Wauguzi nao watishia Kugoma; Waipa Serikali siku 3 kuanza kushughulikia madai ya madaktari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wauguzi nao watishia Kugoma; Waipa Serikali siku 3 kuanza kushughulikia madai ya madaktari

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ALOYCE MPANDANA, Jan 27, 2012.

 1. ALOYCE MPANDANA

  ALOYCE MPANDANA Senior Member

  #1
  Jan 27, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 170
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  TAMKO LA WAUGUZI KUHUSU HALI YA HUDUMA ZA AFYA MUHIMBILI KUFUATIA TOFAUTI KATI YA MADAKTARI NA WAFANYAKAZI WENGINE KATIKA SEKTA YA AFYA NA MWAJIRI

  Chama cha Wauguzi Tanzania tawi la Hospitali ya Taifa Muhimbili, tunasikitika kwa hali inavyoendelea hadi hivi sasa hatuna taarifa ya kupatikana kwa muafaka kati ya watumishi sekta afya hususani madaktari na Mwajiri (Serikali), kutokana na hali iliyojitokeza bado tunazidi kusisitiza serikali kukaa meza moja na kuangalia kwa kina chimbuko la matatizo yaliyojitokeza ili kuyatafutia ufumbuzi kwa faida ya umma wa watanzania. Matatizo yapo yanajulikana yatafutiwe ufumbuzi haraka, pande zote mbili ziwe flexible katika kufanya maamuzi. ·

  Wauguzi hufanya kazi na kada nyingine ikiwa ni pamoja na madaktari hivyo hatuwezi kutimiliza mahitaji ya wagonjwa sisi peke yetu, hali imezidi kuwa mbaya. · Kwa kuwa muuguzi ni mtumishi wa karibu sana na mgonjwa kuliko watumishi wengine wa afya tunaona wanavyoteseka, hali hii inatuumiza kisaikolojia na kimwili pia, wauguzi ndio wanaonekana wabaya na wameshaanza kutukanwa nawagonjwa na ndugu zao kwa kukosa huduma, wizara tumeiambia pia. ·

  Hali ya huduma kiujumla imezidi kuzorota na itafika wakati hatutaweza kumudu majukumu yetu ya kazi na hatupendi tufike huko kwani tunajua madhara yake hivyo hatupo tayari kuona hali hii ikiendelea, · Katika mazungumzo yetu na wizara, tunashukuru kwa jitihada zinazochukuliwa na serikali.

  Hata hivyo tumeona bado kuna matatizo kwa upande wa uuguzi wizarani, tunaiomba wizara kuunda kurugenzi ya uuguzi ifikapo Julai mwaka huu, hatujapendezwa na suala hili kuchukua muda mrefu pasipo sababu za msingi na tunasikitika kwamba hakuna jitihada za makusudi za kufanikisha kilio hiki cha wauguzi kwa muda wa hivi karibuni. Tunaiomba serikali kuzingatia ombi hili ili kurudisha imani kwa wauguzi.

  haki za msingi za wauguzi ikiwa ni pamoja na uniform allowance wauguzi wapewe pesa zao na sio kuwashonea kutoka MSD. Pamoja na haya yapo mengi ambayo tumeongea na wizara tunasubiri kuona utekelezaji wake ni imani yetu kuwa wizara itayatekeleza kwa wakati muafaka. ·

  · Tunaomba serikali iwasikilize wafanyakazi kwa ujumla wake katika sekta ya afya na kutafuta suluhu ya matatizo yaliyopo,
  · Waziri mkuu atumie busara yake awafuate madakitari na awaite wizara ya afya wazungumuze na madakitari. e
  · Tunawaomba wenzetu madaktari na watumishi wengine wakubali kukutana na ujumbe huo.
  · Mh. Rais afany mabadiriko ya wizara ya afya · Katibu mkuu ateuliwe anayejua mambo ya afya
  ·

