Wauza dawa za kulevya waja na stahili mpya kali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wauza dawa za kulevya waja na stahili mpya kali

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by engmtolera, Jan 25, 2012.

 1. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #1
  Jan 25, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  [TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]
  WAUZAJI wakubwa wa dawa za kulevya nchini, wamekuja na mbinu mpya ya kuingiza biashara hiyo haramu nchini, Tanzania Daima Jumatano limebaini.
  Katika mbinu hiyo, wafanyabiashara hao hujifanya wasamaria wema kwa kuamua kugharimia matibabu ya wagonjwa walio na hali mbaya kiasi cha kupoteza matumaini na kuwasafirisha kwenda nchini India kwa matibabu, huku wakijua fika kwamba hawawezi kupona.
  Imeelezwa kuwa baada ya kufika India na mgonjwa kufariki akiwa hospitali, hujitolea kugharamia kurejesha mwili ukiwa umebebeshwa shehena ya dawa za kulevya tumboni.
  Hivi karibuni, gazeti hili lilifuatilia kwa kina nyendo za mwili wa kijana mmoja aliyefariki katika hospitali moja nchini India ikiwa ni siku mbili tu baada ya kuwasili katika hospitali hiyo.
  Vyanzo vyetu vya habari vilisema kuwa kijana huyo (jina limehifadhiwa) ambaye alikuwa maarufu kwa uuzaji wa simu za mikononi katika eneo la Posta, alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya figo kwa muda mrefu.
  Inaelezwa kuwa baada ya kutibiwa katika hospitali mbalimbali na kupoteza matumaini ya kuishi, alirejea nyumbani, huku ndugu zake wakiwa wamekata tamaa ya kumponyesha ndugu yao.
  “Madaktari walisema kabisa mgonjwa wetu asingepona. Lakini walikuja watu waliojifanya wasamaria wema na kuomba wamsafirishe kwenda India kwa matibabu,” alisema mmoja wa ndugu wa karibu wa kijana huyo.
  Kwa mujibu wa habari hizo, kijana huyo alisafirishwa hadi India Jumatatu iliyopita na kufariki siku ya Jumanne.
  “Kwanza alisafirishwa bila ndugu, lakini tulipata taarifa za kifo chake siku moja tu baada ya kuwasili katika hospitali hiyo. Mwili wake ulirejeshwa Ijumaa iliyopita na ulizikwa siku hiyohiyo katika makaburi ya Kinondoni,” kilisema chanzo chetu cha habari.
  Habari hizo zilisema kuwa mwili wa marehemu ulipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere, ulikaa kwa muda mfupi na baadaye kusafirishwa kwa gari la wagonjwa kwenda katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, ukisindikizwa na pikipiki maalum ya polisi.
  Mwili huo ulipowasili katika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, ulihifadhiwa kwa takriban saa mbili na hakuna ndugu aliyeruhusiwa kuuona mwili wa marehemu.
  “Pale Muhimbili ndugu walizuiliwa kabisa kuuona mwili hadi baadaye waliitwa ndugu wachache pamoja na mama wa marehemu ambao waliruhusiwa kuiona sura na kuthibitisha kuwa ni mwili wa ndugu yao.
  Baada ya hapo ulifugwa tena kwenye sanduku maalumu walilokuja nalo na kwenda moja kwa moja makaburini,” alisema mtoa habari wetu.
  Kwa mujibu wa habari hizo, gharama za kununua eneo la mazishi na nyingine zote, zilifanywa na wasamaria wema hao na baadaye kumpatia mama wa marehemu ubani wa sh milioni mbili.
  Siri kwamba mwili wa marehemu huyo ulibebeshwa shehena ya dawa za kulevya, ilitolewa na mmoja wa wafanyakazi wa chumba cha kuhifadhia maiti ambaye alimjulisha mmoja wa ndugu wa marehemu kwamba tumbo la ndugu yao liliondolewa kila kitu ili kuhifadhi dawa hizo za kulevya.
  Kamanda wa polisi wa kupambana na dawa za kulevya nchini, Godfred Nzowa, akizungumza na gazeti hili, alisema hiyo ni staili mpya kutumiwa na wafanyabiashara hao, lakini kwao inaweza kuwa ni staili ya zamani.
  “Hii ni mbinu mpya na kali maana ndiyo kwanza naisikia. Moja ya changamoto tunayokutana nayo katika vita hii ni mbinu mpya zinazotumika kuingiza biashara hii haramu nchini.
  “Unapotoka na mgonjwa kwenda nje kwa matibabu, unakuwa na nyaraka zake zote, hivyo urejeshwaji wa mwili wake kama atafariki, unakuwa na urahisi hasa kama chanzo cha kifo chake kinajulikana, ndio maana mbinu hiyo ni rahisi kuliko ile ya kuja na mwili ambao haujulikani mgonjwa alifariki kwa sababu gani,” alisema Nzowa.
  Kamanda Nzowa aliwataka wananchi kutoa ushirikiano hasa kama kuna mtu alisafirishwa kwa matibabu nje katika mazingira ya aina hii na kurejeshwa.
  Alisema kikosi chake kinalifanyia uchunguzi tukio hilo na kusisitiza kuwa wananchi wanapaswa kutoa ushirikiano kukabiliana na vita hii

