Wauza "unga" wamuweka pabaya KOMBANI | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wauza "unga" wamuweka pabaya KOMBANI

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bajabiri, Aug 21, 2011.

1. B

Bajabiri JF-Expert Member

#1
Aug 21, 2011
Joined: Jan 1, 2011
Messages: 9,755
Likes Received: 27
Trophy Points: 0
Wabunge wametishia kutopitisha bajeti ya mama Celina KOMBANI, Mbunge mmojawapo aliyetoa kitisho hicho ni FELIX MKOSAMALI. Hayo yalijiri jana kwenye semina juu ya vigogo wa madawa ya kulevya.

Wabunge waliijia juu mahakama kwa nini raia wa PAKISTAN waliokamatwa na mzigo mkubwa wa unga waliachiwa kwa dhamana wakat watanzania wanasota ndani? Kutokana na hilo wametaka hakimu awajibishwe na wamependekeza kuwa ifike wakati wauza unga wanyongwe. Mama Komban aliposimama na kutaka kuongea alikumbana na zomeazomea ikabidi Werema aongee na kuahidi kuwa atafuatilia kuhusu hakimu.

Jambo lingine liliotia aibu ni kwa taasisi mbili kubwa za KIDINI hapa nchini ambazo zimetajwa kuwa huwa zinahusika sana na biashara hii, nazo ni BAKWATA na KANISA KATOLIKI. Haya MUFT TUAMBIE KUMBE MKIENDA MAKKA MNAHUSIKA NA KUBEBA UNGA NA PENGO TUNAOMBA MAJIBU YA NZOWA

2. Mtego wa Noti

Mtego wa Noti JF-Expert Member

#2
Aug 21, 2011
Joined: Nov 27, 2010
Messages: 2,229
Likes Received: 133
Trophy Points: 160
hapo kazi ipo.....sasa tumwamini nani katika hii dunia?

3. Kurunzi

Kurunzi JF-Expert Member

#3
Aug 21, 2011
Joined: Jul 31, 2009
Messages: 4,003
Likes Received: 325
Trophy Points: 180
BAKWATA NA KANISA KATOLIKI nimejua kwanini JK alipata kigugumizi du!

4. B

Bajabiri JF-Expert Member

#4
Aug 21, 2011
Joined: Jan 1, 2011
Messages: 9,755
Likes Received: 27
Trophy Points: 0

Hahahahaaaa, kwa nini? au kwa sababu kote kunamgusa kimaslahi,,,,,

5. n

nguluvisonzo JF-Expert Member

#5
Aug 21, 2011
Joined: Dec 27, 2010
Messages: 511
Likes Received: 7
Trophy Points: 35
Ndio maana ma alhaji wengi ni wajanja wajanja(wauza unga) hii ni hatari,maandamano yanahatarisha usalama wa taifa, Mufti vipi ? mlikuwa mnatayarisha mazingira mazuri ya kupitisha unga?JK pole kila anaye kutetea ni muhalifu katika tasnia yake,amakweli nchi imeoza.

6. B

Bajabiri JF-Expert Member

#6
Aug 21, 2011
Joined: Jan 1, 2011
Messages: 9,755
Likes Received: 27
Trophy Points: 0
Nimehuzunishwa sana na stori hii,hasa kwa taasisi yangu ya kidini BAKWATA,ndio maana jk alipoongea walinyamaza kimyaaaa,

7. Njowepo

Njowepo JF-Expert Member

#7
Aug 21, 2011
Joined: Feb 26, 2008
Messages: 9,297
Likes Received: 381
Trophy Points: 180
Ni zama za serikali legelege ndo maana yote hayo yanafanyika na hakuna wa kuchukuliwa hatua

8. JoJiPoJi

JoJiPoJi JF-Expert Member

#8
Aug 21, 2011
Joined: Aug 8, 2009
Messages: 2,458
Likes Received: 1,331
Trophy Points: 280
Sidhani taasisi kama bakwata inahusika na biashara ya madawa ya kulevya, ila inawezekana kuna watu ndani ya taasisi wanahusika(binafsi) na biashara, serikali iwashughulikie na sio ijumuishe Taasisi nzima

9. Gamaha

Gamaha JF-Expert Member

#9
Aug 21, 2011
Joined: Jul 17, 2008
Messages: 2,695
Likes Received: 752
Trophy Points: 280
Nakubaliana na wewe Mkuu

10. B

Bajabiri JF-Expert Member

#10
Aug 21, 2011
Joined: Jan 1, 2011
Messages: 9,755
Likes Received: 27
Trophy Points: 0
Hata NZOWA ndivyo alivyosema,kuwa baadhi ya watu wa BAKWATA,ila serikali mechelewa sana

11. f

fukunyungu JF-Expert Member

#11
Aug 21, 2011
Joined: May 16, 2011
Messages: 726
Likes Received: 29
Trophy Points: 45
dini zote ni sawa! Ili mradi kufuata misingi ya dini yake!weka pembeni dini za shetani.

