Wauza unga wanaishi maisha ya kifahari jela, wengine wanalala kwao usiku na upelekwa jela kukikucha

Kama anafadhili ofisi ya serikali basi ata rais na waziri watakuwa wanajuwa.
 
Sheria zipo, hili nalo linamsubiri JPM?Akishaondoka je?
Hapo tu! Yaani kuwajibika kwa wasaidizi wa JPM ni kama 0, wao ni mpaka wamsikie anakuja au kutembelea basi utawaona watakavyokuwa busy na kujifanya wako field! Kumbe muda wote ni ndani ya kiyoyozi, ma VX, kunywa chai na kusoma magazeti...Wanamuangusha sana raisi wetu..lakini kwenye luninga na radio utawasikia wanavyojitapa na kujigamba wana vyeti vya usomi vya ajabu! Bure kabisa..
 
Ndiyo Tanzania unavyo ambiwa kwamba hapa wanatupiga changa la moto, wanajuana sana wanatufanya children na
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Kwa hiyo Kamishna anamaanisha nini? Kwamba anayoosha mikono?
Maana naona nae anaanza siasa sasa za makamera, movie na ma likes kwenye media! Kwa nini asi-deal na hizi ishu kimya kimya?
 
Hapo tu! Yaani kuwajibika kwa wasaidizi wa JPM ni kama 0, wao ni mpaka wamsikie anakuja au kutembelea basi utawaona watakavyokuwa busy na kujifanya wako field! Kumbe muda wote ni ndani ya kiyoyozi, ma VX, kunywa chai na kusoma magazeti...Wanamuangusha sana raisi wetu..lakini kwenye luninga na radio utawasikia wanavyojitapa na kujigamba wana vyeti vya usomi vya ajabu! Bure kabisa..
Hii ni ishara akiondoka, mambo yatarudi zaidi ya yale ya zamani, wasaidizi wa JPM ndo hawajui kujiongeza kabisa, wapo busy na media utadhani ni sehem ya majukumu yao, si DCs,RCs,Polisi.....mawaziri ni aibu tu
 
Hii ni ishara akiondoka, mambo yatarudi zaidi ya yale ya zamani, wasaidizi wa JPM ndo hawajui kujiongeza kabisa, wapo busy na media utadhani ni sehem ya majukumu yao, si DCs,RCs,Polisi.....mawaziri ni aibu tu
Kupenda kupewa nyadhifa halafu kukataa kuwajibika, iko ndani ya tamaduni, JPM anahitaji sio chini ya miaka 20 na zaidi kuondoa hizi tabia..Wewe mwenyewe ushaoyaona customers services, ofisi binafsi n.k. Ila kwa kulalamika aise?! Ni hatari, hatupendi kufanya kazi kabisa..Hili swala liko chini ya Magereza, ila ukiuliza watajifanya hawana taarifa, labda ndugu yetu Mwigulu Nchemba aende pale na fagia la chuma..
 
Makonda aliipeleka hii vita kwa style sahihi tukaingiza ujuzi ambao hausaidii sana...Just name and shame...ndio style sahihi....

Kaza buti kamishna...tuletee watuhumiwa tuwajue ili waabike na kote kule wanaposaidia hiyo misaada haramu wawatambue.

Majina yanayotakiwa kufichwa ni yale ya kimkakati tu.
Na hakufanikiwa,labda kumshitaki wema na msokoto wa Bangi
 
Sasa sisi wananchi tufanyeje after kujua kua wanaishi maisha ya kifahari gerezani??
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Na hakufanikiwa,labda kumshitaki wema na msokoto wa Bangi
Ni kweli ilikuwa ni style ya kipekee, labda hakukaa chini kuongea na wajuzi, ila kulikuwa hamna namna, madawa yalianza kuharibu watoto na vijana wetu, huku kwetu uswazi kunatisha, kuna vijana walikuwa hodari sana shule na kwenye shughuli za mtaa sasa ni vibaka tu sababu hiyo, ila sasa tuiboreshe, iwe na meno, iwe na makali, ieweleke kuwa "mzungu wa unga" sio "role model" bali mhalifu kama jambazi au zaidi..
 
HII NI HATARI KUBWA, SERIKALI LAZIMA IING'OWE HII MIZIZI YA WAUZA UNGA. Iit ITEMBELEE MAGEREZA KWA KUSHITUKIZA., WAONDOWE WAKUBWA WA PRISON NA KIFUNGO JUU WOTE WANAOSHRIKIANA NA HAWA WAUWAJI WA TAIFA. HII NI HATARI SANA. ITAKUWA MAFIA YA ITALY KUWATOWA ITAKUWA KAZI, NA SHIDA ZETU NYINGI, NI RAHISI SISI SOTE KUNUNULIWA. SERIKALI IWAFILISI WAKIKUTWA NA HATIYA. MAREKANI INAFANYA HIVYO. CHINA INAWANYONGA AMA LIFE IN PRISON NA KAZI NGUMU. MALI ZAO ZINAWEZA KUCHUNGUZWA HATA KAMA WAMEANDIKA MAJINA YA JAMAA ZAO. UKINIKUTA MIMI MAMANTILIE, SIJAFANYA KAZI MAISHANI YANGU, WALA BIASHARA MALA NA LIJUMBA LA MAMILLIONI, NIFUNGIE CHUMBANI UNIHOJI NITASEMA KILA KITU. DAWA ZA KULEVYA NI HATARI SIO TU KWA WATOTO WETU NI TAIFA ZIMA. WASIPEWE NAFASI KUENDELEA NA BIASHARA HIZI. WOTE TUMUSAIDIE MKURUGENZI HUYU KWA KAZI HII NGUMU.
 
Mi nashangaa watu wanasema kamishna analalamika. Lakini tujue kwamba huko magereza hapamhusu, yeye kazi yake ni kuzuia na kupambana na drugs, kisha mahakama itoe haki na askari magereza 'wadili' na wafungwa.

Hivyo mi sioni kama analalamika ila ni anatoa picha halisi ya kwamba huko kwenye magereza pia kumeoza. In short ni kwamba kuna maafisa ya magereza wapo kwenye payroll ya drug lords
 
Back
Top Bottom