Watumishi watoro kazini

Jang Bo Go

JF-Expert Member
Oct 22, 2011
854
253
Habari wadau

Katika ziara ya waziri mkuu leo huko Lindi imeripotiwa na mkuu wa mkoa wa Lindi kuwa kuna zaidi ya watumishi 50 ambao ni watoro na wengine 7 ni watumishi hewa. Pia zaidi ya milioni 30 imepotea kuwalipa hao watumishi.

Sasa hawa watoro ni wale wasiofika maeneo ya kazi kwa siku kadhaa au ni wale walioenda masomoni bila ruhusa maana haijatolewa ufafanuzi? Inakuaje hapo wadau.

Kwa mtazamo wangu hakuna tofauti ya mtumishi hewa na mtumishi mtoro maana huyu mtoro nae analipwa pesa ambayo hajaifanyia kazi.

Hii vita ni ngumu sana.

Source: Channel Ten, Habari.
 
mkurugenzi yeyote anayelipa mishahara watumishi hewa ama watoro ilifaa kufungwa jela maisha. taratibu za kiutumishi zinafuatwa? kuna ukweli kwamba wakurugenzi huidhinisha mishahara ya watumishi watoro na kujilipa wenyewe. wa kulaumiwa ni serikali kuwaendekeza wakurugenzi na maafisa wa hazina wasiowaaminifu...
 
Back
Top Bottom