Kijogoodi
JF-Expert Member
- Mar 29, 2021
- 1,363
- 2,372
Wakati Magufuli anatenga zaidi ya trillion mbili kwa ajili ya kuchimba na kupanua bandari ya Mtwara, Dar ,Tanga na ile ya Kalema Chadema walipinga na kuita hayo ni matumizi mabaya ya pesa za uma.!
---' ---- ----- ---
Mtwara. Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Mkoa wa Mtwara imepokea mtambo mkubwa (Crane) kwa ajili ya kupakulia mizigo bandarini yenye uwezo wa kwenda zaidi ya mita 45 ndani ya maji.
Akizungumza wakati wa kupakua mtambo huo Kaimu Meneja wa Bandari Mtwara, Norbert Kalembwe amesema kuwa mtambo huo utasaidia kuongeza kasi ya upakuaji mizigo bandarini kwa meli za aina zote.
Amesema kuwa mtambo huo una vipande zaidi ya 160 ambavyo vitaungwa na kupata mtambo mmoja utakaokuwa ukitembea kwenye reli iliyopo ndani ya bandari.
"Mtambo huu umeletwa na meli mbili mahususi kwaajili ya kuhudumia shehena ya makasha umeagizwa na Serikali crane moja inaunda vipande 160"
"Unauwezo wa kwenda ndani ya bahari kwa mita 45 unauwezo wa kichukua mzigo umbali huo itatembea kwenye reli mwanzo wa gati hadi mwisho wa reli meli ndogo mbili zinaweza kujipanga lakini huu mtambo ukaenda kichukua meli ya pili. Ni sehemu ya makakati wa Serikali kuboresha Bandari ya Mtwara." Amesema Kalembwe
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanal Ahmed Abbas amesema kuwa kufika kwa mtambo huo kutaongeza kasi ya upakuaji wa mizigo.
"Mtambo huu kwetu ni fursa na umekuja kufungua Bandari hii ambapo kwa sasa meli zitakuja bila crane na tutakuwa na uwezo wa kupaku mizigo hapa hapa." amesema Kanal Abbas