  tanzania daima  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #2
  Jan 25, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,061
  Likes Received: 5,552
  Trophy Points: 280
  mkuuu hizo kelele tu unafikiri mh nzowa ajui kinachoendelea
  loh polen wafiwa ndio hivyo kufa kufaaanaa tutafanyaje bana
   
 3. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #3
  Jan 25, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  tena tunaelezwa kuwa mwili ulisindikizwa kwenda muhimbili kwa pikipiki maalum ya polisi,je hiyo maiti ilikuwa ni ya waziri? ama ilikuwa ya jeshi? ama ilikuwa ya polisi? ama ilikuwaje?
  hapo ndipo tunachoka kabisaaaaaa
   
 4. taffu69

  taffu69 JF-Expert Member

  #4
  Jan 25, 2012
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  [h=1]Staili ya kutumia miili ya marehemu ilitumika siku nyingi sana sio kwa madawa ya kulevya tu bali pia kwenye usafirishaji wa silaha.

  Angalia staili nyingine inayotumika sasa na nafikiri wengi bado hawajashtukia njia hii.....

  Woman caught smuggling 1.5kg of cocaine in her DREADLOCKS on flight to Bangkok[/h]
  • The smuggled cocaine had a street value of £93,000
  • Nolubabalo, 23, was hired as a drug mule for £1,200
  • Judges in Thailand can impose the death penalty for drug traffickers

  By Stewart Maclean
  [updated]
  A woman was caught trying to smuggle 1.5 kilograms of cocaine in her dreadlocks on a flight to Bangkok, it was reported today.

  South African Nobanda Nolubabalo, 23, was arrested and held in Thailand's capital yesterday after customs officers allegedly noticed a suspicious white substance in her hair.

  Officials later carried out a search and discovered she had allegedly matted the Class A drug into her dreadlocks before boarding a flight from Brazil.
  SCROLL DOWN FOR VIDEO


  [​IMG] Arrested: South African Nobanda Nolubabalo held at customs in Bangkok as police check her dreadlocks

  Thailand's Bangkok Post reported that the smuggled cocaine had a street value of £93,000 (4.5 million baht).

  The newspaper reported: 'Authorities found something unusual about her dreadlocks.[related]
  'A search found traces of white substance which turned out to be cocaine.

  'A total of 1.5kg of cocaine was found hidden in her hair.'
  Nolubabalo was today being held in custody after being held at Bangkok's international Suvarnabhumi Airport as she disembarked a Qatar Airways flight which had come from Sao Paolo via Doha.

  [​IMG] Testing: Officials carried out a search and discovered she had allegedly matted the Class A drug into her dreadlocks


  [​IMG] The evidence: Officials laid the cocaine matted dreadlocks on a table in Bangkok customs for testing  The Bangkok Post reported that the suspect had allegedly admitted trying to smuggle the drug and claimed she had done so after being hired to work as a drug mule by a Thailand-based businessman for £1,200 (60,000 baht).
  Thailand has some of the toughest anti-drugs laws on the planet, with judges permitted to impose the death penalty for traffickers.

  The South African's arrest follows the execution of another South African citizen this week for drug smuggling in China.

  Janice Linden, 38, was killed by lethal injection on Monday after she was caught in November 2008 trying to smuggle 3kg of crystal meth into the southern Chinese city of Guangzhou.

  South Africa's president Jacob Zuma appealed unsuccessfully to the Chinese government to commute the sentence before she was put to death in prison.

  [​IMG] Tough law: Thailand has some of the toughest anti-drugs laws on the planet, with judges permitted to impose the death penalty for traffickers  [​IMG] Drug mule: The South African woman was only paid £1,200 to smuggle the cocaine, which had a street value of £93,000
  Source: Woman caught smuggling 1.5kg of cocaine in her dreadlocks on flight to Bangkok | Mail Online
   
 5. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #5
  Jan 25, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145

  mmmmmh

  hii kali mkuu na inavyo onekana hawa madada wa SA ni kiboko sana kwa kusafirisha madawa
   
 6. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #6
  Jan 25, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  mkuu hii taarifa yako ina mapungufu mengi na pia inautata, mimi nimeikataa kwa 100% ni kama story fulani hivi za vijiweni au mabaraza ya kahawa anyway hao ndio waandishi wetu wa habari wa tanzania hahaha waandishi makanjanja.NIMEIKATAAAAAAAAAAAAAAA
   
 7. Kaliua urambo

  Kaliua urambo JF-Expert Member

  #7
  Jan 25, 2012
  Joined: Apr 21, 2009
  Messages: 606
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Arabuni wananyongwa
   
 8. Tripo9

  Tripo9 JF-Expert Member

  #8
  Jan 25, 2012
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 2,167
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Same word twice?!!! Kweli UMEIKATAA
   
 9. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #9
  Jan 25, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Kushindana na wauza unga ni ishu!
  Cjui wanaokamatwa kesi huishia wapi?ni kweli huwa wanahukumiwa?
   