  · Hivyo basi ifikapo Jumatatu tarehe 30 January 2012 bila ya kuwa na muafaka kuhusu tofauti na mvutano uliopo hivi sasa, basi nasi uwezo wetu wa kuvumilia hali hii ya sasa utakuwa umefikia wakati wa kukaa vikao endelevu. . · Chama kinawapongeza wauguzi hospitali ya taifa muhimbili kuendelea kutoa huduma na kinawasihi kuendelea na kazi hadi watakapokuwa wametangaziwa vinginevyo. …………………………

  Paul Magesa
  Mwenyekiti Imetolewa na chama cha wauguzi Tawi la Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Nakala; Waziri wa Afya – WAUJ Mkurugenzi Mtendaji – Hospitali ya Taifa Muhimbil Mkurugenzi – Kurugenzi ya Uuguzi na Ubora - Hospitali ya Taifa Muhimbili Mkuu wa Chuo - MUHAS Rais – Chama cha Wauguzi Tanzania Rais – Chama cha Madaktari Mameneja wa majengo – Hospitali ya Taifa Muhimbili
   
 2. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #2
  Jan 27, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,781
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  MH....Mwaka huu kazi ipo!!!
   
 3. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #3
  Jan 27, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  moto ndio kwanza unaanza
   
 4. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #4
  Jan 27, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  sijui lini unazmika
   
 5. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #5
  Jan 27, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Tatizo la viongozi wa serikali kula pesa wenyenyewe hk wanasahau watumishi wengine wa umma wakisota
   
 6. m

  mareche JF-Expert Member

  #6
  Jan 27, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 475
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  jk yupo radhi kusafiri kwa mamilion ya kodi zetu kwenda kwenye mikutano isiyokuwa na tija kwa taifa bdl ya kuyumia pesa hizo kulipa madr ngoja wauguzi nao wagome tutakufa wote
   
 7. usininukuu

  usininukuu JF-Expert Member

  #7
  Jan 27, 2012
  Joined: Aug 8, 2011
  Messages: 380
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Serikali haitakiwi kuwapuuza wauguzi na madaktari kwani madhara yake ni makubwa.
   
 8. saragossa

  saragossa JF-Expert Member

  #8
  Jan 27, 2012
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 2,141
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  Ndo naiangalia ITV mida hii! Balaa!
   
 9. Tausi Mzalendo

  Tausi Mzalendo JF-Expert Member

  #9
  Jan 27, 2012
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 1,471
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mbivu na mbichi zitajulikana siyo mbali sana! Hivi Serikali yetu tukufu inayosikiliza, imekuwa kiziwi ghafla? Vipaumbele vya serikali viko wapi?Hivi haioni madhara yaliyo mbeleni? Binadamu ana roho moja isiyo na spea. Ikitoka imetoka.Hivi mtawaambia nini wapiga kura wenu waliowaweka madarakani?
   
 10. Lasikoki

  Lasikoki JF-Expert Member

  #10
  Jan 27, 2012
  Joined: Jan 10, 2010
  Messages: 642
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  kah! Kazi ipo, ewe Mungu tunusuru
   
 11. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #11
  Jan 27, 2012
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  sasa subiri wauguzi wafanye kweli ndo wizara itatambua kuwa sekta ya afya ni muhimu kuliko umuhimu wa rais wetu kwenda kufanya mazungumzo na david kameroon!
   
 12. D

  Dan08 Member

  #12
  Jan 27, 2012
  Joined: Aug 23, 2009
  Messages: 67
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  "serikali yenu ndugu wanainchi ni sikivu sana"utasikia viongozi akiwe PM wakisema...usikivu upo wp,kila kitu ni siasa tu kwa viongozi wetu
   
 13. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #13
  Jan 27, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,768
  Likes Received: 6,091
  Trophy Points: 280
  MAJIBU MEPESI: CHADEMA hao!
   
 14. A

  August JF-Expert Member

  #14
  Jan 27, 2012
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,509
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  hao wauguzi hawaijui sirikali? atakuja Pasco hapa na waraka wa sirikali kwamba within 48 hours watakuwa wamepewa summary dismissal, na Pasco hato wapa nauli wa makazi shauri yao!
   
