Watumishi wengi wa serikali mnatia huruma mno, ni katikati ya mwezi ila nimepokea zaidi ya simu 10 mkiomba msaada wa pesa

Sawa Comred Nyboma nadhani wamekusikia na
Wengine wesema acha sifa
Kama kina Nshomile
tatizo la watumishi wengi
Bia tamu🎶🎵
Bia tamu🎵🎶
 
Ni watumishi wa serikali kutoka idara tofouti tofouti nyeti na zisizo nyeti, watumishi hawa wa Mama Samiah Suluhu Hassani wanatia huruma mno kila ifikapo katikati ya mwezi.

Na kwa hili ilivyo kwa sasa ya vitu kupanda bei, kuna kufanya maendeleo kweli ukiwa mtumishi wa serikali?

Niwaase watumishi, pindi mnapopata mishahara yenu muache kutumia hovyo kwenye mabaa na kuhonga wanawake hovyo pasipo kufanya seaving ya 40% ya kile unachopata mwisho wa mwezi, maana kwa simu za leo nimejisikia vibaya mno na mwisho nimeshindwa kuwaelewa? Kama hiyo mishahara mnayolipwa inawatosha kweli au ni vile mmeridhika na maisha ya mishahara kwamba mna uhakika wa kuupata kila mwisho wa mwezi, na imewapelekea nyie kubweteka pasipo kufikiria kuwa na kitu cha ziada cha kuwaingizia kipato?

Ushauri kwenu mjitahidi kubadilika muishi kulingana na kipato chenu, hizi starehe mnazofanya mjini mkumbuke zina mwisho mbaya mtakuja kukumbuka umri umewatupa mkono na hakuna cha maana mlichofanya pindi mkiwa watumishi.

Mwisho kabisa niwapingeze waalimu, katika watumishi wa serikali hawa wanaongoza kuishi ndani ya mishahara yao, sijawahi kuwasikia wakililia shida kama watumishi wengine, popote mlipo walimu pokeeni pongezi zangu za dhati.
Uneamua kututangaza sasa
 
Back
Top Bottom