Sijui kutawaliwa sana na wakoloni kumetufanya kutozingatia kukusanya jamii na kuwa kitu kimoja na badala yake kuzingatia kutawanya watu kutokana na misingi ya itikadi , jinsia,kabila,koo,rangi,na hasa dini.
Imekuwa ikifumbiwa macho na watawala kwa muda mrefu mambo haya yakiwagawa watu mfano:
Naomba watanzania tusikubali udhalimu wa aina hii uendelee kutugawa na kuacha tukilia na ujinga iliokubuhu, maradhi(hata malaria na kipindupindu ambayo yanatokana moja kwa moja na matatizo yao kama watawala) na UMASKINI wa kupindukia.
Imekuwa ikifumbiwa macho na watawala kwa muda mrefu mambo haya yakiwagawa watu mfano:
- AL huda:Ndani ya gazet hili wakati wa uchaguzi kuna mada zakusikisitisha sana, mfano siku moja wameandika mgombea wa chama fulani hapendi wanawake wa kiislamu.Haya mambo yameachwa na ndio yanayochangia kwa kiasi kikubwa yale yaliopewa jina la majeraha ya uchaguzi.Nataka kuuliza watawala wako wapi jamani kwani haba na haba hujaza kibaba..
- Matamshi makali kwenye vyombo vya habari:Hili limejitokeza sana wakati uchaguzi wetu ukielekea mwishoni.Tulishuhudia viongozi mbalimbali wa makanisa na misikiti wakitoka mbele ya jamii kupitia vyombo vya habari wakitoa kauli ambazo kwa wengi zilionekana za kawaida lakini kwa mtu makini ilionyeesha kuna vita za ndani kwa ndani ambazo walikuwa wanapigana nazo.Hili pia limejitokeza kwenye vyombo vya habari mfano gazeti moja lilionyeasha idadi ya viongozi wa kikristo na waislamu.Huu ni mojawapo ya mpuzi ambao sikutegemea taifa langu lingekubali ufanyike