WaTZ wananyimwa fursa za jumuiya ya africa mashariki? Ni amri au ni sheria?

Ziroseventytwo

JF-Expert Member
Mar 27, 2011
7,961
13,589
Kwa kutokuelewa,au kutokujua,baadhi ya wafanya biashara wameshindwa kufanya shughuli zao kwa uhuru kufuatia marufuku iliyowekwa kwa amri(sijui) au kwa sheria(sijui) kusafirisha mazao ya chakula hususani mahindi kwenda nchi ya kenya kupitia mpaka wa tarekea...ni nini maana ya soko la pamoja? Hawa polisi wanaosumbua watu hapo rombo wanafanya kazi kwa sheria au amri? Mimi ni muadhirika wa hawa jamaa. (polisi)WanaJF, fursa za EAC ni zipi? Naomba kuwasilisha
 
Bei ya mahindi Dar,arusha iko juu.
karatu wanakufa njaa halafu wewe unaenda kuuza mahindi kenya.wewe sio mzalendo!safi sana polisi wa tarakea.
 
Bei ya mahindi Dar,arusha iko juu.
karatu wanakufa njaa halafu wewe unaenda kuuza mahindi kenya.wewe sio mzalendo!safi sana polisi wa tarakea.

mkuu hapa 2nazungumzia fursa, na tuliambiwa tuchangamkie, jibu hoja ni amri au sheria? Kwani mkulima anatakiwa kuuza mazao yake wapi,dsm na arusha?
 
Niliwahi ksikia jamaa wa serikalini wanaliongelea hili kuwa kama wataruhusu sana kuuza nje basi inaweza kuleta shida kwa soko la ndani kwani hii bidhaa inaweza kwenda juu sana kwa kuwa mahitaji ya ndani yatakuwa juu na supply itakuwa ndogo. Kama ni kweli basi ilikuwa ni kwa ajili ya kumpunguzia maumivu mtz "KAMA NI KWELI" nkaona kuna lojic hapa!
 
mkuu hapa 2nazungumzia fursa, na tuliambiwa tuchangamkie, jibu hoja ni amri au sheria? Kwani mkulima anatakiwa kuuza mazao yake wapi,dsm na arusha?

fursa ulizoziona ni kuuza chakula kenya wakati karatu watanzania wanakufa na njaa!
 
ni kisheria ndugu, huruhusiwi kuexport chakula mpaka kwa kibali maalum. Kibali hicho kinatoka wizara ya kilimo na chakula na ni mpaka wajiridhishe kuwa ipo surplus kubwa ya chakula ndio ombi lako linaweza kukubaliwa. kwa hiyo ndugu badilisha biashara, kwa hali ya hewa ilivyo sasa hivi tanzania sidhani kama unaweza pata hicho kibali labda upitie njia za panya ambazo sio uzalendo.
 
Back
Top Bottom