Wauzaji wa bidhaa za forever living mnaboa sana!

Evelyn Salt

JF-Expert Member
Jan 5, 2012
48,782
2,000
Habari za weekend.....

Wauzaji wa bidhaa za forever living, kwanza hongereni kwa kufanya hiyo biashara inayohitaji kipaji cha hali ya juu kuweza kuongea sana na kumshawishi mteja, ni kipaji kwakweli.

Back to topic, mmekua mnatumia mbinu za uongo na kulazimisha sana mteja ili mtangaze biashara aaagrrrr hii mbinu yenu Inakera sana,inaboa sana

Mfano 1: siku za karibuni nikialikwa mahali, nikaambiwa ni semina nauliza semina ya nini nikaambiwa semina tu nihudhurie napigiwa simu za kusisitiza nikaona isiwe tabu ngoja niende nikaahirisha vitu vya muhimu kwenda semina, kumbe ni kwenda nyumbani kwa mtu kuoneshwa bidhaa za forever, wtf? Kwanini umdanganye mtu? Can you imagine nilikua nafeel vipi wakati naoneshwa hizo bidhaa? Mxyu nilikua nimekasirika sana

Mfano 2: dada mmoja kwenye group la whatsapp alitoa mwaliko, jaman karibuni kwangu sehemu flani kuna shughuli, msosi na bia vipo mtakula mtakunywa mtasaza, tunauliza ni nini ubarikio, engagement au nini mchango vipi anakomaa nyie njooni tu eeeh walaji na wanywaji wakaenda eneo la tukio wamevaa suti kumbe ni kuoneshwa bidhaa za forever, Wiki nzima group kimya hakuna anaeongea kumbe watu wamenuna

Mfano 3: Wauzaji wa online, mtu anasema una mtaji wa laki njoo whatsapp tufanye biashara ukiuliza biashara gani unaambiwa njoo whatsapp, unaenda whatsapp anakutumia video la mb 100 kutangaza forever.

Hii ni mifano michache, hivii hamuoni mnakwaza watu? Hakuna mbinu nyingine za kutangaza bidhaa zenu bila uongo??? Au bila kudanganya hamuuzi? Mnakera sanaaaaa
Ni hayo tu
 

Evelyn Salt

JF-Expert Member
Jan 5, 2012
48,782
2,000
mimi waliniita mahali fulani kwa ajili ya semina nauliza semina ya nini naambiwa ni semina ya motivation & inspiration kufika bhana nikaona kuna tickets zimeandaliwa ambazo hazikutaja chochote kuhusu forever living zaidi ya picha za watu wamevaa suti nikajua yeeeess ndo penyewe hapa

akatokea jamaa mmoja akaongea takriban dakika 90 na wala hakuongea kitu chochote kuhusu forever living na kwa kweli aliongea vizuri sana kitu kimoja kilichonifanya nihisi kuna ulaghai ni kabla ya yeye kuanza kuongea aliweka speech ya nani sijui ambayo ilisaidia ku-brainwash watu na kuwaandaa kwa ajili ya kuikubali hiyo forever living

baada ya hizo dk 90 ndo akaanza kuleta masuala ya unene sijui na kuonyesha picha za sehemu za mwili wa binadamu zilizoathiriwa na magonjwa kama tezi dume nk halafu huyooo akafunua koba lake akatoa dawa za forever living aisee nilishikwa na hasira kali nikanyanyuka na kusepa muda huo huo
:D:D:D:D
 

