Waumini wa Kakobe watimua wahandisi wa Tanesco | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waumini wa Kakobe watimua wahandisi wa Tanesco

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Sumbalawinyo, Jan 29, 2010.

 1. Sumbalawinyo

  Sumbalawinyo JF-Expert Member

  #1
  Jan 29, 2010
  Joined: Sep 22, 2009
  Messages: 1,286
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  Mgogoro kati ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na waumini wa Kanisa la Full Gospel Fellowship kuhusu kupitisha njia ya umeme wa msongo wa Kilovoti 132 mbele ya kanisa hilo, umechukua sura mpya, baada ya waumini hao kuwatimua wahandisi wa shirika hilo waliokwenda kufanya tafiti.
  Tukio hilo lilitokea jana saa 6:30 mchana, baada ya wahandisi hao wakifuatana na polisi kufika eneo la kanisa hilo lililopo Mwenge kwa ajili ya kuanza utafiti kuhusu athari zitakazotokea umeme huo utakapopitishwa.
  Mratibu wa Mgogoro huo kwa upande wa kanisa hilo, Emmanuel John, alisema watu hao ambao walijitambulisha kuwa wanatoka Kampuni ya Dico na Tanesco walifika eneo hilo na kueleza kuwa walikwenda kwa ajili ya kufanya utafiti wa athari zitakazopatikana kwa binadamu, jengo na vifaa vya kanisa hilo.
  Alisema, kabla ya tukio hilo, juzi walipokea fax kutoka Wizara ya Nishati na Madini ikiwataarifu kuwa itatuma jopo la wahandisi kwenda kufanya utafiti, lakini haikueleza siku na saa ambayo watu hao watafika.
  Alisema mtafaruku uliibuka baada ya waumini kuwaarifu wahandisi hao kwamba hawawezi kuwaruhusu kufanya kazi hiyo bila kuwepo kwa Askofu Kakobe, kwani muda huo hakuwepo.
  "Waumini walipinga kufanya kazi hiyo ikiwa Askofu Mkuu hayupo, lakini wenzetu walikuwa wabishi wakataka kuenndelea na kazi zao kitu ambacho kilileta mvutano mkali," alisema.
  Baada ya mvutano wa muda mrefu, waliamua kumpigia simu Askofu Kakobe ili wajadiliane na watu hao, ambapo baada ya majadiliano hayo iliamuriwa wahandisi hao warudi walipotoka na kazi hiyo ifanyike leo wakati askofu huyo akiwepo.
  Mgogoro huo unaodumu kwa miezi miwili sasa umesababisha waumini wa kanisa hilo kuanzisha ulinzi nje ya kanisa kupinga hatua yoyote ya Tanesco kutekeleza mradi huo.

  CHANZO: NIPASHE
   
 2. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #2
  Jan 29, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Kazi ipo!
   
 3. Mahai

  Mahai JF-Expert Member

  #3
  Jan 29, 2010
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 351
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Dah hi kali, kwa hiyo wako pale kwa ajili ya kakobe na sio kwa manufaa ya kanisa lao kwa ujumla.
   
 4. K

  Kalimwage Member

  #4
  Jan 29, 2010
  Joined: Jan 29, 2010
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Waumini wa Kakobe wana haki kabisa ya kufanya yote hayo, before hiyo service ilitakiwa kupita left hand side if you come from ubungo, means UDSM side, but UDSM walikataa kabisa wasipitishe ktk eneo lao nadhani UDSM walifanya tafiti zao na kuona ni hatari tupu,

  Bigup KAKOBE
   
 5. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #5
  Jan 29, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Yangu macho!

  Vipi kuhusu minara ya simu iliyozagaa vibarazani mwa nyumba zetu? Ningefurahi kampeni ya Kakobe ingeingia mpaka kwenye minara ya simu!!
   
 6. Mwamanda

  Mwamanda Senior Member

  #6
  Jan 29, 2010
  Joined: Feb 24, 2009
  Messages: 132
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Tanesco walipaswa wafanye kwanza tathmini hii kabla ya kuanza kutekeleza mradi na sio baada ya kuanza utekelezaji wa mradi.Haya ni mapungufu kwa upande wa tanesco.
   