 15. Ndebile

  Ndebile JF-Expert Member

  #15
  Jan 27, 2012
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 3,633
  Likes Received: 1,991
  Trophy Points: 280
  Wauguzi acha hizo! Nyie matatizo yenu mbona ni makubwa kuliko hata madaktari? Mlisubiri wenzenu waanze eti,kwa kuwakumbusha tu nyie mlitakiwa kugoma tangu mwaka jana kwasababu zifuatazo:

  Ni wauguzi pekee wanaolipia leseni za kufanya kazi sh.10,000 hadi 15,000 kila mwaka...na hamjuhi pesa hiyo hutumika kufanya nini? Kuna tetesi kuwa sh.milioni 300 ziliyeyuka pasipo kujulikana wakati uongozi wa lilokuwa Baraza la wakunga la awali lilipobadirishwa kwa mujibu wa sheria ya uuguzi na ukunga iliyopitiswa na bunge.

  Wauguzi nyie ndio kada iliyokuwa haitambuliki kama 'proffesional' hadi hivi majuzi tu,sijuhi ulikuwa unatambulika kama 'Utawa?'hata hivyo Degree,Masters na PhD katika Uuguzi bado muundo wa utumishi wa umma bado unazitambua qualification zote hizo kama 'Registered Nurse' wenzenu madaktari ni tofauti na huo ujinga,yaani hata hilo mpaka muambiwe.

  Wauguzi pamoja na wingi wenu na uzito wa kazi zenu mishahara yenu ni ya chini sana bado hamna ushirikiano,ilo linajidhihirisha kwenye utitiri wa vyama vyenu: TANA,PRINMAT,etc.,mbona madaktari chama chao kimoja...matokeo yake mnaishia kujadili rangi na mishono ya uniform zinazotofautisha EN,RN,PHN nk.shame on you Nurses!

  Gomeni basi kushinikiza kuwepo na Idara ya wauguzi inayojitegemea ndani ya wizara ya afya tofauti na sasa ambapo Muuguzi mkuu wizarani yupo chini ya daktari mkuu wa taifa...uuguzu ni kada inayojitegemea sio lazima kuwa chini ya daktari mkuu,ndiyo maana kila siku mnashitaki kuchapwa vibao na madaktari...mara oh tunafanywa ma-p.secretary wa madaktari. Sijasema msishirikiane bali nawafahamisha mipaka na upekee wa kazi zenu na hivyo hakuna sababu ya kusubiri ma dr. wagome ndio mjitokeze....

  Wauguzi pazeni sauti...mbona nyie ndio mnaongoza kwa kuambukizwa AIDS kutokana na kuchomwa sindano zenye viini vya maambukizi na hamna bima wala fidia,mnaugua TB nyie kwa kukaa muda mwingi na wagonjwa na lishe yenu duni.

  Kwa kifupi matatizo yenu ni mengi na si vizuri kuwaegemea drs..
   
 16. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #16
  Jan 28, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  hali itakiwa mbaya sana pale clinical officers watakapoingia rasmi kwenye mgomo.nahisi tunaelekea huko.
   
 17. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #17
  Jan 28, 2012
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Huu ni mwaka 2012 according to Mayans and other ancient knowledgeable giants, 2012 is the End of Time,
  not end of the World!

  End of Time maaana yake;
  Ni mwisho wa kujificha nyuma ya uongo.
  Ni mwisho wa Chepeo kuitwa kijiko.
  Ni mwisho wa kutawala kwa mkono wa chuma.
  Ni mwanzo wa ujsiri hekima na uwazi
  Ni mwanzo wa wanyonge kujaa matumaini
  Ni mwanzo wa Nuru kufichua yaliyo gizani.
  Waheshimiwa madaktari safari hii mpaka kieleweke.
  Huyo aitwaye IRON LADY atabadili jina na kuitwa HAYAWANI LADY
   
 18. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #18
  Jan 28, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Sasa Duhhh. Hawa wafanyakazi wa serikali wanaojenga mahekalu wanapata wapi pesa. Labda hii ni issue ya matabaka.
   
