Watumishi wote wa wizara ya ardhi Morogoro kuhamishiwa mikoa mingine

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,616
141,447
Agizo limetolewa na waziri wa ardhi mh Lukuvi kwamba watumishi wote wa idara ya ardhi mkoani Morogoro wahamishiwe mikoa mingine.

Sababu za waziri Lukuvi kuchukua uamuzi huo ni watumishi hao kushindwa kutatua migogoro ya ardhi mkoani humo.

Source ITV habari!

-----------


Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi William Lukuvi ameagiza kuhamishwa watumishi wote wa sekta ya ardhi katika mkoa mzima wa Morogoro sambamba na kuanzishwa ofisi ya Ardhi Kanda ya Mashariki katika mkoa huo.

Uamuzi huo unafuatia kukithiri kwa migogoro ya ardhi katika mkoa huo licha ya jitihada mbalimbali zinazofanywa na serikali katika kutatua migogoro ya ardhi katika mkoa huo.

Lukuvi alitoa maagizo hayo tarehe 17 Mei 2019 alipokuwa alizungumza na wananchi wa Sokoine katika Kata ya Dakawa wilaya ya Mvomero mkoa wa Morogoro wakati wa ziara yake ya kutatua migogoro ya ardhi katika wilaya ya Kilosa na Mvomero.

Lukuvi alisema, baada ya kutembelea wilaya ya Kilosa amebaini watendaji wa sekta ya ardhi katika mkoa huo wamejisahau na njia pekee ya kufanya ni kuwaondoa watumishi wote wa sekta hiyo na kuwapeleka maeneo mengine kwa lengo la kupata watendaji wapya.

“Majaribio mengi yamefanyika katika mkoa wa Morogoro kama vile kupanga na kupima kila kipande cha ardhi, utoaji hati za kimila pamoja na uamuzi wa Rais John Pombe Magufuli kufuta mashamba makubwa yasiyoendelezwa lakini mambo katika sekta ya ardhi kwenye mkoa huo hayaendi” alisema Lukuvi

Aidha, Waziri Lukuvi alisema, kutokana na mkoa wa Morogoro kuendelea kuwa na migogoro ya ardhi kwa muda mrefu ameamua kuirejesha kanda ya Mashariki ambayo sasa itakuwa kanda maalum ya ardhi kwa mkoa huo itakayokuwa na wataalamu wote wa sekta ya ardhi akiwemo Kamishna Msaidizi wa Ardhi wa Kanda, Wapima, Wathamini pamoja na Wataalamu wa Mipango Miji.

Kwa mujibu wa Lukuvi, kwa sasa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ina kanda nane za ardhi nchini na kuanzishwa kanda hiyo kutawafanya wananchi wa mkoa huo kutokuwa na sababu ya kuhangaika mpaka Dodoma kushughulikia masuala ya ardhi.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alisema, kuanzishwa kwa kanda maalum Morogoro kutaufanya mkoa huo kuwa mkoa pekee Tanzania wenye kanda ya ardhi na kubainisha kuwa ofisi hiyo itatakiwa kuanza kazi mapema mwezi Julai 2019.

Aidha, Lukuvi ambaye katika ziara hiyo aliambatana na Kamishna wa Ardhi nchini Mary Makondo, Kaimu Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani Samwel Katambi, Mthamini Mkuu wa serikali Evalyne Mugasha na Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Kati Ezekiel Kitlya alisema, pamoja na uamuzi huo, ameamua kupeleka timu ya wataalamu 15 kutoka Wizarani kufanya uhakiki wa mashamba yaliyofutwa katika wilaya za Kilosa na Mvomero kwa lengo la kupima na kupanga upya mashamba ili kugawa upya mashamba hayo kwa wananchi wanaostahili na mengine kutolewa kwa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).

Vile vile, Waziri Lukuvi amepiga marufuku wamiliki wa mashamba yaliyofutwa na Raisi kurejeshewa kinyemela mashamba hayo kwa kisingizio cha kuyaendeleza na kusisitiza kuwa iwapo wamiliki wa awali wanayataka mashamba hayo itabidi waombe upya na kama watapatiwa mashamba basi watapewa kulingana na uwezo wao.

