Elections 2010 Waungwana sharif kanunuliwa zanzibar au katishwa?

mwalimumpole

Member
Oct 17, 2010
48
0
NIMEFUATILIA KWA KARIBU MNO KAMPENI NA MCHAKACHO MZIMA WA UCHAGUZI ZANZIBAR, KWA MARA YA KWANZA CUF WAMEIBOMOA PAKUBWA NGOME YA CCM UNGUJA. TAFSIRI YAKE KUWA USHINDI KWA CUF ULIKUWA DHAHILI, SASA NAJIULIZA SHARIF AMEKUBALI MUSTAKABALI WA ZANZIBAR ZAIDI KULIKO USHINDI WAKE?:israel:
 
Sharif kukubali matokeo kiulaini zenji kunaitia kichwa kuuma CCM. Unajua kwa waliopo huko wazenziberi ni wamoja sana. Tunaowasumbua ni wabara na sera zetu za ukandamizaji. Nawatakia watu wa zenji mstakabali mwema katika kuijenga nchi yao
 
Kala mshiko huyu Maalimu, kwa asilimia 1 tofauti na jambo gumu sana kukubali kirahisi sana, ila tuwaachie wenyewe nasi tupange jinsi CHADEMA kitakavyojulikana sana Zenji ambako tunakosa kura za urais.
 
I think Zenji ngoma ndio imeanza, tena ya kukesha kama mlimsikiliza Maalim vizuri nakusoma body language pia
 
Jamani mimi si utani nikiangalia sana chama cha CUF nashindwa kuelewa
1. Hivi kulikuwa na haja gani kwa Sherrif kugombea tena ZNZ, hivi kwanini wasingebadili wagombea, kuna vichwa vingi tu ambavyo vingeleta mabadiriko, ndo maana hata Pemba kura hazikuwa nyingi, watu wanataka mabadiriko. Kuna jamaa yule alikuwa kiongozi wa upinzania bungeni Hamad Rashid angesaidia sana

2. Bara - Lipumba almegombea kwanini? Rais angekuwa mwingine hata Juma Haji Duni au mwingine

Kwa mtazamo wangu kukubali kiraihisi kwa Seif ni uroho tu wa madaraka, alitaka sana kuwa rais wa Zanzibar bila kuangalia kingine chochote..:A S angry: wamenisikitisha sana
Ni mtazamo wangu mimi
 
mtazamo wangu naona kaweka maslahi ya taifa mbele. halafu tujiulize hivi angesema mimi ndie nimeshinda ccm na zec yao wangekubali? bila shaka wasingekubali na matokeo yake wananchi wangeuana na shein bado angekuwa rais cuf wasingemtambua na na kila kitu wangepoteza kama ambavyo iliwahi kutokea. Ninachoona Cuf kwa kukubali kwao wamejipa nafasi ya kushiriki katika serikali wataunda tume huru ambayo itakuwa na mchanganyiko na mungu akipenda 2015 watapita kiulaniiiiiiiiiiii. Hongera Cuf Hongera Mzee wa sawasawa
 
mtazamo wangu naona kaweka maslahi ya taifa mbele. halafu tujiulize hivi angesema mimi ndie nimeshinda ccm na zec yao wangekubali? bila shaka wasingekubali na matokeo yake wananchi wangeuana na shein bado angekuwa rais cuf wasingemtambua na na kila kitu wangepoteza kama ambavyo iliwahi kutokea. Ninachoona Cuf kwa kukubali kwao wamejipa nafasi ya kushiriki katika serikali wataunda tume huru ambayo itakuwa na mchanganyiko na mungu akipenda 2015 watapita kiulaniiiiiiiiiiii. Hongera Cuf Hongera Mzee wa sawasawa

Mimi nimesikia tetesi kwamba Mzee wa Ukweli na Uwizi na Mzee Ruksa walikuwa pale Bwawani wakawaita Mzee wa Sawasawa na ZEC mbele ya Shein na kuwaambia kuwa haiwezekani Shein asiwe rais kwani Zanzibar itaacha kuongozwa na CCM wakati bara itakuwa bado chini ya CCM; sasa Muungano utakuwaje ikiwa Zenj ni CUF na bara ni CCM?

