Wauaji wa albino kunyongwa Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wauaji wa albino kunyongwa Tanzania

Discussion in 'Matangazo madogo' started by MziziMkavu, Sep 25, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Sep 25, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,612
  Likes Received: 4,603
  Trophy Points: 280
  Wauaji wa albino kunyongwa Tanzania
  [​IMG] [​IMG]
  Watu watatu wahukumiwa kifo Mahakama moja iliyopo kaskazini magharibi mwa Tanzania imetoa hukumu ya kifo kwa watu watatu baada ya kumwuua albino.
  Watu hao wamehukumiwa kunyongwa kwa kosa la kumwuua mtoto wa kiume albino mwenye umri wa miaka 14.
  Walipatikana na kosa ya kumshambulia Matatizo Dunia na kumkata miguu yake katika wilaya ya Bukombe iliyopo mkoani Shinyanga.
  Viungo vya albino hutumiwa katika dawa zinazotumiwa na baadhi ya waganga wa kienyeji wakiwaahidi wateja wao kupata utajiri.
  Tanzania imeshuhudia ongezeko la mauaji ya albino katika miaka ya hivi karibuni.
  Idadi kubwa ya watu wamekamatwa, lakini mfumo wa sheria umekuwa ukifanya kazi taratibu, hii ikiwa hukumu ya kwanza kutolewa.
  Kuna kesi nyingine 50 zinazohusu mauaji ya albino katika mahakama za nchi hiyo.
  http://www.bbc.co.uk/swahili/news/story/2009/09/090923_tz_albino.shtml
   
Loading...