Watumishi wa Wizara ya Afya wapandishwa kizimbani kwa wizi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watumishi wa Wizara ya Afya wapandishwa kizimbani kwa wizi

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Gumzo, Apr 18, 2012.

 1. G

  Gumzo JF-Expert Member

  #1
  Apr 18, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [FONT=Georgia,"Times New Roman",serif]Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Morogoro, imewafikisha mahakamani watumishi watatu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na mtumishi mmoja wa hazina ndogo, kujibu shitaka la matumizi mabaya ya fedha.

  Pia, wanashtakiwa kwa kula njama, kutumia vibaya madaraka na kushawishi kutenda kosa kinyume cha tararibu za matumizi ya fedha za umma.

  Washtakiwa hao ni Mkuu wa Chuo cha Afya ya Jamii na Uuguzi kilichopo Hospitali ya Rufaa ya Morogoro, Veronica Mpazi, Makamu mkuu wa chuo, Laurentia Nkulila, Mhasibu wa chuo hicho, Philemon Orungi na mtumishi wa hazina ndogo, Atusubisye Mwabulambo.
  [/FONT]
   
Loading...