Waumini watengwa kwa kuichagua CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waumini watengwa kwa kuichagua CCM

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Dec 3, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Dec 3, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida mamia ya waumini wa Kanisa Katoliki Jimbo la Sumbawanga, mkoani Rukwa, wamejikuta katika wakati mgumu baada ya uongozi wa kanisa hilo kutangaza kuwatenga na wengine kufukuzwa kutokana na madai ya kukiuka kanuni za kanisa hilo.
  Habari za uhakika ambazo zimethibitishwa na baadhi ya waumini hao waliokumbwa na mkasa wa kutengwa na kufukuzwa walidai kuwa kufukuzwa kwao kumetokana na wao kushabikia Chama cha Mapinduzi CCM) katika kampezi za uchaguzi mkuu uliopita wa Oktoba 31 mwaka huu.

  Hata hivyo haikuweza kufahamika mara moja idadi ya waumini waliofukuzwa na kanisa hilo kwa kuwa inadaiwa kuwa ni wa kutoka vigango tofauti vya jimbo hilo na kwamba kila kigango kilipewa taarifa kwa wakati tofauti za waumini wake kusimamishwa au kufukuzwa.

  Katika jitihada za kupata ukweli wa tukio hilo, Tanzania Daima ilifanikiwa kuonana na baadhi ya viongozi wa kanisa hilo jimboni hapo ambao walikiri kuwepo kwa tukio hilo.

  Padri Deogratius Simemba na Padri Leonard Teza, wa familia takatifu, walipotakiwa kutoa ufafanuzi juu ya sakata hilo, walisema kuwa kwa mujibu wa sheria za kanisa hilo waumini hawaruhusiwi kujihusisha moja kwa moja na masuala ya siasa kwa mgongo wa kanisa, hivyo kama kuna waumini walikiuka wanapaswa kuchukuliwa hatua.

  Lakini pia waliongeza kuwa hawakufukuzwa bali tayari walishajitenga na kanisa kutokana na kuidhalilisha imani ya kanisa hilo.
   
 2. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #2
  Dec 3, 2010
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kwanza sijakuelewa unamaanisha nini hapa! pili hauna hushahidi wowote wa jambo hilo.
  tatu haipendezi na si vizuri kuleta thread za mambo yanayoweza kuleta misuguano kwenye jamii.
   
 3. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #3
  Dec 3, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,101
  Likes Received: 4,057
  Trophy Points: 280
  uache uzabazabina wewe... ukisoma ulicho-post, hawajatengwa kwa kukipigia CCM bali kukifanyia kampeni kanisani na ni viongozi walipata dhahama hiyo
   
Loading...