Awali Mkuu wa Idara ya Ardhi na Maliasili katika halmashauri ya wilaya ya Mvomero Rugembe Maiga alimueleza Waziri Lukuvi kuwa migogoro mikubwa ya ardhi katika wilaya ya Mvomero iko katika mipaka ya vijiji na mashamba na kubainisha kuwa wilaya hiyo ina jumla ya mashamba 12 yaliyofutwa na Raisi.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mvomero Yusufu Athuman alisema wilaya hiyo inazo changamoto kubwa katika masuala ya ardhi kwa kuwa wanachi wa wilaya hiyo wana uhitaji mkubwa wa ardhi na sehemu kubwa ya ardhi katika wilaya hiyo iko kwa watu wachache


Mtanzania
 
Agizo limetolewa na waziri wa ardhi mh Lukuvi kwamba watumishi wote wa idara ya ardhi mkoani Morogoro wahamishiwe mikoa mingine.

Sababu za waziri Lukuvi kuchukua uamuzi huo ni watumishi hao kushindwa kutatua migogoro ya ardhi mkoani humo.

Source ITV habari!
Huyu Lukuvi si ndiye alipora shamba la Sumaye na kuiaminisha dunia kwamba hilo ndio lilikuwa mgogoro pekee mkoani morogoro , sasa imekuwaje tena ?
 
Agizo limetolewa na waziri wa ardhi mh Lukuvi kwamba watumishi wote wa idara ya ardhi mkoani Morogoro wahamishiwe mikoa mingine.

Sababu za waziri Lukuvi kuchukua uamuzi huo ni watumishi hao kushindwa kutatua migogoro ya ardhi mkoani humo.

Source ITV habari!
Je hii sababu ya kuwahamisha ni ya kitafiti? Isijekuwa ni kusogeza ndugu karibu. Nimekaa Morogoro, ukiondoa Mvomero na Kilosa penye mizozo ya wafugaji na wakulima, nielezeni ni wapi kwi gine? Na ukiangalia kwa undani, hata enzi za kina Mtaka ( DC), issue ya maeneo hayo imekaa kikabila zaidi. Mfano, ukikuta Mmasai analalamika, ataungwa mkono na Masai wenzake zaidi. Je,Mwanza, Arusha, Dsm nk ndizo nazo ngome za migogoro, nako je?
 
Kuwahamisha ni UDHAIFU wa kiutendaji kwani ni mkoa gani unaopokea watumishi wavivu? Hapa Mimi naona serikali haijawa making na maana yake ni kuwa waziri ameshindwa kusimamia walio chini yake.Kwani ukiwahamisha wote kule wanapokwenda watawajibika kwa Nani? Kama siyo kueneza ubovu nchi nzima?
Rais wetu anachapa kazi halafu waziri Kama huyu anashindwa kutoa maamuzi ya kujenga anaamua kuhamisha ubofu kuusambaza kwa wengine!
Sina uwezo wa kuamrisha hatua za kumchukulia anayeshindwa kutimiza wajibu aliopewa. Ingekuwa amri yangu kauli za waziri ni jibu tosha kuwa amechoka na anastahili kupumzishwa.
VIONGOZI wa chama chetu pendwa CCM hebu tukemee tabia Kama hizi ambazo zinawapa kauli wapinzani.
 
Agizo limetolewa na waziri wa ardhi mh Lukuvi kwamba watumishi wote wa idara ya ardhi mkoani Morogoro wahamishiwe mikoa mingine.

Sababu za waziri Lukuvi kuchukua uamuzi huo ni watumishi hao kushindwa kutatua migogoro ya ardhi mkoani humo.

Source ITV habari!
Mbona Manispaa za Mkoa wa Dar es salaam ndio Balaa? Migogoro toka Wizara ikiwa Dar mpaka imehamia Dodoma.Namshauri awahamishe na Wa Mkoa wa Dsr es salaam.
 
Back
Top Bottom