A
Anonymous
Guest
Watumishi wa Halmashauri ya Ushetu, Wilaya ya Kahama, tumekuwa tukikumbana na changamoto ya kubadilishiwa vituo vya kazi bila kufuata taratibu stahiki. Aidha, watumishi wanaohamishwa hawapewi stahiki zao za uhamisho kama walivyoomba kupitia barua zao zilizowasilishwa katika Ofisi ya Mkurugenzi.
Badala ya kulipwa stahiki zinazostahili kwa mujibu wa kanuni na taratibu za utumishi wa umma, baadhi ya watumishi wanapewa kiasi cha shilingi 500,000 tu kama malipo ya jumla, bila maelezo ya kina kuhusu fedha hizo na msingi wake wa kisheria.
Tunaomba suala hili lipaziwe sauti ili watumishi wapate haki zao za msingi. Ikiwa Halmashauri haina fedha za kugharamia uhamisho wa watumishi, tunaomba viongozi husika, ikiwemo CHMT, Katibu wa Afya na DMO, wasitumie mamlaka au nafasi zao kuwakandamiza watumishi wa afya kwa kuwahamisha bila kuwalipa stahiki zao halali.
Soma Pia: Ucheleweshaji Malipo ya Uhamisho kwa Walimu Nanyumbu ni usumbufu
Tunaomba mamlaka husika zichukue hatua za haraka ili kuhakikisha haki, uwazi na usawa vinazingatiwa kwa watumishi wote.