Ng'wanambula
Senior Member
- Oct 2, 2011
- 197
- 54
Baada ya watumishi wapatao 9932 kutumbuliwa kutokana na kuwa na vyeti fake, taarifa za uhakika tulizozipaa kutokana na uchunguzi tuliofanya zinaonyesha kuwa watumishinwengi kwenye ngazi ya Halmashauri waliokuwa na vyeti fake vya sekondari hasa form 4 walikwepa kutumbuliwa kwa kunyofoa vyeti vyao fake kwenye mafaili yao.
Inasemekana kuwa baada ya kuhisi kubanwa, wengi walikimbilia mafaili yao na kuanza kuondoa vyeti hivyo vya kughushi na hivyo kubakiza vyeti vya darasa la 7 na taaluma tu.
Kwa mantiki hiyo, kama serikali inataka kuwapata watumishi hao ni vema ikafanya uhakiki mwingine ili taarifa zitakazopatikana zikinganishwe na taarifa zilizokusanywa kwenye uhakiki wa awali.
Utagundua kuwa wengi wanwaliowasilisha vyeti vya form 4 hapo awali hawatakuwa navyo kwenye uhakiki mpya kwa kuwa vimeondolewa. Aidha, taarifa sahihi wanazo maafisa utumishi.
Pia serikali naishauri sasa ipange mishahara upya kwa wale walioondoa vyeti vya form 4 kwenye mafaili yao ili mishahara yao iendane na elimu hiyo ya darasa la 7. Wenhi utakuta ni maafisa waandamizi lakini cheti cha form 4 hakipo.
Naishauri serikali ichukie hatua.