Wauaji Kibiti watoa Ujumbe kuendeleza mapambano na wadhulumaji, wasema watu waendelee kutoa taarifa

Evans-Arsenal

JF-Expert Member
Jan 10, 2016
868
1,385
Siku mbili tangu kuuawa kwa polisi wawili wa Kikosi cha Usalama Barabarani ambao walikuwa kazini katika Kijiji cha Bungu B, hali ya wasiwasi imezidi baada ya wauaji hao kusambaza ujumbe unaoeleza kuwa wanaendelea kusaka askari kwa kuwa ni wadhurumaji.

Watu hao wametuma ujumbe mfupi uliondikwa kwenye karatasi na kisha kuutuma katika mitandao ya kijamii, ukidai kuwa waliouawa (japo hawajatajwa majina yao) walidhulumu watu kwa kutumia kazi zao.

“Tunawatangazia wananchi tumewaua hawa kwa sababu wanadhulumu watu kwa kutumia kazi zao na yeyote atakayefanya kazi hapa au nje ya hapa tutamtafuta hata nyumbani kwake. Sisi tumejitolea kufa kuliko kuishi, kwa hiyo dereva au raia popote uwaonapo toa taarifa iwe nyumbani au kazini,” unasema ujumbe huo.

“Hakuna njia ya kumaliza dhuluma isipokuwa chuma tu, hapa chuma tuuu!”

Ujumbe huo ambao umeandikwa kwa mkono kwa kutumia kalamu ya rangi ya bluu unadaiwa kuwa unazungumzia vifo vya askari polisi wawili wa Kituo cha Polisi Kibiti, Sajent Salum na PC Masola waliouawa kwa kupigwa risasi wakiwa kazini.

Mmoja wa madiwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti (jina tunalo) alisema ujumbe huo unawalenga askari wa kawaida na wa Kikosi cha Usalama Barabarani.

Diwani huyo alisema kundi hilo linalofanya mauaji katika wilaya za Kibiti na Rufiji bado lipo na lina nguvu.

“Linaonyesha bado lina uwezo mkubwa wa kufanya mauaji na kutokomea kusikojulikana,” alisema.

Alisema kwa sasa Serikali inapaswa kuongeza nguvu zaidi ya wapelelezi ili kukomesha kikundi hicho ambacho hakijajulikana kinafanya hivyo kwa sababu zipi na wala kinakojificha.

Akizungumzia ujumbe huo, kamanda wa polisi wa Pwani, Onesmo Lyanga alisema Jeshi la Polisi litaendelea kuwasaka.

“Tutapambana nao tu,” alisema Kamanda Lyanga na kukata simu.

Mkuu w Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro alisema wakati alipozungumza na wazee wa wilaya za Kibiti na Rufiji, kuwa wanaoendesha mauaji hayo watalipwa ubaya kama wao wanavyofanya.

Chanzo: Mwananchi Gazeti
 
Ujumbe unaandikwa kwenye karatasi na peni ya bluu utadhani tupo enzi za TANU! Kumbe level ya kundi lililoanza kujijengea umaarufu ni kata.
Rudisheni wanajeshi wetu kambini, aina ya madai ya kundi hili ni ya kijinga sana, hatuitaji nguvu kubwa kuwanasa.
 
Polisi wasikomae kupambana nao sana wakati mwingine wafanyie kazi Motives za hawa jamaa zinazopelekea wakafanya hayo mauwaji,kama polisi wa usalama barabarani wamekuwa TRA au wanyonyaji wajirekebishe basi wakati mwingine makosa ya barabarani yanaweza tatuliwa kwa kuwaelimisha madereva na abiria na sio tu kila mara ni Faini elfu 30 ni kubwa kipindi hiki inaumiza na ukizingatia biashara zimedorora
 
duuh kumbe wanasababu na inawezekana zikawa za msingi upande wao na mbaya zaidi waiendelea kuongea wanaweza wakajikusanyia wafasi wengi ambao kwa njiamoja au nyingine wamewahi kudhulumiwa na polisi au vyombo vingine vya dola, nawaza tu kwa sauti kama mtandao wao ukienea nchi nzima si itakua syria?
 
Back
Top Bottom