Kwa hiyo mnaona jinsi hili swali la muungano linavyoathiri maendeleo kote kote? ...
 
mm niwe mkweli seif ni kiongozi makini na anajua jinsi gani ya kumove na kupanga strategy kama ni karata basi ile ndio karata dume nnampongeza

ila sasa tunataka kuangalia kwa macho mawili ni jinsi gani hekima na busara zake zitaisaida zanzibar
 
Kama lilivyo jina lako.... JE ULIHITAJI WAZANZIBARI WAUWANE TENA??? Matokeo halisi ya Zanzibar Maalim ameshinda je unadhani angelikataa matokeo wale waliozingira hoteli ya Bwawani kutetea KURA ZAO ingelikuwaje matokeo yake??? YA KUUWANA WAMETUACHIA WABARA SASA!!
 
Kama lilivyo jina lako.... JE ULIHITAJI WAZANZIBARI WAUWANE TENA??? Matokeo halisi ya Zanzibar Maalim ameshinda je unadhani angelikataa matokeo wale waliozingira hoteli ya Bwawani kutetea KURA ZAO ingelikuwaje matokeo yake??? YA KUUWANA WAMETUACHIA WABARA SASA!!

Kwenye hizo caps umenichefua sana. Laiti ungekuwa ni raia wa kenya alafu unatamka hayo maneno hadharani kule wangekuchoma moto.
 
Kwa kweli simwelewi, hata jambo la uchaguzi kuwa na dosari alilieleza kirahisi sana. Yule anaenda kuwasindikiza CCM
 
Maalim Seif ni kati ya wanasiasa Ngangari kabisa mwenye kuhimili vema 'Ngunguri Politics'..Hakununuliwa wala kutishwa.Ni ukomavu tu wa kisiasa na mapenzi ya dhati juu ya nchi yake! Wako wanaobeza kwamba amekubali haraka kwakuwa amejua atakuwa 'VP' lakini hebu tujiulize kama 'shein na ccm' nao wangekubali haraka,kama wangeshindwa kwa tofauti ya asilimia moja ya kura..ukipata kigugumizi juu ya how ccm could respond then Jirudi haraka na kumpa Big up mpiganaji huyu ambaye Alitoka na 1st class ya political science hapo Mlimani...BRAVO,MAALIM,BRAVO KARUME,BRAVO SHEIN,BRAVO ZENJI!
 
Kura za Maalim zinazidi za Dakta wa ukweli Shein kwa takriban kura 2800. Kiukweli Zenj haiko tayari kutawaliwa na Wapemba, achilia mbali Mpemba wa CUF, ambayo kwa Unguja inaonekana kama Hizbu. Ongezea uhalisia wa muafaka wa Karume na Seif ambao siyo wa CCM na CUF maana vingun ge hao wawili walikaa peke yao. Kama angekubaliwa Maalim Seif kuapishwa badala ya Dk. Shein, ni nini kingezuia MAPINDUZI mapya ya kumuondoa Maalim Seif. Kwa mara ya kwanza nimekubali kuwa Maalim Seif anaipenda Zanzibar kikwelikweli maana ameamua kujishusha ili Zanzibar itawalike. Hakika kila ajishushae atakwezwa. Hongera Maalim Seif, Hongera Dk. Shein
 
OIC na Mafuta kwanza vyeo baadae. Nimewapenda walivyoweka maslahi ya taifa lao mbele. Lakini pia usisahau mpambano umekuwa wa kisiwa cha Pemba kumpata Rais na kwa hiyo lengo limetimia Dr (wa Ukweli) Shein ni mpemba hata kama hafanani nao sana
 
Back
Top Bottom