 10. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #10
  Jan 25, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 933
  Trophy Points: 280
  Hii vita ni ngumu, tena ngumu haswaa.
  Wanaoingiza mzigo ni viongozi wa nchi na washirika wao.
  Nasema hivyo kwa sababu endapo teja mdogo wa Mkwajuni akibanwa vizuri, atataja aliyemuuzia, aliyemuuzia rejareja akibanwa vizuri atamtaja wholesale dealer, huyu nae akibanwa vizuri atamtaja anaeingiza mzigo.
  Kumpata teja mwandamizi wa ngazi ya chini si tatizo kubwa,
  whats wrong sasa? Huu ni ukweli mchungu...
   
 11. mkomatembo

  mkomatembo JF-Expert Member

  #11
  Jan 25, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 1,466
  Likes Received: 502
  Trophy Points: 280
  Nimechoooooka ! dah ! hata sijui wazuie vipi hili balaa ! jamani ndugu zetu wanaisha kwa hilijanga ! eee Mola
   
 12. mkomatembo

  mkomatembo JF-Expert Member

  #12
  Jan 25, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 1,466
  Likes Received: 502
  Trophy Points: 280
  Samahi mkuu hebu tueleze nasisi tujue umeikataa kwa vipi maana wengine hatuoni mbali!
   
 13. Muuza Sura

  Muuza Sura JF-Expert Member

  #13
  Jan 25, 2012
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 1,990
  Likes Received: 218
  Trophy Points: 160
  style ni zilezile hamna mpya!kipya ni kuongeza mpunga wa kuhonga sehemu nyeti ili mzigo upite kilaini
   
 14. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #14
  Jan 25, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Hivi yule mama Mkenya aliyepigwa marufuku na Obama na baadae kukamatwa na madawa ya kulevya Dar es Salaam kesi yake imekwishaje? Mara nyingi watu wakikamatwa na haya madawa ya kulevya magazeti yanashabikia sana lakini hawafuatilii kujua hatma ya hizi kesi; sintashangaa kama yule mama ameishaachiwa na amerudi kwao Kenya!
   
 15. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #15
  Jan 25, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 59
  Trophy Points: 145
  Hizo mbinu zote mbili hapo juu ya maiti na ya rasta ni za waganga njaa tu,kamanda Nzowa anajua unga ule wa tani kadhaa unavyoingia nchini kwa njia ya bahari,ndio maana mnasikia habari ya sehemu zinazopakana na bahari kama lindi,mtwara bagamoyo kukamatwa madawa ya kulevya ya thamani ya mabilioni,juzi mmsikia habari ya bilioni tisa hapa,nani mwenye tumbo la kubeba mzigo wa bilioni tisa hapa?unga unaingizwa nchini kwa njia ya majahazi,hawa wa kubeba mzigo tumboni ni waganga njaa wa vimilioni 60 mpaka 80.............
   
 16. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #16
  Jan 25, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  habari kama hizi mwandishi anatakiwa azifanyie utafiti wa kina, mahojiano ya kina na ndugu kuhusu yote yaliyotokea tangu mwili uwasili dar, hivi inaingia akilini kweli ndugu yenu amekufa halafu wanandugu hamruhusiwi kumuona tena na mtu baki? baada ya masaa mawili walikwenda kuzika inamaana hata kanisani/msikitini hawakumpeleka? taratibu za dini gani hizi? au alikufa kwa kipindupindu.

  Na kawaida kukitokea hali ya utata hata kama mwili umezikwa wiki utakwenda kufukuliwa na kufanyiwa tena postmoterm na huyo ndugu aliyeambiwa na mtu wa mortuary kuwa vitu vya ndani vyote vilitolewa (moja kwa moja wote walikuwa eneo la tukio hapo muhimbili) alichukua uamuzi gani baada ya taarifa hizo?.. tunaweza kufumua mengi sana hapa kuhusu hawa waandishi wetu makanjanja wa udaku.

  na pia siku hizi kusafirisha madawa kwa kutumia mwili ni ngumu sana kupenya ni bora uyameze au utumie njia nyingine
   
Loading...