 19. C

  CHIEF MGALULA JF-Expert Member

  #19
  Jan 28, 2012
  Joined: Sep 11, 2009
  Messages: 782
  Likes Received: 257
  Trophy Points: 80
  mwaka wa shetani huu,tusubiri na walimu ambao walitaka kulianzisha kabla shule kufunguliwa lakini sijui kilichotokea
   
 20. H

  Honolulu JF-Expert Member

  #20
  Jan 28, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 5,654
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Bado tunawasubiri na maaskari waunge azimio!!! Matatizo si kwa madaktari tu!! nanyi askari amkeni!! Tokeni usingizini!! Someni kwa haraka waraka huu KISHA muwaunge mkono madaktari!!!

  Waraka maalum kwa Askari wote


  MAKALA hii ilikuwa itoke Jumatano ya wiki iliyopita lakini kwa sababu za kiufundi ikashindikana. Imekuwa ni bahati nzuri kwamba inapotoka leo, ijibu swali la askari polisi dereva wa gari la maji ya kuwasha.

  Askari huyo alimweleza Mwalimu Mkuu wa watu jinsi roho inavyomuuma pale anapowamwagia Watanzania wenzake maji hayo ya kuwasha wakati wakidai haki yao. Askari uliyeuliza na wenzako wote someni makala hii kwa utulivu. Huu ni waraka maalumu kwa askari wote wa majeshi yote vikosi vyote Tanzania Bara na Visiwani.

  Kwa lugha ya wazi zaidi nazungumza na askari wa Jeshi la Polisi Tanzania, Askari wa Jeshi la Kujenga Taifa, askari wa Kikosi Maalumu cha Kuzuia Magendo (KMKM), askari wa Jeshi la Magereza na wale wa Jeshi la Wananchi (JWTZ).
  Kuwa mwanajeshi lolote kati ya hayo niliyoyataja si dhambi na si kweli kwamba kuwa mwanajeshi kunakuondolea uwezo wa kufikiri na badala yake ukawa unafikiriwa na watu wengine.

  Wala haimaanishi kuwa askari kuwa kama robot ndio nidhamu bora kuliko zote duniani. La hasha! Mimi nilikataa utumwa huo!

  Mwaka 1999 nilihitimu elimu ya cheti cha ufundi mchundo, yaani Full Technician Certificate (FTC) katika uhandisi wa Elektroniki na Mawasiliano ya Anga, yaani Electronics & Telecommunications Engineering kutoka Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT).

  Nikiwa bado sijapata kazi ya maana, mwezi Aprili mwaka 2000 niliona tangazo la kazi ya Radio Technician katika Jeshi la Magereza. Nikatuma maombi na kuitwa kwenye usaili uliofanyika Chuo cha Maofisa wa Jeshi la Magereza Ukonga, Dar es Salaam mwezi Juni 2000.

  Wote tuliofaulu usaili tulipangiwa siku ya kuripoti Chuo cha Magereza Kiwira kule Tukuyu, Mbeya.

  Kufika kule nilishuhudia mambo ya ajabu. Ingawa wao hufurahia na kusema eti wanakutoa uraiani na kuwa mwanajeshi lakini baadhi ya matendo yanayofanyika wakati wa mafunzo ya jeshi ni ya kuwapumbaza askari wetu ili baadaye wakiwa kazini, watawala wawatumie watakavyo.

  Nilishindwa kuvumilia kaulimbiu ya wakufunzi wa jeshi pale walipoelekeza kwamba chochote kruta (askari mpya mafunzoni) unachoambiwa lazima uitikie “ndiyo afande”. Nilishindwa kuitikia kwa mfano pale mkufunzi mmoja mwenye cheo cha koplo alipotutamkia mfululizo wa sentensi zifuatazo:
  Mkufunzi: Nyinyi makruta mbona wote hamkuja na majembe?
  Makruta: Ndiyo afande!
  Mkufunzi: Hamkuambiwa makao makuu ya jeshi kwamba lazima mje na majembe?
  Makruta: Ndiyo afande!
  Mkufunzi: Kwa hiyo kwa kuwa hamkuambiwa na nyinyi hamkuyabeba?
  Makruta: Ndiyo afande!
  Mkufunzi: Wote ni wapumbavu pamoja na mama zenu waliowazaa.
  Makruta: Ndiyo afande!

