Watz tumelipa milion 180 alizotafuna mama Mongela Bunge la Afrika

Malafyale

JF-Expert Member
Aug 11, 2008
13,813
11,126
Mbunge wa Karatu, Dk. Wilbroad Slaa, amesema atahoji kuhusu tuhuma zinazomkabili aliyekuwa Rais wa Bunge la Afrika, Balozi Getrude Mongella za matumizi mabaya ya Sh. milioni 180 za bunge hilo wakati wa kujadili ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Fedha za Serikali (CAG).

Wiki iliyopita, aliahidi kulipenyeza suala hilo bungeni ili wabunge waihoji serikali sababu za kumlipia Mongella fedha hizo kama njia ya kumnusuru.

“Hatuoni sababu za kupoteza muda kumzungumzia Mongella ambaye si chochote tena kwa kuwa ameshatoka katika wadhifa huo,” alisema Dk. Slaa alipozungumza na gazeti hili jana.

Alisema kama itabainika katika ripoti ya CAG kuwa serikali ilimlipia fedha hizo mali ya walipa kodi, wataitaka izirejeshe na Mongella aadhibiwe.

Alisema kitu ambacho kinaweza kuwalazimisha kumlipua Mongella bungeni ni kama watabaini kuwa bado anaendelea kuitumia ofisi ya Rais wa Bunge la Afrika.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, amesema hoja kuhusu uhalali wa serikali kulipa Sh. milioni 180 zilizopotezwa na aliyekuwa Rais wa Bunge la Afrika, Balozi Getrude Mongella alipokuwa akishikilia wadhifa huo, haina hadhi ya kujadiliwa kwa vile ni jambo dogo kulinganisha na sababu iliyomfanya aachie ngazi katika Bunge hilo.

Balozi Mongella aliachia nafasi yake katika Bunge hilo Juni 2, mwaka huu na baadaye Mbunge wa Karatu (Chadema), Dk. Willibrod Slaa alimtuhumu kupoteza fedha hizo, ambazo alisema zimelipwa na serikali.

Membe alisema hayo juzi mjini Dodoma alipozungumza na Nipashe na kuongeza:

“Nenda ukamuulize Mongella akueleze yaliyomsibu Afrika Kusini. Umuulize kwanini aliamua kuachia Urais wa Bunge la Afrika kabla ya muda wake kufika, atakueleza mambo mengi, lakini hiyo ya serikali kumlipia fedha ni ‘kachembe kadogo’ mno.”

Alisema anashauri kuulizwa Mongella kwa vile tuhuma za kumhusisha na upotevu wa fedha hizo, inawezekana zinatokana na wivu au tatizo la utawala au ukaguzi mbovu wa hesabu. Membe alisema pamoja na kwamba, serikali kumlipia madeni Mongella siyo kosa wala dhambi, suala hilo limegubikwa na utata kwani wanaotoa madai hayo hawajafafanua zilikopelekwa fedha hizo kutekeleza malipo hayo.

Alisema Mongella alikuwa Rais wa Bunge la Afrika, hivyo kama kweli serikali imelipa fedha hizo, aliyepaswa kulipwa alitakiwa awe ni Bunge ama Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU) au Mongella mwenyewe, jambo ambalo wanaotoa madai hayo hawajaainisha.

Juni 15, mwaka huu, Nipashe ilimkariri Dk. Slaa akisema kwamba, taarifa za uhakika alizonazo zinaonyesha kwamba Balozi Mongella alipoteza kiasi hicho cha fedha ambacho alidai kuwa serikali imekilipa kwa kutumia fedha za walipakodi badala ya kumwajibisha kwa kuisababishia serikali hasara. Dk. Slaa alieleza kushangazwa na kauli ya Mongella kuwaita watu wanaohoji matumizi mabaya ya madaraka aliyofanya kuwa ni wahuni wa kisiasa badala ya kujibu tuhuma zinazoelekezwa kwake kwa kutumia hoja thabiti.

Alisema Mongella anapaswa kutambua kwamba, wananchi wanahitaji kufahamu uadilifu wake alipokuwa akiiwakilisha nchi kwenye chombo hicho cha Afrika na uhalali wake wa kutumia fedha hizo kinyume na taratibu.

Kutokana na hali hiyo, alisema ataipenyeza hoja hiyo bungeni ili chombo hicho kiweze kuihoji serikali na kuongeza kuwa iwapo serikali itashindwa kutoa ufafanuzi wa kina wa jambo hilo, atamshtaki Balozi Mongella, ambaye ni Mbunge wa Ukerewe (CCM) kwa Watanzania ambao fedha zao zimetumika kulipia ubadhirifu huo.
 
Habari hii imeniskitisha kuliko habari yeyote ile labda toka nizaliwe!hakika na sijaamini hadi nilipohakikishiwa na mtu wa karibu pale hazina kuwa ni kweli serikali kutumia hela za kodi yetu wamemlipia mama Mongela zaidi ya milion 180 ambazo alizitumia kwa shughuli zake binafsi akiwa kiongozi wa ngazi za juu wa Bunge la Afrika!
Hii naweza kusema"inatokea tu tz"yaani mtu akwapue hela za jumuia,na azitumie kwa faida yake binafsi na serikali kuu imlipie?sijawahi ona hii duniani haki ya Mungu naapia!
Maneno ya waziri Membe kuwa kujadili ulipwaji wa milion 180 alizokwapua mama Maongela ni suala dogo nalo limeniskitisha sana na sasa naelewa vyema kuwa mawaziri wetu tumilion 180 kwao ni tudogo sana<inasikitisha mno!
Na kuhusu habari za waziri membe kuwa habari za hela hizo na ulipwaje wake hazisisimui kama ukielezwa sababu za serikali kulipa hela hizo kwa niaba ya Mongela pia hazina hata chemba ya"sense"!
Liwalo na liwe,hela zetu walipa kodi milion 180 tunazitaka zirudishwe,kama Mama Mongela alisingiziwa kuhusu kupotea kwa hela hizo aende mahakamani kudai haki yake,lkn sio kumaliza mambo kwa kutumia migongo yetu sisi walala hoi.
Milion 180 zingepelekwa kwa wanafunzi wa chuo kikuu walikosa mikopo tungeongeza wasomi wangapi?We need our money back right away,shame on you mama Mongela!
 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, amesema hoja kuhusu uhalali wa serikali kulipa Sh. milioni 180 zilizopotezwa na aliyekuwa Rais wa Bunge la Afrika, Balozi Getrude Mongella alipokuwa akishikilia wadhifa huo, haina hadhi ya kujadiliwa kwa vile ni jambo dogo kulinganisha na sababu iliyomfanya aachie ngazi katika Bunge hilo.

Huu ni utawala wa KIIMLA unaoporomosha Tanzania yetu. Maadili ya kazi ni jambo la msingi na si la ku-compromise.

Kama Waziri wa Mambo ya Nje, Mh. Membe nategemea ungelijua ni kiasi gani cha fedha kimefukuzisha ubunge baadhi ya Wabunge kwenye nchi ya Uingereza walio wafadhili wakuu wa bajeti yetu!!

Hakuna jambo dogo kwenye matumizi mabaya ya ofisi. Hoja hii inahitaji kujadiliwa, tusikubali mambo ya ubabe ubabe haya Watanzania kutoka kwa viongozi wetu ambao tungelipenda kabisa tuwaheshimu, lakini wanajivunjia heshima wao wenyewe. Jambo dogo lisingemfanya Mh. Mama Mongella aache kazi.
 
Duh ebwana ee yaani baada ya kutafuna hela serikali ikakava deni..

Nchi kweli inaliwa na wenye meno.
 
Membe ana maana gani anaposema kuwa hizo milioni 180 ni suala dogo kulingana na mizengwe alyokumbana nayo mongella? kwani mizengwe anayokumbana naye ina uhusiano gani wa moja kwa moja na fedha za walipa kodi mapaka zichukuliwe kumbail out? ni vema angetueleza kinagaubaga hayoo masuala mengine ili tuone kuwa hayo mamilioni ni non issue si kutuletea longolongo kama hizi
 
"Bernard Membe, amesema hoja kuhusu uhalali wa serikali kulipa Sh. milioni 180 zilizopotezwa na aliyekuwa Rais wa Bunge la Afrika, Balozi Getrude Mongella alipokuwa akishikilia wadhifa huo, haina hadhi ya kujadiliwa kwa vile ni jambo dogo"
Membe huenda akawa na mawazo mgando, huwezi kusema kitu kidogo wakati wenzako wamechachamaa hata kutaka aachie ngazi ya uraisi.Membe jimboni kwako sehemu nyingi ni barabara za mchanga; yaani hizo za kifusi hakuna[hapa sizungumzii za lami]. mtu mwenye mawazo mgando hafikirii hizi fedha zinaweza kutengeneza barabara za changarawe umbali gani au kujenga madaraja ya uhakika mangapi kuliko kumwachia mtu mmoja anayetumia kwa "urembo".

lakini hiyo ya serikali kumlipia fedha ni ‘kachembe kadogo’ mno.
Kweli.....kweli huu ni wendawazimu wa kulewa madaraka.Shule ngapi a sekondari zimefungwa mapema kwa kuepusha migogoiro ya chakula kwa sababu hakuna pesa? Leo unasema ni pesa kidogo. Mawazo mgando.
ndiyo niwendawazimu kumlipia mwizi deni analodaiwa kwasababu ya wizi wake toka kwenye kihenge cha familia ambayo haijui kesho yao itakuwaje,ambayo baba umemtuma kaka mdogo katika familia kwenda kuomba msaada kwa rafiki yake bibi japo unga na nauli ya watoto.Halafu akisha mlipia hilo deni mwizi baba anasema ni fedha kidigo hiyo niliyoitoa!!! Kachembe kadogo si kadogo tu bali kadogo "mno".

Membe alisema pamoja na kwamba, serikali kumlipia madeni Mongella siyo kosa wala dhambi,suala hilo limegubikwa na utata kwani wanaotoa madai hayo hawajafafanua zilikopelekwa fedha hizo kutekeleza malipo hayo.

Aibu! kutoa fedha ambayo ingewafaa wanyonge na kusema si dhambi wala kosa.

Sasa kama hawajafafanua zilikopelekwa nini kiherere cha kwenda kumlipia mlikitoa wapi wakati mnafahamu kuna technicallity? Shame upon you!
 
Hii ni nchi ya ajabu sana, na huyu mama ndio kweli katuwakilisha WaTanzania kwenye medani ya kimataifa kuhusu UFISADI kivitendo,
haya mambo ya Ufisadi wa WaTanzania yameshajulikana almost Africa nzima kama sio dunia na kwa kweli imetushushia sana credibility yetu, sasa huyu mama baada ya kwenda kisafisha nchi yeye ndio kaenda kuichafua zaidi tena hadharani
mimi sidhani kama kweli watanzania walivyokuwa wanaeshimika kimataifa kama Salim A Salimu, Bgd. Hashimu Mbita, Prof Haroub Othman, Asha Migiro, Tibaijuka na Wengineo hiyo heshima kama kweli bado hipo,
Sasa ubovu wa setrikali bado ni uleule tu, mtu kakutwa na kashfa kubwa lakini bado watu wanamfanyia sherehe na kumchinjia ngombe, hivi hata hao wa kimataifa watatuonaje kwamba huyu mama kachemsha lakini Serikali inambeba hivyohivyo kimataifa tena hadharani, sisi hatujuhi hivyo visenti kavitumia wapi, lakini fedha yangu ndio ilipie deni lake, kama kajenga basi waTanzania ndio tulimjengea, kama kasomesha watoto, basi ndio watanzania wote tuliowasomesha watoto wa Mama Mongell wakati wakwetu wanafukuzwa Vyuoni, ni aibu sana kwa serikali

WaTanzania tunaitaji Second Rebelation, ya kututoa kwenye hii phase
 
Jamani TZ inakwenda wapi??180m kama ingekuwa kuongeza kwenye madawa kila mwezi mngesema hakuna....watu wetu wanakufa vijijini kukosa dawa analipiwa mtu alietumbua faida yake kweli nchi haina mwenyewe haki tena
 
"Bernard Membe, amesema hoja kuhusu uhalali wa serikali kulipa Sh. milioni 180 zilizopotezwa na aliyekuwa Rais wa Bunge la Afrika, Balozi Getrude Mongella alipokuwa akishikilia wadhifa huo, haina hadhi ya kujadiliwa kwa vile ni jambo dogo"
Membe huenda akawa na mawazo mgando, huwezi kusema kitu kidogo wakati wenzako wamechachamaa hata kutaka aachie ngazi ya uraisi.Membe jimboni kwako sehemu nyingi ni barabara za mchanga; yaani hizo za kifusi hakuna[hapa sizungumzii za lami]. mtu mwenye mawazo mgando hafikirii hizi fedha zinaweza kutengeneza barabara za changarawe umbali gani au kujenga madaraja ya uhakika mangapi kuliko kumwachia mtu mmoja anayetumia kwa "urembo".

lakini hiyo ya serikali kumlipia fedha ni ‘kachembe kadogo’ mno.
Kweli.....kweli huu ni wendawazimu wa kulewa madaraka.Shule ngapi a sekondari zimefungwa mapema kwa kuepusha migogoiro ya chakula kwa sababu hakuna pesa? Leo unasema ni pesa kidogo. Mawazo mgando.
ndiyo niwendawazimu kumlipia mwizi deni analodaiwa kwasababu ya wizi wake toka kwenye kihenge cha familia ambayo haijui kesho yao itakuwaje,ambayo baba umemtuma kaka mdogo katika familia kwenda kuomba msaada kwa rafiki yake bibi japo unga na nauli ya watoto.Halafu akisha mlipia hilo deni mwizi baba anasema ni fedha kidigo hiyo niliyoitoa!!! Kachembe kadogo si kadogo tu bali kadogo "mno".

Membe alisema pamoja na kwamba, serikali kumlipia madeni Mongella siyo kosa wala dhambi,suala hilo limegubikwa na utata kwani wanaotoa madai hayo hawajafafanua zilikopelekwa fedha hizo kutekeleza malipo hayo.

Aibu! kutoa fedha ambayo ingewafaa wanyonge na kusema si dhambi wala kosa.

Sasa kama hawajafafanua zilikopelekwa nini kiherere cha kwenda kumlipia mlikitoa wapi wakati mnafahamu kuna technicallity? Shame upon you!

Kwa hiyo Membe anataka kupingana na Audit report ya KPMG? sasa kama hataki kukubali Independent Audit report , atamwamini nani ? Au kwa kuwa na yeye anafuja Pesa hivyo hivyo ndio maana anasema 180millioni ni jambo dogo, basi ujue wamezoe kupiga mabillioni ndio wanaona pesa.
 
Duh ebwana ee yaani baada ya kutafuna hela serikali ikakava deni..

Nchi kweli inaliwa na wenye meno.

Si ajabu bila hata kumuuliza Fisadi Mongella maswali mazito kuhusiana na ufisadi wake huo!!!
 
Kwa hiyo Membe anataka kupingana na Audit report ya KPMG? sasa kama hataki kukubali Independent Audit report , atamwamini nani ? Au kwa kuwa na yeye anafuja Pesa hivyo hivyo ndio maana anasema 180millioni ni jambo dogo, basi ujue wamezoe kupiga mabillioni ndio wanaona pesa.

Mh.Presdaa wa Bunge la Afrika, huenda hakutumia hizo pesa kwa manufaa yake binafsi bali kwa manufaa ya nchi na ndiyo maana Serikali inajitosa kulipa.Vinginevyo haiingia akilini ni vipi mtu afuje pesa kwa raha zake kisha serikali iingie gharama kufidia.
 
huyu mama katuaibisha sana.kaona wanaweza kufanya ufisadi tanzania basi kafikiri ata kule kuna mambumbu kama serikali ya tanzania.sasa membe anasema kumlipia mil 180 ni jambo dogo,kama mili 180 ni ndogo kwanini hawatoi hio kuwapa madawati wanafunzi? mpaka leo shule watoto wana kaa chini wao wanatafuna hela.
malipo ya mungu hapa hapa dunia na mafisadi wa ccm mungu lazima atawalaani tu mmoja mmoja kwa kula mali ya walalahoi.
 
Mh.Presdaa wa Bunge la Afrika, huenda hakutumia hizo pesa kwa manufaa yake binafsi bali kwa manufaa ya nchi na ndiyo maana Serikali inajitosa kulipa.Vinginevyo haiingia akilini ni vipi mtu afuje pesa kwa raha zake kisha serikali iingie gharama kufidia.
hakuna hela iliotumika kwa manufaa ya nchi hapo,wenzake anawaona wanafuja hela zaidi ya hapo,sasa kitu gani kimfanye yeyteachukue mil 180 kwenye bunge la africa kwa ajili ya serikali ya tanzania?
 
If what has been said is true, the next question ought to be who authorized that transaction?
 
serikali kulipia deni ni kosa kubwa na kuonesha jinsi gani serikali imejaa viongozi wenye maovu makubwa kiasi cha kuweza kusaidiana mwenzao anapokamatwa kaiba.ndio maana mafisadi nao wanalindwa mpaka leo kwa vile ni kundi moja.angekuwa nyerere hai leo angesema tuwaogope mafisadi kama ukoma.ccm ni kama ukoma sasa hivi.
 
Kauli ya Membe kwamba suala hili ni dogo linanikumbusha kuhusu yule waziri wa zamani wa Miundombinu alipodai sh 1bn/- zilikuwa ni 'vijisenti' tu. Lakini viongozi wetu ni reflection ya jamii ilivyo. Utashangaa Slaa pekee ndiye aliyeguswa na hilo suala wabunge wengine esp CCM wameuchuna tu! Ingekuwa mahali pengine kauli hiyo ilikuwa ni ya kutakiwa kujiuzulu. Kwa suala la kukwapua hela zetu azirudishe. Kama wanaona ni kidogo si angetoa mfukoni kwake? Ni lini tutapata viongozi wenye uchungu na raslimali zetu? Kiongozi unayedhani ana unafuu kumbe ni wa kutupwa. Oh, Mungu tusaidie wazaliwe akina Nyerere wengine!
 
Back
Top Bottom