 7. Ng'azagala

  Ng'azagala JF-Expert Member

  #7
  Jan 29, 2010
  Joined: Jun 7, 2008
  Messages: 1,275
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  majengo ya UDSM yapo mbali sana na barabara. hiyo point haina msingi

  kwani athari ni mpaka ingekuwa(left) udsm side as you call it?

  hebu linganisha kakobe side na udsm side na pia distance ya udsm side mpaka kwenye makazi/maofisi ya UDSM na pia kanisa la kakobe.
  na hii athari ni kwa waumini wa kakobe tu kwani kokote itakapopita kuna watu wanaishi. na pia ni vyema watu wajue kuwa umeme haupiti kwenye kiwanja cha mtu (kakobe for that matter). unapita kwenye eneo la hifadhi ya barabara. hivyo huu ni ubinafsi

  pia watu wafikirie line nyingine za umeme kutoka kihansi/ kidatu/ mtela zimepita wapi?
   
 8. M

  Magezi JF-Expert Member

  #8
  Jan 29, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Kakobe ni mwizi tu hata wanao hangaika naye eti ni askofu wao nao ni wehu. Serikali ingekuwa ya maana kwanza ingemkatia umeme kakobe na kuondoa service line.
   
 9. M

  Magezi JF-Expert Member

  #9
  Jan 29, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Kwani mabango ya kakobe/kanyani si yapo kwenye hifadhi ya barabara??
   
 10. Maarifa

  Maarifa JF-Expert Member

  #10
  Jan 29, 2010
  Joined: Nov 23, 2006
  Messages: 2,880
  Likes Received: 1,050
  Trophy Points: 280
  Kunji hilo??? Au!!!
   
 11. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #11
  Jan 29, 2010
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  na bado mwaka wa uchaguzi huu lazima kwa vyovyote taaaaanesco itasalimu amri.
   
 12. M-bongotz

  M-bongotz JF-Expert Member

  #12
  Jan 29, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,732
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Una uhakika na hii kitu wewe au unashabikia tu, mbona UDSM ni mbali sana kutoka katika eneo la barabara ya Sam Nujoma pamoja na kwamba eneo hilo lote ambalo lipo adjacent na hiyo road ni la chuo?
   
 13. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #13
  Jan 29, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Kama unatokea Ubungo Upande wa:

  Kulia kuna:-
  - CHUO CHA MAJI
  - CHUO KIKUU (a couple of Workshops + TANESCO Transformer)
  - MLIMANI CITY
  - ENEO LA "FISADI MTOTO"
  - ENEO LA ASKOFU RWEGASIRA
  - OIL COM
  - JESHI
  - ??? (Maduka ya Hardware)
  - BP

  Kushoto kuna
  - SISIMIZI (BAR na Mnyama kwa Saaaaana)
  - Abandoned NHC House(s)
  - Mama Mkapa Complex
  - TCRA Headquaters (mpya)
  - Kituo cha Mafuta (do not remember the name)
  - Residential cum Office Cum Bar(s)
  - Masista wa Katoliki (Enock alisoma hapo chekechea)
  - Kanisa la FGBF aka Zakary (i) Kakobe
  - Jengo la Bwana Heri (Restaurant/Car Park)
  - Mafundi Seremala
  - Wachonga Vinyago
  - Maduka ya Hardware
  - Kanisa (Zamani Msalanga Baa)
  - Stendi (mbofu mbofu) ya Mwenge


  Sasa unashangaa nini mradi kupita upande wa kushoto? Compare NI nani zaidi upande wa KULIA na Kushoto?

  Hao waumini hata wakeshe mwaka mzima Nyaya za Umeme zitapita upande wa Kanisa la Zachari(y) Kakobe
   
 14. Dreamliner

  Dreamliner JF-Expert Member

  #14
  Jan 29, 2010
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 2,034
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Hawana cha kufanya!
   
 15. M

  Materanus Member

  #15
  Jan 29, 2010
  Joined: Jan 18, 2008
  Messages: 42
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii inaonyesha watu hawa wanaweza kujitoa muhanga kwa ajili ya Kakobe na sio Mungu wao. Kwani tangu lini Mungu alipingana na maendeleo? ndiyo maana Mungu aliwahi kulalamika kuwa "Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa". sorry ni kitabu gani wala verse lakini habari ndiyo hiyo.
   
