WaTZ tuache kudanganywa kirahisi kwenye sakata la DOWANS | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

WaTZ tuache kudanganywa kirahisi kwenye sakata la DOWANS

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Chifunanga, Apr 1, 2011.

 1. Chifunanga

  Chifunanga JF-Expert Member

  #1
  Apr 1, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 291
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Wadau,
  Naona kama tunapelekeshwa na sisi tunaenda kama upepo.

  Sasa kuna discussion ya NANI ALIPE deni la DOWANS.

  Hii discussion haitakiwi kuwepo kabisa.

  Issue sio NANI ALIPE....issue ni kwamba HAKUNA KULIPA KABISA.

  Tuache kupoteza muda kudiscuss nani alipe, kwa sababu tukiendelea na hii discussion itaimply kuwa tumekubali kulipa na sasa issue ni nani alipe.

  Sijui nyie, lakini mi bado sijakubali kulipa, kwa hiyo discussion ya nani alipe ni useless kwangu.
   
 2. Tina

  Tina JF-Expert Member

  #2
  Apr 1, 2011
  Joined: Jul 9, 2007
  Messages: 571
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 45
  Mkuu kuna tatizo gani watu wakijadili kwamba wale waliohusika kulazimisha madudu, kukiuka sheria za manunuzi, kuibeba Richmond na kuiingiza kinyemela Dowans, huku wakiilazimisha TANESCO kukubali tu kutekeleza mambo yao kwa lazima, WALIPE WAO. Si wanajulikana. Si ndio uwajibikaji huo? Kulipa ni wajibu. Lakini si lazima serikali au TANESCO ndo walipe!
   
 3. H

  Haika JF-Expert Member

  #3
  Apr 1, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Nakubali kuwa discussion ya KATI YA TANESCO NA SERIKALI NANI ALIPE' haina haja, lakini ndiscussion ya NANI AWAJIBISHWe kwa kutufikisha HAPA nimuhimu na ijadiliwe kwa kina bila kumung'unya maneno wala majina.

  nilishawahi kusema zamani humu kuwa tunajisumbua kumtaja tu Rostam hapa.

  Cha muhimu ni kufuata TRAIL OF OF OUR MONEY' tutawapata wengi tu, sio tu huyo tunaemjua. Ila huwa nahisi watu wanaogopa kuwa na wenyewe wanaweza wakawa humo ndani.
  ugumu uko wapi, kama bajeti ilikuwa sh 1000, 300 imetumika, 700 haionekani, lazima kuna signatures, au kuna mtu kakimbia kaacha kazi, kuna account numbers, kuna bank slips, transfers zitakaazoonyesha mlolongo fulani.
  sijui kwanini kunakuwa na shida, naomba kueleweshwa.
  Saa ingine nahisi, kuwa wanakubali atajwe tu huyo, ili afunike mauozo mengine.
   
Loading...