Wauguzi hospitali ya Mirembe wagoma wakidai posho | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wauguzi hospitali ya Mirembe wagoma wakidai posho

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Salary Slip, Oct 6, 2012.

 1. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #1
  Oct 6, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 25,015
  Likes Received: 37,744
  Trophy Points: 280
  Wauguzi wa hospitali ya mirembe mkoani Dodoma wamegoma wakidai kuongezewa posho ya muda wa ziada wa kazi.

  Wauguzi hao wanadai kiasi cha sh 3000 wanacholipwa ni kidogo ukilinganisha na kiwango wanacholipwa wengine.

  Muuguzi mmoja ameiambia Nipashe kwamba wameamua kugoma baada ya kuona serikali haiwaangalii umuhimu wao.

  Muuguzi huyo alisema kuwa mwezi julai walilipwa sh 10,000 lakini mwezi uliofuatia walilipwa kiwango tofauti jambo lililowashitua na kutaka kujua sababu zake.

  Mganga mkuu wa hospitali hiyo Dr. Erasmusi Mndeme alikanusha kuwepo mgomo wa madaktari na kusisitiza kuwa waliogoma ni wauguzi.

  Aidha alisema kuna baadhi ya madaktari na wauguzi wanaingia kazini mara mbili kwa siku kutokana na upungufu wa wafanyakazi ktk hospitali hiyo.

  Dr.Mndeme alisema swala la malipo ktk hospitali hiyo liko kwenye viwango tofauti kulingana na vyeo vya watumishi hao.Alisema kuna watumishi wanalipwa sh 25,000,20,000,15,000,10,000 na kiwango cha chini cha malipo ni sh 5000 hadi sh 3000.

  Alisema kulingana na viwango hivyo ndio maana wauguzi wanaona wanapunjwa bila kufahamu kuwa katika nafasi walizonazo kuna utofauti mkubwa wa malipo wanayolipwa pindi wanapofanya kwenye ziada ya masaa.

  Chanzo:Nipashe la trh 06/10/2012.

  Hapa ndipo tunapoona ule umuhimu na ulazima wa ule mgomo wa madaktari kwani serikali hii ni kama sikio la kufa halisikii dawa.
   
 2. sindano butu

  sindano butu JF-Expert Member

  #2
  Oct 6, 2012
  Joined: Aug 20, 2012
  Messages: 478
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 45
  poleni wagonjwa na ndugu zao kwa itilafi hii. lakini kama wangepandisha call allowance kuwa elfu hamsini kwa mabingwa ,wachini wangefaidika kidogo . Jamani,kama MBUNGE kukaa kwenye sofa bungeni analipwa pesa zaidi ya elfu sabini HALAFU kwa kazi ya KUBISHANA wakati nesi anakesha USIKU MZIMA kwa elfu tatu huku akiokoa uhai wa watu. hii tanzania, sijui ndo sera ya CCM, uwezi ukawekeza bungeni wakati kwenye elimu na afya kuna kasoro, JAMANI WAKATI umefika watanzania tubadirike , TUACHE SIASA Kwenye afya na elimu ,ILA TUWEKE SIASA KWENYE KUBISHANA!!!
   
 3. Tram Almasi

  Tram Almasi JF-Expert Member

  #3
  Oct 6, 2012
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 755
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mkuu wewe unaongelea nesi ambaye anatibu wagonjwa wa kawaida lakini Mirembe hawa ni watu wenye matatizo ya akili, usiku huo wanaweza wakafanya lolote!Unakumbuka yaliyotokea wodi ya wagonjwa wa akili pale Muhimbili? jamaa vilimpanda na akaamua kuwapiga wenzake hadi kufa na nesi aliyekuwa zamu ilibidi akimbie sana kuokoa roho yake.
  So eneo la kazi la hawa ni hatarishi kwa njia yoyote ile. Wana risks za kuuawa, kubakwa na hata kuumizwa kwa njia nyingine yoyote. Hivi jamani watu wanajua kwanini kuna msemo ''Huyu anafanya kazi wodi ya vichaa na yeye amekuwa kama kichaa'' au ''Usimshangae huyo dokta si anafanya kazi wodi ya vichaa?''. Let us be serious jamani na mambo yanayohitaji u-serious.
   
Loading...