Wauguzi sita Temeke wasimamishwa Kazi kwa kuuza gloves

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
Naibu Waziri wa Afya, Dk Hamis Kigwangalla amewasimamishwa kazi wauguzi sita katika hospitali ya Temeke kwa kosa la kuomba rushwa.

Wauguzi waliosimamishwa ni Hadija Salum, Beatrice Temba, Agnes Mwampashe, Elizabeth Mwilawa, Mariam Mohamed na Marion Said, ambao walikuwa zamu katika wodi ya wajawazito wakati wa tukio hilo.

“Nimewasimamisha kazi wauguzi wote waliokuwa zamu jana (juzi) asubuhi, nakuagiza Msajili wa Baraza la Wauguzi uwasimamishe hadi utakapowasafisha kupitia kamati ya msajili,” alisema Dk Kigwangalla.

Mmoja wa wajawazito, Loshan Seif alisema alipowasili juzi asubuhi kwa ajili ya kujifungua, muuguzi mmoja wa zamu alimtaka kulipia Sh5,000 za gloves.

“Siku zote huwa natumia bima lakini jana (juzi) wakaniambia hawatumii, nitoe Sh5,000 za gloves, baadaye niliambiwa natakiwa kuwa na uzi wa mshono, sindano na vingine hivyo kama sina nitoe fedha,” Seif.

Dk Kigwangalla alifanya ziara ya ghafla hospitalini hapo jana saa 9.00 alasiri.

Akizungumza jana alasiri baada ya kufanya ziara ya ghafla Hospitalini hapo na kupata malalamiko hayo kutoka kwa wanawake waliojifungua.

“Mama anaambiwa atoe fedha ya gloves Sh5,000 wakati dukani zinauzwa Sh1,000, nataka liwe fundisho kwa wote wanaotuongezea vifo vya wajawazito kwa tamaa ndogondogo,” alisema Kigwangalla.

Katika ziara hiyo, Dk Kigwangalla alishuhudia ubovu wa vyumba viwili vya upasuaji na kutoa maelekezo kwamba, virekebishwe ndani ya miezi sita.

“Hali ni mbaya ndani ya hizi ‘theater’ zote mbili zifanyiwe ukarabati iwapo itashindikana nitazifunga, lazima ziwe na hadhi yake na nitakuja kukagua,” alisema.
 
12809593_1050095048388286_3006907623577884863_n.jpg

TUKIANZA NAMNA HII TUTANYOOKA TU, HIZI RUSHWA NDOGO NDOGO NDIO HASWA ZINAZOTUUMIZA SANA WATU WA CHINI, PESA YAKO YA KULA NA FAMILI UNAMPA MTU HUKU ROHO INAUMA, MADAKTARI, MANESI, MAHAKIMU, POLISI WAJIANDAE KUISOMA NAMBA HII NI TNZANIA YA MAGUFULI,SAMIA NA MAJALIWA SIO YA JK NA MZEE WA RICHMONDULI KUJUA NA KULEANA ITS OVER
Nani alikwambia uwe mtu wa chini? Walaumu wazazi wako ambao hawakukupa elimu ya kuwa mkubwa unakofanya kazi.
 
Hii itashabikiwa na watu wenye akili ndogo tuu, utasimamishaje roster nzima ya wauguzi waliofanya kazi usiku na mchana Kisa umeambiwa na mgonjwa njiani kuwa kuna muuguzi kamuuzia glove. Hii ni ubovu wa kufanya maamuzi. Na madhara yake mtayaona kimya kimya.
 
Ila Kudhibitisha hiyo rushwa ni kaz sanaa.....naona hawa wauguz wakishinda kesi......
 
Kabla hajawasimamisha kulikuwa na upungufu mkubwa wa manesi, baada ya kuwasimamisha hao watano ina maana upungufu umeongezeka zaidi, kwa hiyo atakaye umia ni mwananchi huyohuyo aliyelalamika, rushwa ya elfu tano waziri alitakiwa kutumia busara ya kuwaonya tu na kuwataka wamrudishie mgonjwa pesa yake
 
Hii itashabikiwa na watu wenye akili ndogo tuu, utasimamishaje roster nzima ya wauguzi waliofanya kazi usiku na mchana Kisa umeambiwa na mgonjwa njiani kuwa kuna muuguzi kamuuzia glove. Hii ni ubovu wa kufanya maamuzi. Na madhara yake mtayaona kimya kimya.
Wanasema omba na utapewa, ndio wanachoomba hiki watanzania watu watumbue majipu ya kila siku kwenye sector matatizo yake ambayo kiini chake ni kikubwa zaidi.

