Wauguzi sio vibaya kuwaiga madaktari kwenye hili

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,305
12,600
Nilifurahi sana nilipowaona Madaktari chini ya Rais wao wa chama cha MAT walivyojipanga kwa unyenyeketi kuomba kuongea na Rais kuelezea mambo mapana yanayohusu Madaktari nchini na mambo mengine yenye maslahi kwa taifa.

Jambo kama hili ni vema kuigwa na taaluma nyingine nchini nchini ikiwemo ya wauguzi ambao ndiyo uti wa mgongo wa sekta ya afya nchini.

Huduma ya Muuguzi ndiyo inayoamua mgonjwa apone, apone na ulemavu au afe, inaamua kama mgonjwa apone haraka au achukue muda mrefu kupona na kurudi nyumbani, ndiyo inayoamua kidonda cha operation kipone au kioze.

Bila Muuguzi hakuna operation hata moja itakayofanyika ikafanikiwa, bila muuguzi hakuna kulazwa wodini wala ICU, bila muuguzi hakuna kuzaa leba wodi, bila muunguzi hakuna vidonda kupona, bila muuguzi hakuna kutundikiwa madrip wodini, bila muuguzi hakuna mgonjwa atakae ogeshwa wodini, bila muuduguzi hakuna kuchomwa sindano, bila muuguzi hakuna chanjo, bila muuguzi hakuna uzazi wa mpango, nk, nk, nk.

Kama walivyo wenzao madaktari wauguzi pia lazima wanazo kero zao nyingi sana za kumueleza Mh. Rais azijue na ikiwezekana azitafutie ufumbuzi hata kama ni kwa kutamka maneno tu.

Mfano, Rais Magufuli alitatua baadhi ya kero za madaktari kama kwa kuwapa matumaini tu akisema:

Rais Magufuli: Rais wa MAT amezungumza hapa wanahitaji jengo kwa ajili ya shughuli zao. Nimemuuliza hilo jengo la ghorofa ngapi, akajibu 3. Nikamuuliza mmekadiria kiasi gani, akasema bilioni 3. Nikashangaa ghorofa 3 bilioni 3! Nikaona hapo kuna ufisadi wa aina fulani.

Milioni 500 zinajenga Kituo cha Afya, kwenye hiyo hela kuna Vituo vya Afya sita maana yake mtachangishwa ninyi wanachama mpaka mchoke. Kama MAT wanahitaji jengo, mimi nitawapa jengo bure. Tutatafuta hata hapa Dar, ofisi nyingi zimehamia Dododma.

Rais Magufuli: Sijawahi kutoa jengo kwa bodi nyingine kama kwa Wahandisi lakini natoa kwa Madaktari kwa kuwa natambua kazi kubwa mnazofanya kwa Watanzania. Madaktari oyeee, Madaktari safiiii. Msiwe na wasiwasi ninaposema oyeee, sitasema CCM ni Madaktari tu leo.

Rais Magufuli: Ninachosema ni kuwa Madaktari hawatakiwi kupata 'frustrations' yoyote inayoweza kutekelezwa na Wizara husika. Inatakiwa shida zao zishughulikiwe kwa haraka na udharura kwa sababu wao pia wanawashughulikia wangojwa kwa morali hiyo.

Rais Magufuli: Nakubaliana na ninyi, haiwezekani mtu ambaye ni 'professional' kila mahali unamuona mtu mwingine anatishia kumweka ndani tu. Haiji wala haifurahishi. Unafanya upasuaji unatoka kule bahati mbaya damu zinavuja unawekwa ndani. Si atakufa na unayemtibu?

Rais Magufuli: Najua siku hizi hamuwekwi ndani sana, sisi tumeambiana huku kwetu wala msiwe na wasiwasi. Najua akikuweka ndani kesho akija anaumwa na wewe utamuweka ndani. Ila msifanye hivyo kwa kuwa utakuwa unabeba dhambi kwa Mungu, kazi yenu mkaifanye vizuri.

Rais Magufuli: Nafahamu kuna Madaktari takriban 2,700 hawajaajiriwa bado, hili nalifanyia kazi. Nafikiri tunaweza kuanza polepole hata kuchukua 1,000. Waziri wa Utumishi tunaweza?