12. Lokissa

Lokissa JF-Expert Member

#12
Aug 21, 2011
Joined: Nov 20, 2010
Messages: 7,079
Likes Received: 154
Trophy Points: 160
rpiort ya Nzowa ni ya kitoto kabisa, huwezi kusema vijana wachache walioenda kwenye kongaMano
huko AustriA ndio kanisa katoliki.unapozungumzia kanisa au usilamu lazima uonyeshe uhusika
kwa viongozi wa hayo madhehebu kama padri,askofu au shekhe.sasa vijana 2 au wahujaji wawili
waliojipachika ktk safari za kuhiji ndio uhusishe bakwata na kanisa katoliki kwa ujumla?

hata mtoto wa grade 1 hawezi kuamini huu upuuzi.kwa nn asiwataje hao viongozi
wakubwa wanaohusika na hii biashara? sii anawaogopa????

kuhusu hakimu kama aliwapa dhamana na upande wa mashtaka haujachukua hatua yoyote
kupinga rufaa hiyo mahakama kuu basi inawezekana mnamlaumu bure hakimu badala ya kulaumu
serikali yenyewe kwani mashtaka yanapofunguliwa mahakamani huwa DPP ana nguvu kisheria

kuliondoa shtaka lile mahakamani mda wowote na hakimu hana namna ya kukataa bali kutangaza
kesi imefutwa kwa vile upande wa mashtaka hauna nia ya kuendelea na kesi tajwa,
WANAJF jueni kuwa hakuna ofisi inayonuka rushwa kama ofisi ya DPP.wale wakishapewa
million 50 unadhani ni wajinga waendelee na kesi wkt hela zipo???
kesi nyingi tu hata za mauaji ukifika kwa
DPP ukatoa vijisent fasta utaandikiwa NOLE kuwa DPP hana nia ya kukuishtaki tena ktk kesi hiyo ya mauaji,,,,,,,,,,,, rushwa rushwa.....
.la pili hakimu hawezi kuwajibishwa kwa vile wanalindwa na sheria(wana immunity)
hata kama katoa hukumu isiyo halali..la msingi hapa serikali hiyo hiyo inayojifanya kuwatafuta wauza madawa ndio hiyo hiyo inayouza hayo madawa..waanze kujitaja kwanza,,,,kama umesoma habari ya nzowa yeye kasema analindwa na zaburi kwnai kazi yake ngumu.

13. B

Bajabiri JF-Expert Member

#13
Aug 21, 2011
Joined: Jan 1, 2011
Messages: 9,755
Likes Received: 27
Trophy Points: 0
Lokissa umenena point za msing sana,,,,,,DPP NA TAKUKURU,ni mavi ya bata

14. gwino

gwino JF-Expert Member

#14
Aug 21, 2011
Joined: Nov 19, 2010
Messages: 335
Likes Received: 1
Trophy Points: 35
tumaini langu Tz ya leo siri zote ziko hadharani ingawa viongozi wanazani hatujui kinachooendelea dhid yao pamoja na ubabaishaji wao

15. B

Bajabiri JF-Expert Member

#15
Aug 21, 2011
Joined: Jan 1, 2011
Messages: 9,755
Likes Received: 27
Trophy Points: 0

na zitaendele kumwagika tu,maana kitunza siri kimetoboka watawala wanawaza kimasaburi zaidi

16. mikatabafeki

mikatabafeki JF-Expert Member

#16
Aug 21, 2011
Joined: Dec 29, 2010
Messages: 12,837
Likes Received: 2,101
Trophy Points: 280
lakin hao waliotajwa kwenye orodha bdo ni vidagaaa tu kuna mapapa behind ambao wanatunziwa siri tu

17. Mamndenyi

Mamndenyi JF-Expert Member

#17
Aug 21, 2011
Joined: Apr 11, 2011
Messages: 29,062
Likes Received: 6,513
Trophy Points: 280
wenye uwezo wa kupata huo mkanda waliouonyesha bungeni jana watuwekee ili tumshike mchawi wa taifa letu.

18. K

KANAN Senior Member

#18
Aug 21, 2011
Joined: Aug 20, 2011
Messages: 124
Likes Received: 33
Trophy Points: 45
Maoni yangu viƶngoz wa serikal wawe makin sana wanavyo toa maoni yao hasa yanayohuru hisia za watu...as a great thnker ni hayo tu.

19. Kiby

Kiby JF-Expert Member

#19
Aug 21, 2011
Joined: Nov 16, 2009
Messages: 5,202
Likes Received: 1,007
Trophy Points: 280
Ile ripoti ni ya kitoto sana, hata mwalimu wa chekechea ana upeo wa kutoa ripoti ya watoto darasani mwake kwa upeo kuliko hii ya nzovwa. Huu ndio ubaya ya usanii.

20. Ngambo Ngali

Ngambo Ngali JF-Expert Member

#20
Aug 21, 2011
Joined: Apr 17, 2009
Messages: 3,194
Likes Received: 134
Trophy Points: 160
Sikutegemea Wabunge watoe mawazo kuwa jaji aliyetoa dhamana eti anyongwe, hivi kweli wabunge mpaka leo hawajui kuwa Hakimu akikosea hakuna hatua anayoweza kuchukuliwa kwa ajili hiyo?

Polisi more so Kikosi cha kuzuia madawa ya kulevya wamekaa kisanii sana kuliko kikazi, was the seminar kwa wabunge necessary? was it necessary tro show a video clip of the said suspects.

Nzowa na mwenzio fanyeni kazi acheni usanii.

Loading...