Watumishi Wizara ya Afya wamkumbuka Wilson Mukama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watumishi Wizara ya Afya wamkumbuka Wilson Mukama

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by CULCULUS, Feb 2, 2012.

 1. CULCULUS

  CULCULUS Senior Member

  #1
  Feb 2, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Leo nikiwa nimevinjari ndani ya Ofisi za Wizara ya Afya kwa shughuli zangu binafsi niliingia Ofisi moja ambayo nilikuta Watumishi wapo katika mjadala mkali wa kulinganisha Uongozi wa Katibu Mkuu wa sasa Bi Blandina Nyoni na aliyekuwepo kabla Mzee Wilson Mukama ambae alihamishiwa Wizara ya Maji kisha kustaafu na baadae Kikwete akamteua kuwa Katibu Mkuu wa CCM Taifa hadi sasa.

  Watumishi waliokuwepo ambao walikuwa takribani 12 hivi walionyoesha ni jinsi gani Wilson Mukama alivyokuwa anawajali kwa kuwalipa stahili zao haraka mfano Malipo ya likizo, uhamisho, Overtime, nk. Wanakereka na jinsi Nyoni anavyoendesha Wizara kwa kutumia watu waliowataja kuwa ni maaskari wake (Informers) wa kusikiliza huyu anasema nini na yule anasema nini dhidi ya utawala wake. Kibaya zaidi wanaghadhabika na jinsi Blandina Nyoni anavyojidai ni mlinzi wa mali za serikali wakati yeye ndiye mdokozi mkubwa wa mali hizo. Kwa haraka haraka wanaonekana ni watumishi waliochoka na kuukatia tamaa na uongozi uliopo. Mmoja wao alisema hivi nanukuu: 'Licha ya kwamba ni MwanaCCM lakini tutamkumbuka sana Wilson Mukama, ni Katibu Mkuu bomba sana, hatutakuja kumpata mtu kama yeye' Mwisho wa kunukuu..
   
 2. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #2
  Feb 2, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Wamemsahau Hilda Gondwe na Mama Mwafisi. Hawa walikuwa ni vichwa.
   
 3. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #3
  Feb 2, 2012
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145

  Kwenda zao kule. Kwani matatizo ya wizara yameanza kwa Nyoni? Huyo Mukama aliwalipa fedha ngapi madaktari kama maboresho ya mishahara yao? Tuache propaganda. Nyoni ni kama Mukama tu ila katika circumstances tofauti. Hata Mukama wangegoma kipindi chake na katika mazingira kama haya yangemfika tu. Watanganyika tunaongozwa na matukio. We are really stupid.

  Nyoni ni mwanamke na nusu acheni utani. Hongera sana mwanaume aliyemwoa, if not why not?

  Huwezi kukurupuka katika mambo ya kisera na bajeti. Nyoni hiyo ni base yake. Wizara ya afya kuna siasa sana najua. Sasa wanataka kumsulubu lakini Nyoni si wizara ya afya. Yeye ni mtendaji au mfanyakazi kama yeyote wizara ya afya. Hata ikiwa wakimtoa matatizo ya wizara ya afya hayatakwisha au kabisa kutatuliwa na yeyote yule. Wizara ya afya inahitaji efforts za jumla.
   
Loading...