Wauaji Kibiti watoa Ujumbe kuendeleza mapambano na wadhulumaji, wasema watu waendelee kutoa taarifa

Siku mbili tangu kuuawa kwa polisi wawili wa Kikosi cha Usalama Barabarani ambao walikuwa kazini katika Kijiji cha Bungu B, hali ya wasiwasi imezidi baada ya wauaji hao kusambaza ujumbe unaoeleza kuwa wanaendelea kusaka askari kwa kuwa ni wadhurumaji.
Watu hao wametuma ujumbe mfupi uliondikwa kwenye karatasi na kisha kuutuma katika mitandao ya kijamii, ukidai kuwa waliouawa (japo hawajatajwa majina yao) walidhulumu watu kwa kutumia kazi zao.

“Tunawatangazia wananchi tumewaua hawa kwa sababu wanadhulumu watu kwa kutumia kazi zao na yeyote atakayefanya kazi hapa au nje ya hapa tutamtafuta hata nyumbani kwake. Sisi tumejitolea kufa kuliko kuishi, kwa hiyo dereva au raia popote uwaonapo toa taarifa iwe nyumbani au kazini,” unasema ujumbe huo.
“Hakuna njia ya kumaliza dhuluma isipokuwa chuma tu, hapa chuma tuuu!”
Ujumbe huo ambao umeandikwa kwa mkono kwa kutumia kalamu ya rangi ya bluu unadaiwa kuwa unazungumzia vifo vya askari polisi wawili wa Kituo cha Polisi Kibiti, Sajent Salum na PC Masola waliouawa kwa kupigwa risasi wakiwa kazini.
Mmoja wa madiwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti (jina tunalo) alisema ujumbe huo unawalenga askari wa kawaida na wa Kikosi cha Usalama Barabarani.
Diwani huyo alisema kundi hilo linalofanya mauaji katika wilaya za Kibiti na Rufiji bado lipo na lina nguvu.
“Linaonyesha bado lina uwezo mkubwa wa kufanya mauaji na kutokomea kusikojulikana,” alisema.

Alisema kwa sasa Serikali inapaswa kuongeza nguvu zaidi ya wapelelezi ili kukomesha kikundi hicho ambacho hakijajulikana kinafanya hivyo kwa sababu zipi na wala kinakojificha.
Akizungumzia ujumbe huo, kamanda wa polisi wa Pwani, Onesmo Lyanga alisema Jeshi la Polisi litaendelea kuwasaka.
“Tutapambana nao tu,” alisema Kamanda Lyanga na kukata simu.

Mkuu w Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro alisema wakati alipozungumza na wazee wa wilaya za Kibiti na Rufiji, kuwa wanaoendesha mauaji hayo watalipwa ubaya kama wao wanavyofanya.

Source:
Mwananchi Gazeti


Huyo diwani asubiri Noah nyeusi.
 
Annoyance! Maadam wananchi hawataki kushirikiana na dola polisi wote warudi mjini kupiga hela za brashi.Kibiti watajisoti out wenyewe.
Kibiti mkiiacha kwa wapiganaji, mjini hakutakalika. Mi nashauri aende Kule mzee wa misukule, akawakemee, wakigoma awataje, maana anajua vitu Vingi, ambavyo binadamu wa kawaida havijui
 
Askarii mmoja alimuuliza YESU ..''na sisi je tufanye nini? Yesu akamjibu MSIDHULUMU WALA KUWASHTAKI WATU KWA UONGO...

Napinga mauaji ya askari wetu ila pia napinga dhuruma,uonevo na unyanyasaji unaofanywa na askari.
 
Mwenyenzi Mungu atuepushe na janga hili la mauaji. Hamna kitu kizuri kama Amani. Mengine yote ni subsets
 
Afadhali wamesema agenda yao.jeshi la polisi lijipime kiwango cha utendaji wake kwa misingi ya sheria na haki.
Hawa watu ni wa Kudeal na kumalizana nao kabla hawajaenea.
(japokuwa hata polisi wana tabia Zach kishenzi zisizovumilika)

Ukikubali kwenda na matakwa yao wakifanikisha moja, wana demand na kingine.

Ndio maana Marekani raia wao akikamatwa mateka wakiambiwa watoe hata tshs 10,000 hawatoi
 
Nchi hii haina wataalam wazuri wa IT , wanashindwa Ku trace eneo LA kibiti kwa Satellite ! Bado Tupo nyumaa saaNa kitaaluma.
 
Wauaji Watakuwa Wanajua Mbinu Zote Za Kijasusi Ndio Maana Wanaipa Tabu Serikali Ila Watajulikana Tu
 
Back
Top Bottom