contagious

JF-Expert Member
Jul 14, 2015
531
500
Forever living wanajua kumganda MTU khaaa! Mi pia kuna MTU alikua ananiganda wee....kuona ananiganda sana ...nikataka kujua zaidi kuhusu forever longing coz nilikua naijua tuu kawaida...nikaingia Google nikawanasoma habari zake, katika kusoma nikakutana na mzungu mmoja, yeye yuko forever nae...tukaendelea kuchati kuhusu forever....hapo nikagundua kumbe kuingia forever kumbe mnaandikiana hadi mkataba....akanitumia mkataba ktk ambao watu hupaswa kusaini wakitaka kujiunga forever living....nikausomaa....katika kifungu cha Tisa au kumi if I'm not mistaken kinasema hivi ukijiunga forever living "HUWEZI KUJITOA FOREVER LIVING UNTILL THE EVENT OF DEATH" nikamuuliza kuhusu hichi kifungu akawa nae hana majibu ya kujitosheleza. Nikarudi kwa yule alokua ananiganda nikamuuliza kuhusu hicho kifungu mbongo mwenzangu ( c unajua wabongo tulivyo waongo) akasema hicho kifungu hakipo OK nikamwambia nitumie huo mkataba...akasema atanitumia...mpaka Leo....!! Kwa hiyo tuwaonee huruma wameingia ktk kampuni na kusaini mikataba wasoijua kiundani...mtu huwezi kulazimishwa kukaa mahali ambapo hamna maslah....km MTU ameingia kwa hiari atoke kwa hiari....kwa hyo wanatafuta watu wa kusaini mikataba ya ki- bogus.
KAMA VILE KUINGIA MKATABA NA bayport, UNAJUTA UKITAKA KUTOKA, WALE NAO UNAJISAINISHA KIFO NA NDOA ZA LAZIMA.
 

Evelyn Salt

JF-Expert Member
Jan 5, 2012
48,782
2,000
Au na wewe ni oriflame nn mkuu, niletee lotion, ya dry skin na body spray
:D:D:D:D
Sijawahi kuwaza hizo biashara asee
Kumuuzia mtu wa kawaida lotion ya laki tatu inahitajika ujitoe ufahamu kama watu wa forever living
 

The Messenger

JF-Expert Member
Jul 2, 2014
1,528
2,000
Unawezaje kumshawishi mtu ambaye ujamweka wazi from the beginning ili awe willing kuchakua kusuka au kunyoa?? WTF i hate lies and i hate the way lies do... DAMN IT
 

oyaya karanga

Member
Dec 27, 2015
74
125
Cha ajabu zaidi unakuta mtu ambae ni graduate with fresh thinking nae amefall kwa huu upumbavu.
Yaani nilishangaa kukuta graduate wanne ktk semina pale ACACIA VICTORIA
Ila nikakumbuka uelewa while at college
 

kikaniki

JF-Expert Member
Nov 20, 2014
214
250
Sijawahi kuona watu wa Oriflame wanatumia nguvu hivi na udanganyifu wa hali ya juu.... Sijui asee labda, forever living ni too much
Mimi niliwahi kumla dada mmoja wa forever living. Kila siku alikuwa ananisisitiza nijiunge.

Nikaenda kwake kupata somo, mwisho nikatenda dhambi ya zinaa.
 

Evelyn Salt

JF-Expert Member
Jan 5, 2012
48,782
2,000
Cha ajabu zaidi unakuta mtu ambae ni graduate with fresh thinking nae amefall kwa huu upumbavu.
Yaani nilishangaa kukuta graduate wanne ktk semina pale ACACIA VICTORIA
Ila nikakumbuka uelewa while at college
Hizi biashara zinashusha heshima teh
Jamaa mwingine nae mtu wa maana, yupo kwenye ofisi kubwa tu serikalini nikashangaa siku moja kanitumia video ndeefu kufungua nakuta ni rifaro
Nikajiuliza "hadi huyu"???
Kuna vitu sio vya kufanya asee
 

akenajo

JF-Expert Member
Oct 21, 2012
1,620
2,000
mie kuna dada mmoja wa hizo living product kidogo anigombanishe na mke wangu, asubuhi tuu simu ooh tuna product hizi ,mke wangu akahisi mmhh anaibiwa
 

Danp36

JF-Expert Member
Jul 31, 2010
1,837
1,500
Okay nimekupata.
_____________
Hii ni Gari aina ya Jeep Grand Cherokee ya Kimarekani yenye thamani ya zaidi ya milioni 90 za Kitanznaia mpya kabisa yaani 0 km iliyonunuliwa na dada Huyu Blandina Njau kama wiki sita zilizopita naye anafanya biashara hii ya Forever Living.
kwahiyo biashara yoote kaambulia gari tu?.alafu blandina tu ndio katoka na wengine ambao hawazidi 20%?.
basi probability ya kutoka ni 30% less. Maana blandina kila miaka namsikia na ile jeep yake ?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom