Watumishi wabovu serikalini wafukuzwe kazi sio kuwahamishia mikoa ya pembezoni! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watumishi wabovu serikalini wafukuzwe kazi sio kuwahamishia mikoa ya pembezoni!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mwanajamii, Mar 30, 2012.

 1. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #1
  Mar 30, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  ‎'RUKWA SIYO JALALA'
  Mkuu Wa Mkoa Wa Rukwa Eng. Stella Manyanya Amesema Mkoa Wa Rukwa Siyo 'Jalala' La Kutupia Watumishi Walioshindikana Katika Mikoa Mingine Na Badala Yake Serikali Kuu Iache Tabia Ya Kuwahamishia Watumishi Wa Aina Hiyo Katika Mkoa Huo.

  Alisema Rukwa Kama Ilivyo Mikoa Mingine Nchini Inahitaji Kupiga Hatua Kimaendeleo Hivyo Watumishi Wasio Na Maadili Na Walioshindikana Ktk Mikoa Waliotoka Hawawezi Kuusaidia Mkoa Huo Ktk Harakati Zake Za Kusonga Mbele Kimaendeleo Hivyo Si Busara Kuhamishiwa Mkoani Humo. Namnukuu "Watumishi Wabovu Wasio Na Maadili Wamekuwa Wakiletwa Mkoani Rukwa Kama Adhabu, Sasa Katibu Mkuu Utumishi Upo Hapa, Tunakuomba Walioshindikana Mikoa Mingine Msiwalete Huku, Wafukuzeni Kazi, Sisi Tukiwabaini Mmewaleta Tunawarudisha Kwenu Mara Moja, Hili Sio Jalala La Watumishi Wa Aina Hiyo."

  JE NI KWELI KUPELEKWA RUKWA, SONGEA N.K KIKAZI NI ADHABU?
   
 2. maziwa ya mgando

  maziwa ya mgando Senior Member

  #2
  Mar 30, 2012
  Joined: Mar 29, 2012
  Messages: 167
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Anapiga mayowe tu naye, si akasemee bungeni.
  Huwezi fukuza mfanyakazi mbovu wakati huna kawaida ya kuwapima utendaji.

  Ajira za serikalini ni permenent, hupangiwi malendo ya kufikia kwa mwaka wala kwa kipindi cha utumishi wako.
  Wako kufukuza kwa kipimo gani? Kwa taratibu gani.
  Wizi mtupu.
   
 3. Nelsweeter

  Nelsweeter Senior Member

  #3
  Mar 30, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 141
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndio hata Kigoma
   
Loading...