 16. e

  ezekielboaz Member

  #16
  Jan 29, 2010
  Joined: Jan 16, 2010
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  du!kumbe paka akitoka panya hawatawali' hiyo
   
 17. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #17
  Jan 29, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,578
  Likes Received: 3,877
  Trophy Points: 280
  Bigu up, umezungumza professionaly na hili ni tatizo kubwa ambalo watanzania wengi hawajui.

  mbaya zaidi inatokea ndani ya wizara ambayo ilitakiwa iwe na risk analysts, is the same way wanafanya migodini kwa kisingizoi cha maendeleo.

  usije ukakuta mradi unaenda kwa tajiri mmoja anakiwanda chake, after yrs watu wanpata magonjwa, hakuna maandishi ya kuwashtaki, people need to rethink this ina global way.

  Tanesco they are dead wrong in this case!

  thanks for this
   
 18. M

  Mlokole 1 New Member

  #18
  Mar 1, 2010
  Joined: Mar 1, 2010
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo na watanzania wengi hupenda kuongelea jambo bila kulifahamu kwa undani au bila kufanya research ndogo tu. Kwa mfano, hili sakata la Kakobe na TANESCO liko hivi: katika kusambaza umeme Tanesco hujenga laini za misongo mikubwa na midogo kama 440Kv, 220KV, 132Kv na nyingine. Na kila laini ina vigezo vyake vya umabli kutoka makazi ya watu hadi pale ilipo laini. Sasa kwa hii laini ya 132Kv inapaswa kujengwa eneo la wazi lenye ukubwa wa mita 15 yaani 7.5mt kila upande. Hiyo ni minimum safe distance kwa hiyo unaweza kuwa mkubwa zaidi ya hapo.Sasa pale kwa Kakobe umabli huo haupo, ule uliopo ni 2.8-3mt pekee, hivyo laini ikiwekwa waamini na mitambo ya kanisa kutakuwa na athari kubwa.Halafu kwa taarifa yenu Kakobe ni mtu makni kuliko mnavyofikiria na huu upinzani anaoonesha ulipaswa kuoneshwa na kila mtu inapopita laini hiyo lakini watanzania wengi ni hawana ujasiri wa kupinga kitu hata kama kina madhara kwao. Ni vizuri kufahamu kwamba hapa Kakobe hapingi maendeleo bali anapinga ufisadi wa TANESCO na BICO ya chuo kikuu cha Dar es Salaam ambao wamefoji vipimo vya umbali ili ionekane kuna mita 7.5 lakini ukweli ni mita 2.8 hata wewe ukienda pale leo utathibitisha hilo.Halafu kuhusu yeye kutozungumzia scandal nyingine katika nchi hii hiyo iko wazi kwamba kama angefanya hivyo ninyi haohao mngesema hili halimhusu na kuanza kumwita majina ya kashfa. Hili ni la watanzania wote kuamua kupambana na scandals hizo na sio mtumishi wa Mungu Kakobe.Kuhusu waamini wanapeana zamu na kwa taarifa yenu wapo wasomi waliobobea katika taaluma zao, wenye nafasi kubwa serikalini na jamii na hata matajiri, kwa hiyo wanapeana zamu sio kwamba wakati wote ni walewale.Ningewashauri mfanye utafiti na kufika kanisani ili mmjue kakobe badala ya kutoa kashfa kwa mtumishi wa Mungu msije mkalaaniwa. MUNGU AWABARIKI NA KARIBU KANISA LA FULL GOSPEL MAHALI PANAPOHUBIRIWA KWELI TUPU MPATE KUOKOLEWA NA BWANA YESUAsante sana!
   
 19. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #19
  Mar 1, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180

  Agrrrrrrrrr KIBWETERE mwingine huyuuuuu.
   
 20. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #20
  Mar 1, 2010
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Wewe ndo kibwetere.vinginevyo tupe points zako za maana kuhakikisha kuwa huo umeme hauna madhara kwa WENYENCHI(wakiwemo waumini wa Full gospel).
  Tubadilikeni jamani tusipende kuburuzwa.pengine na nyie mnaomkashifu Kakobe mna hisa na Tanesco.
   
Loading...