gurta

JF-Expert Member
Sep 17, 2010
2,237
2,000
praimari hamna kufeli bwana, wamekosa tu alama za kutosha
 

Misterdennis

JF-Expert Member
Jun 4, 2007
1,748
1,500
ccm haina policy yoyote kuhusiana na kundi hili la Wtz wanaoishia drs la saba. To ccm these are not Tanzanians.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom