Watumishi waafya mnatakiwa kuripoti kabla ya june 24

MITOCHONDRIA

Senior Member
Feb 21, 2013
147
34
Hivyo ndivyo lilivyokuwa linasomeka tangazo la wizara ya afya lilivyowataarifu, watumishi wote wa wa kada za afya. Sasa mm najiuliza kuna haja gani ya kupromise tarehe mbele ya public ambalo kutimizwa kwake ni vigumu. Leo ni tarehe 18 june hata hayo majina na jinsi walivyopangiwa maeneo yao mapya ya kazi bado, hebu wana jf mwenye infor atujuze.
 
walikuwa morogoro wanapanga nadhani kuna list mpya ya majina itatoka
Does it make sense?
Wizara inawezaje kupanga tarehe ya mwisho kuripoti lakini inashindwa kupanga tarehe ya kuanza kuripoti?

Mleta mada amesema mpaka sasa bado hata orodha ya majina ya waliopata ajira haijatolewa na haijulikani ni lini itatoka na hapo hapo tarehe ya mwisho kuripoti ni 24/Juni/2013.

Kweli Tanzania ni nchi ya kusadikika.
 
Mi naishangaa sana hii serikali ya Tanzania jinsi inavyofanya kazi kwanza ikumbukwe waziri kombani alisema kwamba watumishi wataanza kazi mei mosi, mei mosi ikaja ikapita, wizara wakatoa tangazo tarehe 28 mei na kusema mwisho wa application ni tarehe 10, ilipofika hiyo tarehe wakatoa tangazo lingine kwamba deadline itakuwa tarehe 20 lakini mwisho wa tarehe ya kuripoti ya kuripoti haikubadilishwa yaani tarehe 24, leo ni tarehe 19 bado list ya post bado haijatoka na kutokana sheria ya utumishi inawataka waajiri kutoa wiki 2 kwa watumishi wapya kuripoti kazini hii ina maana tutarajie tangazo jingine la kupeleka mbele tarehe ya kuripoti kazini. Hii nchi mpaka hasira!
 
sina lakini ilishakuwepo usiniulize wapi na lini!

acha fikira mgando, unanipa wasiwasi na elimu yako au na ww ndio form four wa mwaka nn, hoja zako hazina uzito, hiyo orodha ulinayo ni ya kwako. Wizara haijatoa orodha yoyote. Jitahidi usionyeshe madhaifu yako humu jf kuna watu wa aina tofauti. Pengine itakuchukua si chini ya miaka kumi kufika hulu tulipo.
 
acha fikira mgando, unanipa wasiwasi na elimu yako au na ww ndio form four wa mwaka nn, hoja zako hazina uzito, hiyo orodha ulinayo ni ya kwako. Wizara haijatoa orodha yoyote. Jitahidi usionyeshe madhaifu yako humu jf kuna watu wa aina tofauti. Pengine itakuchukua si chini ya miaka kumi kufika hulu tulipo.
kumbe wewe unasubiri ile ya kutolewa na wizara!ha ha ha!
 
kumbe wewe unasubiri ile ya kutolewa na wizara!ha ha ha!

sasa kwani wao walisema watatoa wapi, zaidi ya wizara kutoa orodha? acha kutuuzia chai kwenye serious issues,kama huna updates unaweza pita tu!
 
utake usitake list ya majina ipo tayari, kitambo sana wametoka morogoro. lolote laweza kutokea kutokana na vimemo katika ofisi ya katibu mkuu kutoka..... OMBA MUNGU LISIJELIKANYOFOLEWA LA KWAKO LIKAWEKWA LA NANII. ha! ha! natania tu hakuna list yoyote we subiri wizara wa post.
 
dah hawa watu wanaongoza hii wizara ni janga la taifa
kwa vile wao hawatibiwi kwny hospitali za umma ndo mana wanafanya hvyo huwezi kuongea hata siku moja kuna upungufu wafanyakazi wakelewa ....mtaani kuna madaktari wengi sana lakini hawataki kuajiri ...
ukiuliza utaambiwa bado vibali havijatoka vya kuajiri..
ila vibali na bajeti za kuwapeleka viongozi aka vigogo nje kwa ajili ya matibabu hata kama malaria vipo tele ..
kuzaliwa nchi kama hii ni majanga makubwa
 
Back
Top Bottom