Wauwaji wa RPC wakikamatwa na wauwaji wa Makada wa Chadema wakamatwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wauwaji wa RPC wakikamatwa na wauwaji wa Makada wa Chadema wakamatwe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Wimana, Oct 15, 2012.

 1. W

  Wimana JF-Expert Member

  #1
  Oct 15, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 2,453
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 145
  Waziri Lukuvi amenukuliwa na Mwananchi leo kuwa Serikali itahakikisha wauwaji wa Kamanda RPC Barlow wanakamatwa. Kauli yake imenifariji sana na inaonyesha kuwa inao uwezo na itautumia kuwashika wauwaji hao.
  Hata hivyo, napenda kutahadharisha kuwa kukamatwa kwa wauwaji hao na kushindwa kuwakamata wauwaji wa Makada wa CDM; Mbwana Masudi na Msafiri Mbwambo kwenye chaguzi ndogo za Igunga na Arumeru Mashariki kunaweza kuleta tafsiri ya kuwa kuna baadhi ya Watanzania uhai wao una thamani kuliko wengine.
   
 2. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #2
  Oct 15, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Je mwalimu Doroth alishawahi kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na mmoja wapo wa vigogo wa nchi hii??

  hili ni swali muhimu kwa wapelelezi wetu huko mwanza.Isije ikawa wanatwanga maji kwenye kinu.
   
 3. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #3
  Oct 15, 2012
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Wimana,
  Inavyoonekana ni kweli kuna uhai una thamani kuliko wa wageni. Kwa mfano kuwa tukio la vijana wawili, Ewald Mtui na Shadrack Motika (Mwenyezi Mungu awaweke pema) waliuawa na polisi pale Arusha. Hadi sasa wauaji hawajapelekwa mbele ya vyombo vya sheria pamoja kulikuwa na tume/kamati zimefanyia kazi tukio hilo.
  Rejea: Home
   
 4. Mystery

  Mystery JF Gold Member

  #4
  Oct 15, 2012
  Joined: Mar 8, 2012
  Messages: 7,950
  Likes Received: 6,711
  Trophy Points: 280
  Kwani ulikuwa hujui kuwa haki ya kuishi hapa nchini ipo kwa wakubwa tu, na wanyonge wanastahili kuuawa kama kuku? Hebu jiulize maswali machache, alipouawa Ally Zona pale Morogoro na Daudi Mwangosi huko Nyololo, Iringa. Hatukuwahi kusikia kauli za kujiapiza za wakuu wa polisi kutamka kuwa watawatafuta wauaji kwa nguvu zote hadi ikibidi kutumia Interpol, badala yake ikaundwa kamati 'miyeyusho' ya Jaji Ihema, ambayo imetoa matokeo ambayo hata ukimpa mtoto mchanga atajua ni ya kupikwa! Sasa kauawa RPC,ndiyo tunaambiwa hata Interpol itatumika kuwasaka wauaji kokote kule hata kama ni nje ya mipaka yetu, hiyo ni dhahiri kuna double standards za utendaji wa polisi. Ingawa kuna utata mkubwa ya mauaji wa RPC huyo, ambaye inasemekana alikuwa akimrejesha 'mtu wake' nyumbani saa 8 usiku, wakitoka kwenye kikao cha harusi! Usije kushangaa watuhumiwa wote watakaokamatwa wakawa wafuasi wa CDM, na mauaji hayo wakayahusisha na mambo ya siasa! Mambo yanayofanyika TZ hivi sasa, yanaweza kuifanya Tanzania yenyewe iwe miongoni ya maajabu saba ya Dunia!!
   
 5. real thinker

  real thinker Senior Member

  #5
  Oct 15, 2012
  Joined: Jun 24, 2012
  Messages: 119
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Barlow ni binadamu kama wengine nae anastahili kufa mbona tumeona watu wengi wamekufa kwa utata kama vile mwangosi na profesa mwaikasa hawajaapa kuwatafuta wauaji? Au kwa vile yeye alikuwa policcm?
   
