Watumishi wa Umma waombwa na Hazina kuorodhesha Dini na Kabila zao. Rais Samia na Wasaidizi wako, haya yanafanyika kwa lengo gani?

Boss sio kweli mm wakati naanza ajira kuna kipengele kwenye mkataba wangu ajira za serikali kinauliza dini.Hili jambo sio jipya nashangaa kuona mleta mada analikuza kana kwamba limekuja leo.Au kwakuwa kwenye ajira za serikali ni mgeni.
Hiyo ilikuwa zamani sana ikafutwa baadaye
 
Kipolisi nadhani kuulizwa kuhusu kabila kuna justification.
Bado hakuna justification yoyote hapo. Kuna mambo ni ya kitaifa au ya kibinaadamu zaidi kuliko ki kabila. Hicho mnachoita "tabia za kikabila" ni matokeo ya kimazingira zaidi na wala siyo genes hivyo huathiriwa zaidi na mazingira anayoishi kuliko kabila lake. Haya ni miongoni mwa masalia ya ukoloni kama yale ya binaadam alikuwa nyani. Hizi ni sawa na stori za kuamini eti kuna makabila ni malaya kuliko mengine: siyo kweli.

Much as satisfaction level au sababu za sex almost sawa, ni mazingira tu aliyoishi mtu ndiyo hutoa tafsiri ya jambo flani litendeke vipi au alipe value gani kiasi mtu huyo akiishi mazingira mengine tabia hiyo hubadilika. Infact, kuendelea kuwepo kwa vijitabia vya hovyo vinavyonasibishwa na ukabila ni matokeo ya elimu mbovu inayoshindwa kuleta "convergence" kwenye hayo mambo ya msingi. Mhehe aliyezaliwa au aliyeishi na kusomea Texas definitely hatakuwa sawa na mhehe aliyeishi huko Mufindi. Then essence ya kabila kwenye tabia inatoka wapi hapa!

Mfano mwingine, jamii inamuona mmasai kama ni mtu mshamba, duni, anayefaa kuishi porini tu na mifugo yake. Is that true? Je hakuna wamasai wengine ambao kwa kupata Elimu, au exposure au kuishi na jamii/ mazingira mengine wamekuwa tofauti na mfumo wa asili waliouzoea.

Ukabila ni jambo ambalo halina afya yoyote na popote kwenye society ya Tanzania au jamii iliyostaarabika.
 
Mbona cc wachagga tumebaguliwa sana tumeporwa pesa zetu live. Na kutolewa makazin na kufilisiwa hamkusema na yule mh sana chief. Cc hatuon jipya hapo. Kwetu tulishakubali yote tunapambana na maisha tu kaz ipo kwenu.
 
Hii siyo nchi aliyotawala mchongameno ambayo idadi ya watu haikufika hata milioni 10. Leo nchi ina watu milioni 60. Bila kuwagawanyisha watu nchi haitawaliki. Divide and conquer strategy. Tuendelee hata nchi za Marekani na Ulaya wanakuuliza ethnicity/race/language kwenye mambo mengi tuu na wanaishi kwa usalama. Mnaogopa nini nyie?
 
Kwenye rekodi za serikali huwa hakuna dini wala kabila la mtu. Nyerere aliondoa hiyo zamani sana wakati taifa bado ni changa, na hata marais waislamu Mwinyi na Kikwete hawakuirudisha. Sasa tumepata mwislamu kamili ndiye anayeyaleta. Katika teuzi wake naona kipengele cha dini kimekuwa ni cha muhimu sana kwake; na ili kukihalalisha ndiyo maana ameunganisha na ukabila akianzia na kurudisha uchifu.

View attachment 2095774



Kichuguu,
Hizo takwimu hapo chini zinatoka katika Waraka wa Uchaguzi wa Shura ya Maimamu Tanzania.
Uliwekwa kwa madhumuni ya kuwazindua Watanzania hali iliyoko nchini:

''Serikali ya awamu ya tano ilipoingia madarakani Mwaka (2015), Rais alifanya uteuzi wa Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Wilaya na Wakurugenzi mbalimbali. Uteuzi wake ulikuwa kama ifuatavyo:

Mawaziri na Manaibu: 30.

Waislamu 10, sawa na asilimia 33%.

Wakristo 20, sawa na asilimia 67%.

Makatibu Wakuu na Manaibu: 50.

Waislamu 10, sawa na asilimia 20%.

Wakristo 40, sawa na asilimia 80%.

Wakuu wa Mikoa na Wilaya: 166.

Waislamu 41, sawa na asilimia 25%.

Wakristo 125, sawa na asilimia 75%.

Makatibu Tawala wa Mikoa na Wilaya: 163.

Waislamu 24, sawa na asilimia 15%.

Wakristo 139, sawa na asilimia 85%.

Wakurugenzi mbalimbali: 249.

Waislamu 45, sawa na asilimia 18%.

Wakristo 204, sawa na asilimia 82%.

Manaibu Kamishna wa Polisi: 25.

Waislamu 5, sawa na asilimia 20%.

Wakristo 20, sawa na asilimia 80%.

Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Polisi: 33

Waislamu 7, sawa na asilimia 21%.

