Wauaji wengine wa albino wahukumiwa kunyongwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wauaji wengine wa albino wahukumiwa kunyongwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mongoiwe, Nov 2, 2009.

 1. Mongoiwe

  Mongoiwe JF-Expert Member

  #1
  Nov 2, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 521
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  Mahakama kuu huko Shinyanga imefanya kweli tena kwa kuwahukumu kunyongwa mpaka kufa washitakiwa wane wa mauaji ya mtu mwenye ulemavu wa ngozi (Albino) Lyaku Wily (50) ambaye pia alikuwa na ulemavu wa akili.

  Waliokumbwa na adhabu hiyo ni hawa; Mboje Mawe(46), Nchenyenye Kishiwa (65), Sayi Lyamaya (4 na Sayi Mafizi (33) wote wakiwa ni wakazi wa wilaya ya Bariadi mkoani Shinyanga.
   
 2. October

  October JF-Expert Member

  #2
  Nov 2, 2009
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 2,147
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Saafi sana. Hiyo ndio adhabu wanayostahili.
   
 3. Original Pastor

  Original Pastor JF-Expert Member

  #3
  Nov 2, 2009
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 1,256
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Ok sawa sawa Kabisa hii ni fundisho naomba Rais aweke sain haraka ili nao wakatumikie Ahera big up hakimu.
   
 4. Prince Alberto

  Prince Alberto Member

  #4
  Nov 6, 2009
  Joined: Jun 18, 2009
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wanaforum wenzangu embu tumuhamasishe ndugu kikwete aweze kutia saini yake haraka kwa wale jamaa waliohukumiwa kunyongwa kwa kushiriki kuwaua maalbino huko shinyanga,
   
 5. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #5
  Nov 9, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Wako wapi wale watetezi wa haki za bin'Adam wanaokejeli adhabu ya kifo.
   
 6. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #6
  Nov 9, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mpaka waone something Islamic..ndio utawaona wanajidai kuua mbaya wanafiki kwelikweli..ukiuua dawa yake kifo...finito..
   
 7. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #7
  Nov 10, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]Mahakama ya Rufani Kanda ya Mbeya, imemhukumu adhabu ya kunyongwa hadi kufa mkazi wa wilaya ya Ileje, Obadia Kijala, baada ya kupatikana na hatia ya mauaji na uchunaji ngozi za binadamu.
  Akisoma adhabu hiyo jana, Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufani Kanda ya Mbeya, John Mgeta, alisema Obadia na wenzake watatu ambao wamefariki wakiwa rumande, walitenda kosa hilo Juni 15, 1999 katika kijiji cha Kisyesye kilichopo wilayani Ileje.
  Alisema mtuhumiwa pamoja na wenzake hao walimchuna ngozi mtoto Ezekia Kimwegile (11) mkazi wa Kisyesye wakati akiwa anachunga ngo’mbe mbali kidogo na eneo la nyumbani kwao.
  Msajili huyo wa mahakama aliongeza kuwa wahusika wa tukio hilo walifanya kosa hilo la uchunaji kwa makubaliano ya kuiuza ngozi hiyo kwa bei ya Sh. milioni 18 za Tanzania mara baada ya kufanikiwa.
  Alisema mara baada ya kupata ngozi hiyo mshitakiwa pamoja na wenzake walienda kwenye nyumba ya kulala wageni ya Mwanitu iliyopo wilayani Rungwe mahali walipokuwa wanakutana na mnunuzi wa ngozi hiyo ambaye alimtaja kwa jina moja la Joel.
  Pia alifafanua kuwa wakati mikakati hiyo ikiwa inaendelea askari walipata taarifa kuhusu tukio hilo na ndipo walipoweka mitego na kuwakamata watuhumiwa hao wakiwa na ngozi ya binadamu.
  Naibu Msajili wa mahakama hiyo, alisema adhabu hiyo imetolewa na jopo la majaji wa Mahakama ya Rufani baada ya kubaini kuwa mshitakiwa alihusika na tukio hilo.
  Awali msajili huyo alisema kuwa rufani hiyo iliyosikilizwa na majaji wa tatu, Jaji E. A Kileo, S. J. B. Wana na S. Mjasiri alipinga adhabu hiyo na kudai kuwa utoaji wa uhai wa mtu ni kinyume cha Katiba ya nchi. Hata hivyo majaji wawili, walikubaliana na adhabu ya kifo iliyokuwa imetolewa na Mahakama Kuu.
  Akifafanua kuhusu pingamizi la Jaji Kileo, Mgeta alisema mahakama ya Rufani inasikiliza rufaa kwa kutumia jopo la majaji, hivyo pingamizi hilo haliwezi kuzuia adhabu kutolewa.
  Kijalo alihukumiwa kunyongwa Februari 7, 2007 na Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya wakati watuhumiwa wengine watatu waliokuwa wamehukumiwa na mtuhumiwa huyo kufia mahabusu kwa maradhi mbalimbali.
  Aliyetoa hukumu hiyo ni Jaji wa Mahakama Kuu, Othman Chande, baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri.
  Alitoa hukumu hiyo kama fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo katika jamii.
  Watuhumiwa wengine walioshirikiana na Kijalo walitajwa kuwa ni Anyandwile Mtafya, Edwin Steven na Richard Kajula, ambao kwa pamoja ilielezwa kuwa walimchuna ngozi marehemu Ezekia kisha kutupa maiti yake.
  Watuhumiwa hao walifariki dunia wakiwa mahabusu kutokana na maradhi yaliyowakabili na mahakama iliendelea na mashitaka dhidi ya Kijalo, ambaye alikutwa na hatia kutokana na ushahidi sahihi uliopatikana.

