Watumishi wengi wa serikali mnatia huruma mno, ni katikati ya mwezi ila nimepokea zaidi ya simu 10 mkiomba msaada wa pesa

Walimu tuna haiba ya ustaha na aibu kuombaomba lakini siyo kwamba hatuishiwi ni ile tu tunatumia kwa level yetu ya salary ndogo yenye kulengwa na machoz
Mkiwa na msururu wa madeni ya nguo na mapochi bila kusahau viatu aka skuna.Mnaongoza kwa mikopo kwenye Taasisi ndogo za fedha kuanzia saccos mpaka vicoba
 
Mkuu, au unakopesha kwa riba?!!
Huwa nawapa bila riba nimegundua napoteza fedha nyingi sana kwao, hivyo nimeamua kutowakopesha tena wakitaka pesa sasa nitawaambia waende kwenye taasisi za mikopo pia mazoea yanapelekea wengi kutokurudisha pesa kwa wakati.
 
Pongezi za dhati kutoka kwangu, mna nidhamu ya fedha sana pia ndoa nyingi ambazo zinahusisha mwalimu huwa zinadumu sana sijajua mna siri gani ya kipekee kiasi hicho?
Nilihitaji kufahamu juu ya hili...walimu wanaongoza kudumisha ndoa kuliko fani zingine
 
Na mimi naweza kuja mkuu kwa ajili ya ujira? Hali mbaya.
Hapana kuna mmoja tunasumbuana ana pesa yangu nyingi, hivyo ameondoka na wema wangu wote. Sitoazima ama kukopesha mtu fedha tena sasa hivi mawajibu sina fedha ya kukopesha kama urafiki uishe tu maana wengine wanaendekeza sana urafiki mwisho wa siku hawarudishi fedha.
 
Sawa mkuu.Ila sijaomba pesa.Nimeomba kazi kama ipo.
 
Ni watumishi wa serikali kutoka idara tofouti tofouti nyeti na zisizo nyeti, watumishi hawa wa Mama Samiah Suluhu Hassani wanatia huruma mno kila ifikapo katikati ya mwezi.

Na kwa hili ilivyo kwa sasa ya vitu kupanda bei, kuna kufanya maendeleo kweli ukiwa mtumishi wa serikali?

Niwaase watumishi, pindi mnapopata mishahara yenu muache kutumia hovyo kwenye mabaa na kuhonga wanawake hovyo pasipo kufanya seaving ya 40% ya kile unachopata mwisho wa mwezi, maana kwa simu za leo nimejisikia vibaya mno na mwisho nimeshindwa kuwaelewa? Kama hiyo mishahara mnayolipwa inawatosha kweli au ni vile mmeridhika na maisha ya mishahara kwamba mna uhakika wa kuupata kila mwisho wa mwezi, na imewapelekea nyie kubweteka pasipo kufikiria kuwa na kitu cha ziada cha kuwaingizia kipato?

Ushauri kwenu mjitahidi kubadilika muishi kulingana na kipato chenu, hizi starehe mnazofanya mjini mkumbuke zina mwisho mbaya mtakuja kukumbuka umri umewatupa mkono na hakuna cha maana mlichofanya pindi mkiwa watumishi.

Mwisho kabisa niwapingeze waalimu, katika watumishi wa serikali hawa wanaongoza kuishi ndani ya mishahara yao, sijawahi kuwasikia wakililia shida kama watumishi wengine, popote mlipo walimu pokeeni pongezi zangu za dhati.
Watumishi wengi hawana nidhamu ya matumizi wanatumia pesa vibaya
 
kuhonga wanawake hovyo pasipo kufanya seaving ya 40% ya kile unachopata mwisho wa mwezi,
Unajua 40% ya salary ya mfanyakazi wa serikali? Sijaajiriwa ila 40% ni ndoto, hujaoa/hujaolewa, huna watoto, huna dependants, huna school fees wala house rent, huna wazazi ndio maana
 
Ni watumishi wa serikali kutoka idara tofouti tofouti nyeti na zisizo nyeti, watumishi hawa wa Mama Samiah Suluhu Hassani wanatia huruma mno kila ifikapo katikati ya mwezi.

Na kwa hili ilivyo kwa sasa ya vitu kupanda bei, kuna kufanya maendeleo kweli ukiwa mtumishi wa serikali?

Niwaase watumishi, pindi mnapopata mishahara yenu muache kutumia hovyo kwenye mabaa na kuhonga wanawake hovyo pasipo kufanya seaving ya 40% ya kile unachopata mwisho wa mwezi, maana kwa simu za leo nimejisikia vibaya mno na mwisho nimeshindwa kuwaelewa? Kama hiyo mishahara mnayolipwa inawatosha kweli au ni vile mmeridhika na maisha ya mishahara kwamba mna uhakika wa kuupata kila mwisho wa mwezi, na imewapelekea nyie kubweteka pasipo kufikiria kuwa na kitu cha ziada cha kuwaingizia kipato?

Ushauri kwenu mjitahidi kubadilika muishi kulingana na kipato chenu, hizi starehe mnazofanya mjini mkumbuke zina mwisho mbaya mtakuja kukumbuka umri umewatupa mkono na hakuna cha maana mlichofanya pindi mkiwa watumishi.

Mwisho kabisa niwapingeze waalimu, katika watumishi wa serikali hawa wanaongoza kuishi ndani ya mishahara yao, sijawahi kuwasikia wakililia shida kama watumishi wengine, popote mlipo walimu pokeeni pongezi zangu za dhati.
Huna lolote unafiki tu..itakua wewe ni mwalimu..kwanza walimu ndio wakopaji wa kubwa wamejaa madeni kila mahali.

#MaendeleoHayanaChama
 
Hata wanaofanya kazi Sekta binafsi, hupiga mizinga, tena wafanya biashara hao hao, inategemea na mtu anachoingiza kwa Siku au mwezi.

Kama umevuka hatua ya kuto omba msaada wa fedha kwa mwingine mshukuru Mungu, hata hivyo hao wanao kuomba ni watu wa karibu yako.
 
Back
Top Bottom