Waumini tuna cha kujifunza hapa

Mzururaji

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
1,559
1,272
Jana zilisambaa picha kwenye social media ambazo zilimwonesha Mhe, lowasa akiwa na viongozi wa serikali na chama cha mapinduzi akiwepo Mhe, rais na Katibu Mkuu wa CCM. Picha ilipigwa kanisan huku viongozi hao wakionesha furaha ya waziwazi akiwepo mama Regina LOWASA,
mbali ya kuwa tunajua wana tofauti.


Misingi ya tofauti ya viongozi hawa ni kabla na baada ya uchaguzi mkuu ambapo baada ya matokeo kutoka Mhe, lowasa alinukuliwa sehemu mbalimbali akisema wamemwibia kura hivyo ushindi ulikuwa wake. Toka kipind cha matokeo hakujawahi tokea picha zenye mwonekano wa namna ile ambazo zilizua minong'ono miongoni mwa wananchi wengi wao wakipongeza na wana ukawa wakimpongeza lowasa hasa kuelekea sept mosi.( siku ya UKUTA) Kama utakuwepo.

Kikubwa kilicho zua minong'ono ni aina ya pozi likiwaonesha ni watu wenye furaha na kwamba hakuna lolote kati yao hapa imedhihiri mambo ya majukwaani wameyaweka pembeni na pale walikuwa wanahudhuria ibada ya kikristo ambapo waumini huondoa kinyongo chochote ili kukaribia madhabahu ya Bwana.


Kwa wakristo eneo la msiba na kanisan ni maeneo ya ibada ambapo waumini huwa wanakatazwa kufanya mambo ambayo ni dhambi ambayo yatafanya sala ya toba isipokelewe ndo mana ikaandikwa samehe saba Mara Sabin.


Lakini hayo yakijili kule visiwani kuna waumini wenzetu waligoma kusalimiana kisa siasa tena eneo la msiba. Picha nyingi zilisambaa zikimuonesha maalim seif akigomea salam ya mkono kutoka kwa muumini mwenzie dr shein. Mimi naamini haikuwa sehemu sahihi kuonesha tofauti kwani kwa mujibu wa dini ya kiislam msiba ni ibada ambapo muumini anapata muda wa kutafakari mapito yake wapi anatoka na wapi anaenda ili kujiandalia mwisho mwema kwa mola wake.


Hapa waumini wa kiislam tuna la kujifunza kutoka kwa viongozi hawa waumini wa kikristo ambapo Jana walionesha umoja eneo la kanisa badala ya utengano hapa tegemea kuona wakristo wakiwa wamoja zaidi kupitia viongozi wao ambao wana uwezo Mkubwa kuficha hisia zako kwani kupitia matendo haya ndipo wananchi huungana


Kwetu sisi viongozi ambao ni waumini wa kiislam tunapaswa kujua kuwa waumini wenzetu wanatuangalia na wanajifunza kitu kikubwa kutoka kwetu. Ingawa mnaweza kuhisi kuwa nyie ni viongozi wa kisiasa tuu.
Kwenye majukwaa yenu ya siasa huko haina tatizo lakni tofauti mnapo kuja kizionesha eneo la msiba na nyumba za ibada zinabomoa umoja wa waumini wenzenu.


Mwisho nimpongeze Mhe LOWASA kwani nae alikuwa na nafasi kama yule mwingine kugomea salam au hata kununa.

©malibwadu;-
Kwa sasa mafunzoni kilombero.
 
Hilo la maalim seif ni tatizo lake binafsi sio mafundisho ya dini, hata lowasa angeweza kufanya hivyo kama angeamua

kwani matatizo yake hajui kama pale kulikuwa msiban mpaka alete matatizo yake
 
Maalim ni crystal clear kuwa tokeo lilichezewa,Edo ni inasemekana tokeo lake lilichezewa
 
mjinga sio mimi,BALI KILA ATAKAYE SOMA HYO ID YANGU BHAS NI MJINGA,HYO NI NAFSI YA KWANZA UMOJA,POLE YAKO,
 
kitendo walichomfanyia maalim,ccm na shein huko zanzibar,hakiwezi kuvumilika,kusamehe,au kusahau kirahs kwa binadamu yeyote,kuongoza kwa asilimia 52,alaf mtu anaamua kufuta matokeo kwa sabab anazozijua yeye,alaf ukutane nae umpe mkono wako,ni ngumu sana,machungu aliyo nayo huyajui,kwa hyo KAA KIMYA,
 
Si sahihi kufananisha hali ya bara na ile ya visiwani. Hakuna aliyedhulumiwa huku bara, mengine ni siasa tu ukizingatia ni nadra mno kwa politicians Wabantu kukubali matokeo. Lakini kule Znz kila kitu ni bayana na ni unafiki tu unaopelekea tatizo lisionekane. Tusiingize na dini hapa, Mungu hapendi UNAFIKI.
 
Back
Top Bottom