 6. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #6
  Oct 15, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Kwani RPC siyo kigogo wa nchi hii?

  Issue ni kwamba mpaka sasa wameshakamatwa watu 13 kuhusiana na mauaji ya RPC, waliwashambulia wabunge wa chadema walifanya kitendo hicho mbele ya jeshi la polisi wakaondoka mpaka sasa hawajakamatwa, na hawana mpango wa kuwasaka.

  Mwenye haki ya kuishi Tanzania chini ya uongozi wa rais kikwete ni wakubwa tu. wengine tuliobaki hatuna haki ya kuishi.
   
 7. W

  Wakwe2 Member

  #7
  Oct 15, 2012
  Joined: Sep 28, 2012
  Messages: 91
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Gape limeanza kuonekana baina ya wakubwa na masikini wakubwa wanathaminiwa wakipata tatizo wao ndo wanafill pinch na vyombo vya habari vitatangaza mchana /usiku kuchwa mifano mingi tunaiona mahospitali dawa hakuna vitendea kazi hamna magari ya kubeba wagonjwa hakuna ila mkubwa akiumwa ndege itakodishwa mtu arushwe kwenda nnje sasa sijui kama hao interpole wakija huyo RPC atafufuka au itakuwaje VIONGOZI JIREKEBISHENI ACHENI MAMBO YA AJABU KUMBUKENI SISI MNAOTUTESA NDIO TUNAOLIPA KODI
   
 8. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #8
  Oct 15, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Polisi wamevuna walichopanda.
  Tanzania nzima inalia kwa misiba iliyotokana na uzembe wa polisi.
   
 9. TOWNSEND

  TOWNSEND JF-Expert Member

  #9
  Oct 15, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,597
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  kweli tz inamaajabu sana kwa umri wangu nimetembea dunia lakini sijawahi ona mahali popote police wapo kazini mchana au usiku lakini wanacheza karata lindoni bunduki wameegemeza ukutani

   
 10. M

  Mzee Mukaruka JF-Expert Member

  #10
  Oct 15, 2012
  Joined: Jun 18, 2012
  Messages: 254
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 45
  Haya haya kumekucha! Tusubiri tuone nguvu itakayotumika katika kuwasaka wauaji wa Kamanda Libe. Labda kifo hiki kitawakumbusha kuwa hata wao - vigogo - ni vulnerable na siyo invincible when it comes to "vitu vigumu". All the best in the hunt for wauaji wa mpendwa kamanda wetu Libe!
   
 11. S

  Sunga Member

  #11
  Oct 15, 2012
  Joined: Mar 22, 2012
  Messages: 89
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 15
  sawa wata wapata kwani wao ni dola na kazi yao ni kulinda dola na wala siyo mwangosi wala wa hanga wa chadema!
   
 12. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #12
  Oct 15, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Tatizo ni kwamba hata wakikamatwa, wanaachiwa tena! Si uliona watuhumiwa wa mauaji ya m/kiti wa cdm usa river walivyotoroka katika katika mazingira ya kutatanisha!?
   
 13. KIJOME

  KIJOME JF-Expert Member

  #13
  Oct 15, 2012
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 3,079
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Hii laana itawatafuna na bado wallah,raia ni wengi wanaolia kwa kuuwawa kwa dhuluma na policcm sijamuona Lukuvi na vibaraka wengine mapovu yakiwatoka kama kwenye issue hii iliyowakuta wao wanaojifanya miungu watu...ee Mwenyezi Mungu wetu mwingi wa rehema hakika ni wewe tu mwenye haki...
   
 14. K

  Kifarutz JF-Expert Member

  #14
  Oct 15, 2012
  Joined: Aug 7, 2012
  Messages: 1,694
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hii imekaa njema, Mwangosi aliuawa kwa bomu mbele ya RPC wakakamata mtu 1 tu. RPC akauliwa pasipo kuwepo mashuhuda wamekamata watu 13. Hiki ni kichekesho cha hali ya juu
   
Loading...