Wauguzi wafutiwa leseni kwa kusababisha kifo cha mjamzito Mkoani Mtwara

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,458
Baraza la Wauguzi na Ukunga Tanzania (TNMC), limewafutia leseni wauguzi wasaidizi wawili wa Hospitali ya Wilaya ya Mkomaindo, Masasi mkoani Mtwara, baada ya kupatikana na hatia ya uzembe uliosababisha kifo cha majamzito na mtoto wake."

Wauguzi hao Elizabeth Njenga na Pascal Mnyalu, walishtakiwa kwenye baraza hilo pamoja na wauguzi wengine watatu na madaktari wawili, wote wa hospitali hiyo kuhusika na uzembe uliopoteza maisha ya mjamzito Aisha Romanus.

Wauguzi wengine waliofikishwa katika baraza hilo ni Joyce Nkane na Tumaini Milanzi ambao walipewa onyo kali na Lucia Liababa, ambaye alifutiwa shtaka lake baada ya kuonekana kutohusika moja kwa moja.

Kabla ya hukumu hiyo iliyotolewa na Mwenyekiti wa Baraza hilo, Lilian Msele, pia aliwatia hatiani madaktari wawili wa hospitali hiyo, Amina Mushi na Hashimu Chiwaya, ambao taarifa zao zitapelekwa kwenye Baraza la Madaktari ili hatua stahiki zichukuliwe.

Awali dada wa marehemu Agnes John, alilieleza Baraza hilo kuwa Novemba mosi, mwaka jana, mdogo wake Aisha, alishikwa na uchungu wa uzazi na kuamua kumfikisha zahanati ya Lukuledi na muuguzi wa zahanati hiyo baada ya kumpima aliwaeleza waende hospitali ya Wilaya ya Mkomaindo.

Alisema, hata hivyo alipopiga simu hospitali hiyo ya wilaya wauguzi walimjibu hawakuwa na mafuta ya kutumia kwenye gari la wagonjwa na kulazimika kukodi bajaji ambayo pia iliharibika njiani na baada ya matengenezo walifika saa moja usiku hospitali ya Mkomaindo.

Agnes alisema baada ya kupokewa mgonjwa wake hakupata huduma haraka na kuambiwa aondoke jambo alilolipinga na muda mfupi alimuona mdogo wake akiomba msaada kwa wauguzi hao, lakini hawakumjali na ilipofika usiku wa saa tano akaaga dunia.

Wajumbe wa baraza hilo ambao waliwahoji madaktari na wauguzi hao walishangaa baada ya maelezo yao kuwa tofauti kiasi cha mjumbe Haruna Neke kukerwa kutokana na maelezo waliyoyawasilisha awali baada ya kutakiwa kuandika taarifa kutofautiana na maelezo waliyokuwa wakiyatoa.

Kutokana na hukumu hiyo Mwenyekiti wa baraza hilo, Lilian Msele, alisema wauguzi hao hawatotakiwa kufanya shughuli zozote za kiuguzi kutokana na kukiuka kanuni na viapo vyao walivyokula, pia alilaumu uongozi wa hospitali hiyo kutokuawa na ufuatiliaji wa watumishi wake na iwapo usimamizi ungekuwa mzuri maafa kama hayo yasingeweza kutokea.

Naye Msajili wa Baraza hilo, Agnes Mtawa, aliwataka wananchi kufikisha malalamiko yao waonapo hawatendewi haki na wauguzi na madaktari ili wachukue hatua stahiki huku akibainisha kuanza kusikiliza kesi nyingine iliyotoka mkoani Arusha.

Chanzo: Nipashe
 
Ilifaa wafungwe muda mrefu na kazi ngumu hawa mabazazi, kunyimwa rushwa kidogo tuu ndo watelekeze mgonjwa hadi afe!
Huwa ndio zao. Sijui huwa wanalipwa hela za kuchezea simu kazini. Hili suala lipo sehemu nyingi mno yaani mno. Wasipopewa kitu Basi. Sijui Bora watu warudi kujifungua Kama Bibi na mama zeetu walivyotuza jamani.

Najiulizaga mbona wild animals hajawahi fanyiwa operesheni eti njia ndogo. Na mitindo ya maisha yanachangia
 
  • Thanks
Reactions: ITR
K
Baraza la Wauguzi na Ukunga Tanzania (TNMC), limewafutia leseni wauguzi wasaidizi wawili wa Hospitali ya Wilaya ya Mkomaindo, Masasi mkoani Mtwara, baada ya kupatikana na hatia ya uzembe uliosababisha kifo cha majamzito na mtoto wake."
Kuna Hospital ya mkoa Mwanza Sekotoure kuna wauguzi wa namna hyo wengi sana......Wamefanya shangazi angu akatwe mguu kwa sabb ya uzembe wao na sijui wale ni madaktari au watu gani tena wodi ya private ndio kabisa bora chanfanyikeni utasaidiwa na wagonjwa wenzio
 
Baraza likiwa serious na wataaluma wake watakua serious na kazi..hongereni baraza kwa kazi nzuri ya kusimamia taaluma uzembe ni mwingi sana kwa kweli wengi hupoteza maisha kwa uzembe tu na kuchelewa kupata huduma.

Naamini haki imetendeka.

#MaendeleoHayanaChama
 
Hii ni hatua nzuri kwa wafiwa. Sasa wachukue hatua ya pili kwenda mahakamani kudai fidia. Pesa haitarudisha uhai wa marahemu lakini itatoa fundisho
 
One sided narrative. Ningependa kujua kwa nini walishindwa kumhudumia kwa wakati.

Naamimi kwa 95% ya uhakika hospitali ya wilaya haina emergency service SOP. Kwa hiyo utatupwa. kwenye foleni kama wengine uliowakuta. Kosa la hospitali na serikali nayo yanahusika.

Na kwa nn wasianzie na uzembe wa serikali kitojaza mafuta ya ambulance inayopiga trip mbili tatu tu kwa siku ?

Landcruiser VX V8 la Katibu Tawala wa Wilaya na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya na Mganga Mkuu wa Wilaya yanaweza kukosa mafuta ????
 
One sided narrative. Ningependa kujua kwa nini walishindwa kumhudumia kwa wakati.

Naamimi kwa 95% ya uhakika hospitali ya wilaya haina emergency service SOP. Kwa hiyo utatupwa. kwenye foleni kama wengine uliowakuta. Kosa la hospitali na serikali nayo yanahusika.

Na kwa nn wasianzie na uzembe wa serikali kitojaza mafuta ya ambulance inayopiga trip mbili tatu tu kwa siku ?

Landcruiser VX V8 la Katibu Tawala wa Wilaya na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya na Mganga Mkuu wa Wilaya yanaweza kukosa mafuta ????
Unafikiri baraza limelirupuka
 
Unafikiri baraza limelirupuka
Hukumu za mahakama zinachemkwa na zinatenguliwa sembuse za baraza la wauguzi.

Baraza la Wauguzi haliwezi kuikosoa serikali. Serikali ya nchi kama Tanzania ina nguvu za kimungu.

Kwa nini ambulance ya wilaya haina mafuta. Tuanzie hapo.
 
Back
Top Bottom