wavulana mkikaa na wanaume jifunzeni kuwa wanaume, mnatia aibu!

kindikinyer leborosier

JF-Expert Member
Jan 6, 2018
430
780
habari!
hivi hili wimbi la wanaume wa kileo mbona kila siku linakuja kwa kasi, mwanzo ilikuwa mijini leo mpaka kijijini unakutana na walamba midomo, wasiopenda kupambana kufanya kazi na walau na focus ya maisha, unakosana na mpenzi wako unalia kama mtoto mwanaume mzima, huwezi hata kuthubutu kidogo kuonyesha wewe ni wa kiume mnatia aibu madogo!

mwanzo ilikuwa nachukulia kawaida, ila ngoja nishushe kisa kidogo walau tujifunze!
mwaka jana mwishoni nilikuwa natoka napoishi naelekea kusaka mkate wa kila siku, basi kwenye gari nikakutana na binti kiukweli alikuwa mzuri tukapiga story mbili tatu nikagundua ni mkweli alimaliza kidato cha nne akafeli, akaamua ajikimu kuuza matunda, walau apate vya kujitegemea!

nilipenda alivyokuwa anajieleza na alivyo mkweli, mwisho wa safari tukabadilishana namba za simu, tukawa tunawasiliana kawaida, sikuwa hata na dhamira ya kumtaka kimapenzi, japo kuna muda alikuwa na mawazo hayo!

kuna siku nikamtembelea anakouzia matunda, ukaribu ukaongezeka nae akawa free sana kunieleza mambo yake!

akanambia ana mpenzi wake hua ana wivu sana, anasomea mambo ya umeme! ila anamvumilia kwani kwa sasa hana uwezo wa kumsaidia ila yeye ndo hua anamsaidia!(hahaha) hivyo kidogo anachopata anagawana nae! sikupenda kudadisi zaidi nikaishia hapo, japo nilimshangaa!!

desemba mwishoni nilipoteza simu naye alibadilisha line tukapotezana, hatimae jumapili ya juzi nikakutana nae alikuwa kachangamka sana, tukasalimiana tuakabadilishana tena namba, usiku akaanza kuniandikia ujumbe akieleza kuwa wanaume wengi sana wanamtongoza ila mimi nipo kitofauti, anapenda kukaa na mimi et anajifunza vingi!

akanijuza kama nina mtaji tufanye walau biashara yeyote pamoja, kumuuliza zaidi mtaji wa mwanzo, kumbe tayari kaufilisi, kwa sasa yupo tuu nyumbani, nilimpa pole nikamwambia mpaka nitafiti kwanza, then nitamjuza! kiharaka nikajua mwanaume anahusika!

kizaazaa kinaanza
juzi jumanne aliniandikia ujumbe saa tano asubuhi, kindi habari za kuamka, kiutani nikamwambia unaamka muda huu?

alinijibu hapana ameamka saa 11 asubuhi, na ndio muda wake wa kuamka kwani anakazi nyingi sana asubuhi.

nikamjibu wewe ni mke mwema!

ukimya ulipita kidogo hatimae ikaja txt karibu nyumbani, nilimjibu karibu kwanza wewe kwani weekend tuu ndo hua nakuwa nyumbani na huo muda natumia kufanya usafi!

kidogo ikaja txt kwa namba mpya, wewe ni nani unachat na V, nilimshangaa halaf sikumjibu, akapiga simu, akaongea kwa jazba akisema kijana punguza dharau nakuuliza we nani mbona hunijibu?

nikamwambia nipo bzy kidogo nitafute baadae! dogo anaropoka tuu! nikawa nasoma txt sijibu, jioni mara mwanamke huyo et anaomba samahani kwa kilichotokea kwani mpenzi wake alimnyang'anya simu na kusoma txt hakuelewa ule ujumbe!

nilimjibu txt moja futa namba zangu, bado mnakua mimi si rika lenu?

akawa anaomba samahani, mara kidogo akaanza kuniambia ujue mambo anayosomea ndo hua yanamchanganya, nilicheka sana!

nikamjibu dogo acha ushamba! unachat na mtu usiemjua nikamtumia business card watsap, akatuma viimoj vya kukodoa macho!

kiukweli aibu niliona mimi,
nawasilisha!
 
Sijaelewa uzi wako una maanisha nini hasa. Unasema hawataki kufanya kazi ilhali umeambiwa jamaa yake anasomea umeme. Kusoma kwake tu inaonyesha jamaa anajielewa. Angekuwa yupo tu kitaa anamtegemea demu mada yako ingekuwa na mantiki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hatari sana hebu pitia Uzi wangu nimeweka utakutana na mwanaume kama huyo!!

don't waste your time on lecturing me, this is 2020
 
tapatalk_1579626488850.jpeg

Unforgetable
 
Hii haina tofauti na yale mashamba ya yanayopatikana pale mufindi iringa ambalo ni CHAGUO LA WATANZANIA
Sehemu ya shamba la Chai. Nyuma ni sehemu ya mlima wa Mulanje, nchini Malawi..jpg
 
Back
Top Bottom