  Ni hayo pamoja na mambo mengine ya kulazimishwa kwenda kwenye kile kinachoitwa disko, ambapo pamoja na uchovu wa kutwa nzima wa kazi ngumu na nyingi bado ni lazima ukae hapo mpaka saa 4 usiku tena ukinyooshewa kidole tu na mwenzako lazima usimame na kuimbisha wimbo tena kwa tabasamu, wimbo mmoja wapo ukisema “Magereza ninavyokupenda nitakunywa sumu juu yako”, ndiyo yaliyonifanya nikakataa kazi ya jeshi baada ya wiki moja tu ya mafunzo.

  Siku niliyokataa jeshi ilikuwa ni Jumatano asubuhi ambapo sikwenda mchakamchaka na wakati wenzako wanatawanyika kufanya usafi wa nje maeneo mbalimbali, mimi nilibeba begi langu na kuanza kuondoka chuoni majira ya saa moja na nusu hivi asubuhi.

  Nilikamatwa na mkufunzi mmoja wa jeshi na kupelekwa pamoja na begi langu kwa Ofisa Mafunzo wa chuo. Aliponiuliza sababu nilimtajia mbili, kwanza kwamba sifurahii mambo ya jeshi na kubwa zaidi kwamba mimi ni Msabato na nimeambiwa na wenzangu kwamba hapa hakuna kwenda kusali, siku zote za juma ni kazi.

  Kitu ambacho sitaweza maana Sabato takatifu lazima nipumzike! Bila kuuliza zaidi aliconclude kwa kuniambia kwamba, “Sijawahi kuona mtu anaacha kazi kwa ajili ya mambo ya dini.

  ”Ni dhahiri wewe ulikuja kutupeleleza na hivyo kazi yako imeisha sasa unataka kurudi. Tutakuweka rumande, tena ile ya polisi kwa wiki mbili wakati tunafanya upelelezi juu yako.”

  Askari aliyenileta alianza kunivuta ili kunipeleka rumande lakini nilikataa huku nikiendelea kujieleza kwa ofisa mafunzo ili ajue kwamba sikuwa na mpango huo aliousema.

  Baada ya kuelemewa na hoja zangu alinipeleka kwa makamu mkuu wa chuo ambaye yeye alitumia zaidi Biblia kunihubiri kwamba nakaidi amri ya mamlaka wakati hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu.

  Jibu langu lilikuwa fupi na lenye msimamo mzito kwamba ikiwa mamlaka ya wanadamu inafika mahali inanena tofauti na Mungu, Mtume Petro ametuandikia kwamba katika hali ya namna hiyo, “Imetupasa kumtii Mungu kuliko mwanadamu”.

  Na yeye alinishindwa akanipeleka kwa mkuu wa chuo na wao wote wakiwapo. Ushauri waliokuwa wakimpa mkuu wa chuo ni kwamba mimi niwekwe rumande kwanza ili wafanye upelelezi. Lakini sikuyumba katika msimamo wangu.

  Nilimweleza mkuu wa chuo kwamba mimi ni raia na si mpelelezi. Nilizirudia rudia sababu zangu za kuacha jeshi tena kwa ujasiri mkubwa na kumhakikishia mkuu wa chuo kwamba akinipa hayo ninayoyataka niko tayari kubaki jeshini.
  Hatimaye kauli ya mwisho ya mkuu wa chuo ilikuwa ni hii: “Jeshi ni wito. Tunaweza kumlazimisha huyu kijana kuwa mwanajeshi lakini baadaye ikatuletea madhara makubwa sana.” Akamalizia kwa kusema, “chukueni maelezo yake kwa maandishi kisha arudishe vifaa vya jeshi.”