  http://www.mzalendo.net/mchunaji-ngozi-ahukumiwa-kunyongwa
   
 8. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #8
  Nov 10, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Maalbino wahofu kutolewa kafara uchaguzi Mkuu


  Rais wa Chama cha Maalbino Duniani, Peter Ash, amesema wanahofia mauaji dhidi yao yanaweza kuongezeka zaidi wakati Watanzania wanapoelekea katika Uchaguzi Mkuu wa mwakani.
  [​IMG]Rais wa Chama cha Maalbino Duniani, Peter Ash.

  Alisema hofu hiyo inatokana na wanasiasa wengi barani Afrika, Tanzania ikiwamo, kutegemea zaidi ushirikina katika kupata ushindi kwenye uchaguzi.
  Ash ambaye pia ni muasisi na Rais wa Asasi ya Chini ya Jua (UTSS), inayoshughulikia elimu, afya na uchumi kwa maalbino duniani, alisema hayo alipozungumza na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam jana.
  Mkutano huo na waandishi wa habari uliitishwa na Ash katika ofisi za tawi la asasi hiyo zilizoko Mikocheni ‘B’ jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kuzungumzia maendeleo ya vita dhidi ya mauaji ya maalbino katika nchi ambazo matukio ya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi vimekithiri.
  “Tunahofia mauaji dhidi ya jamii ya maalbino yanaweza kuongezeka tunapoelekea uchaguzi, kwa sababu wanasiasa wengi barani Afrika wanategemea ushirikina kupata usindi kwenye uchaguzi,” alisema Ash.
  Alisema UTSS yenye makao yake makuu nchini Canada, pamoja na mambo mengine, inatoa msaada
  kwa ajili ya kuwawezesha maalbino kwenda kupata elimu popote duniani na kwamba, wametenga zaidi ya dola za Marekani 250,000 kwa ajili ya kutekeleza mpango huo.
  Alishauri kukamilisha mchakato wa kupitisha sheria ya haki za binadamu ya kimataifa ili ianze kutumika mara moja kwa vile itasaidia kuwalinda maalbino.
  “Hata Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Ban Kin-Moon, aliwahi kueleza suala hilo alipotembelea Tanzania,” alisema Ash.
  Alisema hata Tangazo la Haki za Binadamu la Kimataifa limeeleza bayana kwamba, watu wote wana haki sawa mbele ya sheria na pia, wana haki ya kupewa ulinzi dhidi ya ubaguzi au unyanyasaji wa aina yoyote.
  Ash alisema kuwa katika kuhakikisha matukio ya mauaji ya albino hayaongezeki nchini, wao wanaiomba serikali kuhakikisha inaimarisha ulinzi kwa albino.
  Habari za kuuawa kwa maalbino, zilianza kujitokeza mwishoni mwa mwaka juzi, watu zaidi ya 30 wa jamii hiyo waliripotiwa kuuawa na wengine kukatwa sehemu za viungo na kuleta hofu kubwa miongoni mwa Watanzania.
  Hadi sasa baadhi ya watuhumiwa wa mauaji hayo wamefikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili. Hivi sasa Mahakama Kuu ya Tanzania inaendelea kusikiliza kesi mbili za mauaji ya albino katika miji ya Shinyanga na Kahama, mkoani Shinyanga.
  Kabla ya kuibuka kwa mauaji hayo, Watanzania walishuhudia ujinga mwingine unaofanana na huo, wa kuchuna watu ngozi kwa imani za kupata utajiri.
  Watu waliokuwa wakiendesha vitendo hivyo, wamekuwa wakifanya hivyo baada ya kushauriwa na baadhi ya waganga wa jadi.
  Katika kuuonyesha umma hali ilivyo, Agosti, mwaka jana, maalbino walifanya maandamano jijini Dar es Salaam yaliyopokelewa na Rais Jakaya Kikwete katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
  Katika maandamano hayo, maalbino walimweleza Rais Kikwete kwamba hali ni mbaya sana, hususan vijijini, ambako baadhi yao wamekuwa wakilazimika kulala ifikapo saa 10:00 jioni kwa hofu ya kukamatwa na wauaji.
  CHANZO: NIPASHE   
Loading...