Kupewa jengo bure na Mh. Rais sio jambo dogo, bila kuonana na kuzungumza nae isingekuwa rahisi kupewa jengo bila kuchangishana kutoka kwenye mishahara ambayo tayari ina changamoto nyingi.

Inafahamika kuwa wauguzi pia hawatoshi huko kwenye vituo vya kutolea huduma na vyuo vya kufundishia wauguzi, Rais wetu mpendwa anaweza pia kusema neno kwaajili ya zile zahanati zisizokuwa na wauguzi

Wauguzi mnatakiwa kujipanga, kutumia hekima na utii ili pia mtafute nafasi ya kuongea na Mkuu wa nchi badala ya kulalamika chini kwa chini au kutumia njia zisizo rafiki kudai au kupinga kitu.
 
Sisi Hatuna Nguvu...Sisi Hatuna Uwezo...Sisi Hatujielewi.
Shida yenu iko kwenye mind-set, mnashindwa kujiamini na kujenga hoja, hampendani wenyewe kwa wenyewe, mnatafunana wenye kwa wenyewe. Tafuteni viongozi wenye vision wanaoupenda uuguzi kutoka mioyoni mwao. Hawa ni wale ambao hata watoto wao wa kuwazaa wamewashawishi kuwa wauguzi pia.
 
Yote sawa lakini udaktari ulikuwepo kabla ya kuzaliwa YESU.Taaluma ya nurse ilianzishwa na mwanadada Florence Nightingale mwaka 1854 kwenye vita vya Crimea alihudumia askari walioumia na taa yake usiku.Alizaliwa mwaka 1820 akafariki 1910.
Nurse ni muhimu na ni kazi ya wito zaidi kuliko udaktari.Umeshasikia nurse wamegoma?
Bila nurse kazi zitakwenda japo kwa tabu ila bila daktari hakuna kinachoendelea.
Pichani ni muasisi wa nurse
Screenshot_2020-02-22-00-45-14.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uzi mrefu... ungesema tu kuwa na wauguzi mnaomba ajira. Unazunguka kweli.
 
Kila tarehe 12 mwezi May ni Siku ya wauguzi Duniani.
Na Mwaka huu maadhimisho yanategemewa kufanyika mkoani MANYARA na Mgeni Rasmi ni MAKAMU WA RAISI WA JMT,nadhan mamb yote yatakuwa siku hiyo
Yote sawa lakini udaktari ulikuwepo kabla ya kuzaliwa YESU.Taaluma ya nurse ilianzishwa na mwanadada Florence Nightingale mwaka 1854 kwenye vita vya Crimea alihudumia askari walioumia na taa yake usiku.Alizaliwa mwaka 1820 akafariki 1910.
Nurse ni muhimu na ni kazi ya wito zaidi kuliko udaktari.Umeshasikia nurse wamegoma?
Bila nurse kazi zitakwenda japo kwa tabu ila bila daktari hakuna kinachoendelea.
Pichani ni muasisi wa nurseView attachment 1365648

Huenda umekosea hapa. Kazi za muuguzi na Uuguzi ulikuwepo tangu mwanadamu alipoumbwa. Ila nightingale alikuja na formal principles za Uuguzi.
 
Tatizo nokuto jitambua.Wodi ina wagonjwa 70 manesi 2 usiku kucha hii ni hatari sana kwa wagonjwa.Wodi ya wagonjwa wa akili wanalazwa 50 , muuguzi mmoja usiku kucha.
 
Tatizo nokuto jitambua.Wodi ina wagonjwa 70 manesi 2 usiku kucha hii ni hatari sana kwa wagonjwa.Wodi ya wagonjwa wa akili wanalazwa 50 , muuguzi mmoja usiku kucha.
Ndani ya uuguzi kama muuguzi akitoa wazo la wauguzi kwenda kuonana na Mkuu kujadiliana nayekuhusu masuala ya kazi yao ya uuguzi ataandamwa sana na kupigwa vita na viongozi wa wauguzi haohao. Ndo maana hawafiki wanakotaka kwenda
 
Back
Top Bottom