Watanzania wamechoka sasa

Maseke ya Meme

JF-Expert Member
Jul 11, 2007
695
914
Watu wenye hasira wachoma moto makao ya polisi

2007-10-09 11:13:02
Na Renatus Masuguliko, PST Chato


Watu 56 wanashikiliwa na polisi mkoani Kagera kwa kuhusika na vurugu za kuchoma moto makao makuu ya polisi wilayani Chato, kuharibu ofisi za mahakama ya mwanzo, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na kuwajeruhi polisi watano akiwemo Kamanda wa Polisi wa Wilaya.

Tukio hilo lilitokea juzi jioni baada ya kuwepo kwa uvumi wa kukamatwa kwa watu watatu, akiwemo mwanamke mmoja wanaoadaiwa kuwa na ngozi ya binadamu.

Kamada wa Polisi wa Mkoa wa Kagera, Bw. Abdallah Musika, alithibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kwamba mara baada ya kupata taarifa hizo alikwenda eneo la tukio, kurejesha utulivu.

Ni kweli kituo cha makao makuu ya polisi wilaya kimechomwa kwa moto na wananchi na kisha kuvunja na kuharibu majengo na nyaraka za serikali zilizokuwepo katika majengo ya mahakama ya mwanzo ya Chato, alisema.

Alisema kuwa wananchi zaidi ya 300 wanadaiwa kushiriki katika tukio hilo.

Hata hivyo, alisema uvumi huo haukuwa na ukweli wowote wala kuwepo kwa tukio la kukamatwa kwa mtu anayetuhumiwa kujihusisha na uchunaji ngozi.

Kamanda Musika alisema hadi jana mchana watu 35 walikuwa wanashikiliwa kuhusiana na tukio hilo na polisi inaendelea na upelelezi kufahamu chanzo cha kuenezwa kwa uvumi huo.

Alisema hasira za wananchi hao ndizo zilizosababisha baadhi yao kukasirishwa na kitendo hicho ambapo walikusanyika na kuanza maandamano hadi kituoni hapo wakitaka wapewe watuhumiwa hao waliokuwa wamewekwa chini ya ulinzi na polisi jambo ambalo lilipingwa na polisi wa kituo hicho.

Habari zaidi kutoka eneo la tukio zinadai kuwa maandamano ya wananchi hao yalianzia kwenye ofisi ya makao makuu ya CCM wilaya baada ya watu kuhamasishana na kuanza maandamano kabla ya kuvamia majengo hayo.

Alisema watu hao waliokuwa wamebeba silaha mbalimbali zikiwemo marungu, walipofika hapo walitaka kuchukua sheria mkononi wakidai walikuwa wanawahitaji watuhumiwa wanaodaiwa kuchuna ngozi za binadamu hatua iliyozusha mapambano kati yao na polisi waliokuwepo kituoni.

Katika mtafaruku huo wananchi hao waliamua kuchukua sheria mkononi kwa madai kuwa kulikuwepo na mikakati ya kuwahamisha watuhumiwa kutoka kituo kikuu cha wilaya kuwapeleka kusikojulikana, hatua iliyosababisha kuhisi wamehifadhiwa katika ofisi walizozivamia.

Baada ya kutoka kituo cha polisi waliendelea na zoezi lao kwa kuvamia ofisi ya mkuu wa wilaya na baadaye ofisi ya mahakama ya mwanzo.

Kufuatia vurugu hizo polisi waliomba msaada zaidi kutoka Kikosi cha askari wa kuzuia ghasia (FFU), kilichoongozwa na Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Bw. Abdallah Msika.

Polisi ilifanikiwa kuwakamata waandamanaji wachache baada ya wengine kukimbia.

Akizungumza na Mwandishi wa PST, Kamanda Musika alisema kuwa amelazimika kuwepo kwenye zoezi hilo kuhakikisha haki inatendeka kwa kubaini ukweli wa chanzo na mazingira ya tukio hilo lilivyotokea na kuwa watakaobainika kuwa chanzo watawajibishwa.

Katika taarifa yake Kamanda Musika maeahidi kutoa ufafanuzi zaidi mara baada ya uchunguzi wa awali kukamilika na kutaka kuwepo na uvumilivu.

SOURCE: Nipashe
 
Watu wenye hasira wachoma moto makao ya polisi

------
Tukio hilo lilitokea juzi jioni baada ya kuwepo kwa uvumi wa kukamatwa kwa watu watatu, akiwemo mwanamke mmoja wanaoadaiwa kuwa na ngozi ya binadamu.
------

SOURCE: Nipashe

Kwa wenye kupenda machafuko...bahati mbaya tukio haliusiani na siasa za chuki zinazopandwa kwa nguvu zote.
 
wananchi hawana imani tena na vyombo vya dola ambavyo JK anawataka watu wavitumie. itafika mahali wataingia wenyewe bungeni. Hili ni tukio la pili kufuatia lile la Kanali Masawe Dc wa kinondoni na wananchi wa Chasimba.

Na bado siku watapoteza imani na Rais, hili sijui nalo limehubiriwa na wapinzani wasio itakia mema nchi.

Mafisadi ndio wanaitakia mema nchi
 
Pamoja na matukio yote haya bado viongozi wanachapa usingizi,Kelele za mlango hazimzuii mwenye nyumba ......
 
huko ni kuonyesha ni kwa jninsi gani watz wamechoka na uongozi mbovu uliopo kuanzia ngazi ya kijiji/mtaaa mpaka ngazi ya taifa.
ipo siku mambo yatakuwa hivyo bungeni na ikulu kama hawa jamaa hawatabadilika
 
I propose to establish a new political party which will go by the name TANU (Tanzania African National Union). the aim of the party will be to decolonise Tanzania from neo-colonialism , supervise and utilize our resources for the benifits of all Tanzanians and the generations to come
 
Mwaka huo walichoka je sasa wapo taabani au ndio kazi iendelee mpaka waTanzania badala ya kuchoka na kuwa taabani wasinyae kabisa.
 
Back
Top Bottom