Wauza pombe za kienyeji waanzishe viwanda sasa

Ta Muganyizi

R I P
Oct 19, 2010
5,355
2,736
Muda huu hakuna viroba wala bange. Kupata steam imekuwa kazi kweli kweli. Vijana wameona isiwe shida. Wamehamia kwenye pombe za kienyeji, wa kule Sumbawanga wanagonga Sekenke na Msimamishe kwa kwenda mbele. Mikoa mingine wanzuki, Kindi na Komoni hasa usukumani huku imepanda chati. Wengine Lubisi na Mnanasi almaarufu kama (Mna) ndo usiseme. Ukipishana na vijana harufu zao ni kama umepishana na madumu ya pombe kumbe ni binadamu.

Tatizo kubwa ni usafi wa hizo pombe. Hygiene ya pombe hizo ni shida sana. Kuharisha baada ya kunywa ni kawaida sana. Vijana ambao ndo nguvu kazi ya taifa tunaodhani tumewasaidia itafikia wakati hata debe mbili hawawezi kubeba.

Wauzaji hawa washauriwe wafanye packing kama ile Chibuku. Nilikuwa kijiji flani kanda ya ziwa Chibuku ile ya kwenye kiroba kikubwa imeshika chati. Naomba iwepo formal packing ya Komoni, wanzuki, Msimamishe, kindi, Ulanzi, Lubisi, Mnanasi, Sekenke, ili steam isiwe walau na madhara mengine. Mnaweza msinielewe sasa hivi ila pombe za kienyeji zimepanda chati sana na hazina viwango jamani. Maana nafaka za kutengeneza hizo pombe zimekuwa ghali na shida, sasa kuna vitu kibao vinawekwa ili alcohol iwe kali..............mkisikia gongo la mavi mfano msidhani ni hadithi.

Ni hayo tu.
 
Back
Top Bottom