  Wakati naondoka nilimsikia ofisa mafunzo akitoa maelekezo kwa walio chini yake kwamba mwanafunzi mwingine wa jeshi akija kuripoti na kwenye daftari akajaza kwamba ni Msabato, msimsajili kwanza mpaka aje kwangu! Sijui kama Wasabato wameendelea kupokewa kwenye hicho chuo cha magereza lakini ninachotaka askari wote wa majeshi yetu yote na vikosi vyote, ni kwamba askari unaweza kusimama kwa miguu yako na kufikiri kwa akili yako mwenyewe!
  Ndugu zangu askari, nchi imefika mahali ambapo Waingereza hupenda kupaita ‘critical point’. Ni mahali ambapo wananchi wako tayari kwa mabadiliko na watawala wako tayari kwa mapambano ili kubaki madarakani.

  Katika point hii askari wetu wanakuwa na nafasi kubwa ya aidha kuwezesha mabadiliko hayo kutokea kwa wakati wanaoutaka wananchi, tena kwa amani ama kuyachelewesha (si kuyazuia) na kusababisha yatokee baadaye kidogo kuliko wananchi walivyotaka, tena baada ya kumwaga damu nyingi ya Watanzania wasio na hatia!

  Napenda kurudia kwamba hakuna jeshi lolote duniani hata kama tungekusanya majeshi yote ya dunia hii na kuyaleta Tanzania hawataweza kuizuia nguvu ya umma pale inapokuwa imeamua kufanya mabadiliko.

  Napenda tena kurudia kwamba si lazima askari mfanye kile ambacho wakubwa wenu wanataka na kuwaamuru kufanya. Tunaweza kusimama imara na kutetea haki za Watanzania tukiwamo na sisi askari. Niliwahi kugoma kutii amri ya kukamatwa na kuwekwa rumande.
  Lakini pia mifano ni mingi na nisingependa kuchukua mifano kutoka nchi za Ulaya kama Uingereza ambako tulishuhudia wananchi wakiandamana mitaani na askari wao hawakuwahi hata kumpiga kofi tu mwandamanaji hata mmoja.
  Walipohojiwa na vyombo vya habari walisema dhahiri kwamba waandamanaji ni raia halali wenye haki ya kufanya kile wanachokifanya kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi yao. Katiba ya Tanzania na sheria za nchi hii zinatoa haki kama zile za Uingereza. Tofauti ni utekelezaji wa matakwa hayo ya kikatiba na kisheria. Watawala wa Uingereza wako tayari hata kung’oka madarakani ili kutekeleza matakwa ya nguvu ya umma.

  Lakini wale wa Tanzania wako tayari kung’oa uhai wa raia wengi ili mradi kuzuia nguvu ya umma inayodai haki na wananya hivyo kwa sababu ya hofu ya kung’oka madarakani, jambo ambalo hawataki kabisa kulisikia. Na ndugu zangu askari napenda kuwaambia kwamba yote yanafanywa na watawala wetu kwa kuwategemea nyinyi.

  Wanaminya haki zenu nyinyi wenyewe, haki za wazazi wenu, dada na ndugu zenu, marafiki zenu, jamaa zenu na majirani zenu. Chukulia mfano rafiki zangu Mtaki na Edwin. Tumesoma wote shule ya msingi pale Magu.

  Nilichaguliwa kujiunga na Mazengo Sekondari, shule kubwa na ya muda mrefu ambayo sasa imegeuzwa kuwa chuo kikuu bila mabadiliko ya majengo.

  Shule iliyokuwa na maabara nne kwa maana ya maabara ya baiolojia, kemia, fizikia na jiografia. Ilikuwa ni sekondari ya ufundi na hakuna karakana ambayo haikuwapo.

  Shule iliyokuwa na walimu wa kutosha, vyumba vya kutosha vya madarasa na vya kulala mabwenini.
  Katika bweni la Ujamaa kwa mfano, nilikokuwa naishi mimi, kuna vyumba kadhaa havikuwa na watu. Darasa la Form IVA ambalo nilikuwamo lilikuwa na wanafunzi 21 tu darasani.

  Na mazingira mengine mengi ambayo sitaweza kuyataja hapa ambayo yanafanya wanafunzi wa leo wa Chuo Kikuu cha Mt. John wajiulize kama kweli ile ilikuwa ni shule ambayo haina maktaba wala vitabu vya kutosha, na mengineyo mengi mnayoyafahmu.