Upo sahihi kabisa ni aina ya watu gani wanaoweza kuendelea kushabikia hili zoezi sasa ambalo mwanzo wengine tulichukulia kama salamu tu hila kuna mipango zaidi inasukwa kwenye kutatua haya mambo for the long term lakini hakuna.

Kila mtu anajua watafika sehemu watasimamisha watu kazi lakini tatizo liko pale pale na hii ndio njia itakayo tumika kuficha udhaifu wa uwezo wao kama ilivyo kawaida.
 
Kabla hajawasimamisha kulikuwa na upungufu mkubwa wa manesi, baada ya kuwasimamisha hao watano ina maana upungufu umeongezeka zaidi, kwa hiyo atakaye umia ni mwananchi huyohuyo aliyelalamika, rushwa ya elfu tano waziri alitakiwa kutumia busara ya kuwaonya tu na kuwataka wamrudishie mgonjwa pesa yake
Tatizo ni uwezo wao mkuu, sijui kwanini amtaki kusema kiini chenyewe; hata wewe unaweza kuona kuwa sio sahihi iweje waziri ashindwe kufikiria hilo.
 
Ifike kipind muwe mnaelewa hakuna anaye penda kuchukua rushwa za wagonjwa Hosp,,,nilifanya field Tmk hosp tena ktk hiyo word ya wazaz 2014,,kinachotokea Nurses hawatakiw kulaumiwa
Wizara ya afya wanasema mama mjamzto kwenda kujifungua ni bure hosp hiyo sera ni sawa na pongez ila haifanyiwi kaz na serikal kwahiyo haitekelezeki kiuhalisia
Idad ya wamama wanaojifungua pale tmk inafika 80 mpaka 90 kwa shift moja mfano ukiingia night saa mbil usiku mpaka saa mbil asubuh umesimama kuzalisha tu na hapo mpo Nurses 3 na doctor1 wa word ikitokea emergency yeyote ya mgonjwa kwenda theater Nurse mmoja lazma aend theatre na mgonjwa mtabak 2 kuzalisha inafika mda vifaa vya kuzalishia vinaisha pale wordn na mmama anapush hapo na hana vifaa kwakuwa kaambiwa kujifungua ni bure unaweza unajikuta unampokea mtoto na kanga pale maana ukiacha anadondoka chin
Hiyo ilikuwa inagarimu sana maisha ya manese kunabaadh wanapata infections za magonjwa mbalimbali kwa ukosefu wa kujilinda mfno HIV hepatitis na TB,,mfano wa Nurses walio pata infectious ninao..kwahyo ikabid kila mgonjwa anapokuja tu tunaangalia vifaa vyake vya kujifungulia km Gloves,cord clamp,cutegut,gouse au pamba,,km hajaja navyo tunamwambia relatives aliye mleta akanunue vifaa amletee akae navyo mgojwa mdawake wa kujifungua ukifka inakuwa rahis kwa nurse nikumposition tu na kuchukua vifaa vyake na kumzalisha na pale tmk wamama weng wanaoenda kujifungua ni wakipato cha chin sana na ndio maana wako weng
Sasa kumwambia ndugu akanunue vifaa ili vimsaidie mgonjwa wake ni kosa? Na wakat wod haina gloves?
Licha ya hivo baadh ya ndugu ukiwa agiza vifaa wanaenda mojakwamoja hawarud km ni usiku anarud asubuh ndugu yake ameshajifungua,,kuna baadh ya nurse wakaona isiwe tabu wakawa wananunua vifaa vyao huko na kuja navyo kazn km mgojwa hana vifaa ndio hapo ataambiwa leta elf5 anapewa kilichokosekana km ni gloves au any hii yote ni kurahsicha utendaj kaz na Nurse kujilinda na magonjwa maana bila glaves nihatar kat ya wamama80 kumi hapo ni HIV+ve wanaojifungua kwa shift,,,na maranyng hata mahuzurio ya clinik wanaambiwa ukiwa mimba imefika miez 5,6 na kuendelea uwe unatembea na vifaa vya kujifungulia cha kushangaza mpaka anapatwa na Labour pain hata gloves hajanunua na anakuja yupo second stage hata status yake ukiangalia haiandkwa kwenye kad ndio maana nurse anaenda na vifaa vyake ikitokea mgojwa hana vifaa anamuuzia anapata pesa ya nauli hapo na kajikinga na infection ukiangalia mishahara yenyewe majanga laki nne na nusu take om kaz unacheza na blood za wamama
Naibu wazir amekurupuka sana kwa hili
 
Zima Moto. Tekelezeni sera ya huduma bure. Serikali wapeleke vifaa muhimu hospitalini. Magonjwa mengi ya kuambukiza,wauguzi wafanyeje? Wakacheze na damu za mama mikono mitupu? Acheni kunyanyasa watumishi
 
Upuuuzi juu ya upuuuzi yani vifaa hupeleki halafu unataka bure mbona bure itatuponza
 
Mi nadhan lengo ni kujionyesha kwa jamii kwamba wewe ni mkubwa na unaweza kufanya lolote unapokwenda popote kwenye taasisi yako., ivi inangiaje akilini wauguzi 6 uwasimamishe kazi bila kuleta wengine hapo hapo kwa kosa la nurse 1 tu aliyemtoza Tshs 5000 kwa ajili ya kununua gloves?