  Nikafaulu kwa kiwango cha daraja la juu lililoniwezesha kuendelea mpaka chuo kikuu na kupata kazi nzuri kwenye Umoja wa Mataiifa.

  Rafiki zangu nakumbuka mlivyoamua kujiunga na Jeshi la Polisi si kwa sababu mlipenda kazi hiyo ama kwamba mlikuwa na wito wa kuwa polisi kama mnavyodanganywa kwamba jeshi ni wito.

  Nakumbuka mlijiunga huku mkilalamika kwamba mnalazimika kujiunga huko kwa sababu kiwango chenu cha ufaulu hakiwapi fursa ya kazi bora zaidi ya hiyo. Lakini mimi nawafahamu vizuri. Najua uwezo wenu wa darasani. Mliathiriwa na mazingira ya hovyo ya shule mlizosoma.

  Rafiki zangu nyinyi wote leo ni wakuu wa vituo vikuu vya polisi vya wilaya katika wilaya za Mbozi na Igunga.
  Leo hii mimi nimeacha kazi ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kushiriki vema katika mapambano ya kutafuta ukombozi wa taifa hili.

  Wadogo zenu na wadogo zangu mnawajua wako katika juhudi za kutafuta maisha lakini ni magumu. Wengine walikosa kabisa nafasi ya kujiunga hata na hiyo Magu Day.

  Wakaishia Bulima na Kinango, ambako hali ilikuwa mbaya zaidi. Wakafeli kabisa na leo wanahangaika hapa na pale lakini watawala wanawawekea mazingira magumu mno ya kuendesha maisha.

  Na sasa chukulia nao wametambua hali yao duni inasababishwa na watawala walafi na walaghai. Wamejaribu kutumia njia za kidiplomasia kudai haki zao wanakutana na watu wanaitwa wakuu wa wilaya na mikoa.

  Wanaamua kuandamana, mnashiriki kuamrisha askari walio chini yenu kuwapiga na kuwaweka rumande na hatimaye kuwafungulia kesi za kubumba!

  Askari wetu igeni mfano wa askari wa Misri! Pale wananchi walipoamua kuandamana kukomesha utawala wa kidhalimu wa miaka 30 chini ya Hosni Mubarak, askari waliwalinda badala ya kuwapiga.

  Walikataa kwa sababu hata wao walikuwa wakiumizwa na Mubarak lakini zaidi ya hayo, waliokuwa wakiandamana walikuwa ni dada zao na ndugu zao na marafiki zao.

  Hivi sasa nchi iko njia panda. Ugumu wa maisha umeongezeka mara nne na zaidi. Watawala hawalioni hilo wala hawajishughulishi kurekebisha hali ya mambo hususan hali ya uchumi.

  Wako busy na kujiandaa kwa uchaguzi wa 2015. Mawaziri wako busy na kampeni za kuteuliwa kuwa wagombea wa urais kupitia chama tawala hapo 2015 na rais naye yuko busy kuandaa mtu wake ambaye anadhani akimrithisha jumba jeupe la pale Magogoni atasema mwacheni Ndugu Kikwete apumzike kwa amani.

  Taifa limeamua kuandika katiba mpya, rais na serikali yake na chama chake wameamua kuuteka mchakato ingawa haikuwemo kwenye ilani yao ya uchaguzi ili tu waturudishie katiba ya mwaka 1977 na kuipa jina juu ya jalada KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA 2014.

  Natambua juhudi zinazoendelea hasa zikiongozwa na CHADEMA kujaribu kumkumbusha rais kwamba katiba iko juu yake na katiba ni mali ya wananchi na yeye anaajiriwa kwa katiba hiyo na si yeye kujiandalia katiba ili atawale kwa ulaini.

  Lakini juhudi za kidiplomasia zikishindikana hapo ndipo itabidi haki ya watu idaiwe kwa maandamano na hapo askari wote tuungane na kuwa kama Misri, kwa kuwa Katiba mpya ni kwa masilahi yenu pia! Jaribuni kutafakari!
   
Loading...