Kama Waziri anafanya hivyo kwa kuwapenda wananchi kumbe ndio anawaumiza zaidi wananchi pengo la wafanyakazi 6 hasa hospital kwa siku1 tu ni kubwa sana sana linaweza kuathiri zaidi ya watu 100 kwa siku.
 
Hawa Viongozi wetu wamezidi kukurupuka sasa hapo kosa lipo kama hamna gloves walitaka nesi azalishe mikono mitupu sawa glove moja inauzwa 1000 lakini sidhani kama hiyo inaweza kumuhudumia mzazi wanashindwa kupeleka vifaa wanabaki kuwaonea wauguzi.
 
Ifike kipind muwe mnaelewa hakuna anaye penda kuchukua rushwa za wagonjwa Hosp,,,nilifanya field Tmk hosp tena ktk hiyo word ya wazaz 2014,,kinachotokea Nurses hawatakiw kulaumiwa
Wizara ya afya wanasema mama mjamzto kwenda kujifungua ni bure hosp hiyo sera ni sawa na pongez ila haifanyiwi kaz na serikal kwahiyo haitekelezeki kiuhalisia
Idad ya wamama wanaojifungua pale tmk inafika 80 mpaka 90 kwa shift moja mfano ukiingia night saa mbil usiku mpaka saa mbil asubuh umesimama kuzalisha tu na hapo mpo Nurses 3 na doctor1 wa word ikitokea emergency yeyote ya mgonjwa kwenda theater Nurse mmoja lazma aend theatre na mgonjwa mtabak 2 kuzalisha inafika mda vifaa vya kuzalishia vinaisha pale wordn na mmama anapush hapo na hana vifaa kwakuwa kaambiwa kujifungua ni bure unaweza unajikuta unampokea mtoto na kanga pale maana ukiacha anadondoka chin
Hiyo ilikuwa inagarimu sana maisha ya manese kunabaadh wanapata infections za magonjwa mbalimbali kwa ukosefu wa kujilinda mfno HIV hepatitis na TB,,mfano wa Nurses walio pata infectious ninao..kwahyo ikabid kila mgonjwa anapokuja tu tunaangalia vifaa vyake vya kujifungulia km Gloves,cord clamp,cutegut,gouse au pamba,,km hajaja navyo tunamwambia relatives aliye mleta akanunue vifaa amletee akae navyo mgojwa mdawake wa kujifungua ukifka inakuwa rahis kwa nurse nikumposition tu na kuchukua vifaa vyake na kumzalisha na pale tmk wamama weng wanaoenda kujifungua ni wakipato cha chin sana na ndio maana wako weng
Sasa kumwambia ndugu akanunue vifaa ili vimsaidie mgonjwa wake ni kosa? Na wakat wod haina gloves?
Licha ya hivo baadh ya ndugu ukiwa agiza vifaa wanaenda mojakwamoja hawarud km ni usiku anarud asubuh ndugu yake ameshajifungua,,kuna baadh ya nurse wakaona isiwe tabu wakawa wananunua vifaa vyao huko na kuja navyo kazn km mgojwa hana vifaa ndio hapo ataambiwa leta elf5 anapewa kilichokosekana km ni gloves au any hii yote ni kurahsicha utendaj kaz na Nurse kujilinda na magonjwa maana bila glaves nihatar kat ya wamama80 kumi hapo ni HIV+ve wanaojifungua kwa shift,,,na maranyng hata mahuzurio ya clinik wanaambiwa ukiwa mimba imefika miez 5,6 na kuendelea uwe unatembea na vifaa vya kujifungulia cha kushangaza mpaka anapatwa na Labour pain hata gloves hajanunua na anakuja yupo second stage hata status yake ukiangalia haiandkwa kwenye kad ndio maana nurse anaenda na vifaa vyake ikitokea mgojwa hana vifaa anamuuzia anapata pesa ya nauli hapo na kajikinga na infection ukiangalia mishahara yenyewe majanga laki nne na nusu take om kaz unacheza na blood za wamama
Naibu wazir amekurupuka sana kwa hili
Serekali hii maigizo matupu uwezo hawana lakini tabu tu
 
Back
Top Bottom