Wakristo 26, sawa na asilimia 79%.

Jumla Kuu ya Uteuzi:

Waislamu asilimia 20%.

Wakristo asilimia 80%.

Uteuzi huo umekuwa kama Sera kwa teuzi zinazoendelea ndani ya miaka yote mitano. Vilevile kama Mwongozo kwa wateule wenye mamlaka ya kuteuwa. Mwelekeo huo unakinzana na Katiba ya nchi ibara ya 13(4)(5), inayokataza ubaguzi wa aina zote. Kwa hakika Taifa halihitaji kiongozi wa nchi akiwa Muislamu basi ateuwe idadi kubwa ya Waislamu wenzake katika nafasi mbalimbali za uongozi wa nchi au akiwa Mkristo atumie uongozi wake kuteua idadi kubwa ya Wakristo wenzake katika uongozi nchini. Au akiwa Mzanaki ateuwe idadi kubwa ya Wazanaki wenzake katika nafasi mbalimbali za uongozi na mfano wa hayo.''
 
Kama ndio hivi hatuna rais hapa..haya masuala ya ukabila na udini..hayana maana..uwiano apeleke huko mchamba wima.

Mind you katika dunia hii superiority huwezi ikwepa ndani ya jamii...mana kuna wajanja na vilaza tu hata ufanyeje.

#MaendeleoHayanaChama
Eh! Vilaza tena?
 
Habari wana JF ..

Mimi niliahidi sitamkosoa Rais Samia, kwa sababu nilishawakosoa sana ma Rais wa nchi hii hadi nachoka; lakini Kuna mambo ni mazito huwezi hata kufikiri yanaweza kufanyika kwa karne hii.
Napata taabu kuamini kama hili suala ni kweli, na kama ni kweli basi aliye-propose na kulipitisha wote ni viumbe wapumbavu kupita maelezo! Na kama SSH analifahamu hili, na anaacha liendelee, basi nitamdharau sana kwa sababu ni jambo ambalo haliwezi kuwa justified kwa tafsiri yoyote ile!!

I wish hii thread nisingeiona mapema kwa sababu imeniharibia mood sana!
 
Kama ndio hivi hatuna rais hapa..haya masuala ya ukabila na udini..hayana maana..uwiano apeleke huko mchamba wima.

Mind you katika dunia hii superiority huwezi ikwepa ndani ya jamii...mana kuna wajanja na vilaza tu hata ufanyeje.

#MaendeleoHayanaChama
Jiwe...
Ikiwa taifa lolote lile duniani kunakuwa watu wa imani maalum ndiyo wanahodhi nafasi ndani ya serikali kwa kuwa wao ndiyo wenye akili zaidi ya wengine basi hapo kuna tatizo.

Ikiwa taifa lolote lile duniani kunakuwa watu wa imani maalum ndiyo walio nje ya nafasi ndani ya serikali kwa kuwa wao hawana akili kama wenzao basi hapo kuna tatizo.

Lakini ukweli ni kuwa hakuna hali kama hii popote ulimwenguni.
Ukiona dini moja imehodhi fursa zote nchini lazima kutakuwa na walakini.

Ukichunguza walakini huu jibu utalipata.

Ikiwa Tanzania ya leo baada ya miaka 60 ya uhuru hali ndiyo hii ya 20:80 lazima marekebisho yafanyike.
 
Bado hakuna justification yoyote hapo. Kuna mambo ni ya kitaifa au ya kibinaadamu zaidi kuliko keep kabila. Hicho mnachoita "tabia za kikabila" ni matokeo ya kimazingira zaidi na wala siyo genes hivyo huathiriwa zaidi na mazingira anayoishi kuliko kabila lake. Haya ni miongoni mwa masalia ya ukoloni kama yale ya binaadam alikuwa nyani. Hizi ni sawa na stori za kuamini eti kuna makabila ni malaya kuliko mengine: siyo kweli. Much as satisfaction level au sababu za sex almost sawa, ni mazingira tu aliyoishi mtu ndiyo hutoa tafsiri ya jambo flani litendeke vipi au alipe value gani kiasi mtu huyo akiishi mazingira mengine tabia hiyo hubadilika. Infact, kuendelea kuwepo kwa vijitabia vya hovyo vinavyonasibishwa na ukabila ni matokeo ya elimu mbovu inayoshindwa kuleta "convergence" kwenye hayo mambo ya msingi. Mhehe aliyezaliwa au aliyeishi na kusomea Texas definitely hatakuwa sawa na mhehe aliyeishi huko Mufindi. Then essence ya kabila kwenye tabia inatoka wapi hapa!

Mfano mwingine, jamii inamuona mmasai kama ni mtu mshamba, duni, anayefaa kuishi porini tu na mifugo yake. Is that true? Je hakuna wanadai wengine ambao kwa kupata Elimu, au exposure au kuishi na jamii/ mazingira mengine wamekuwa tofauti na mfumo wa asili waliouzoea.

Ukabila ni jambo ambalo halina afya yoyote na popote kwenye society ya Tamzania au jamii iliyostaarabika.
"Hii itategemea na jinsi Mahakama itakavyopima"

Mkuu, hujaona hiyo phrase hapo juu kwenye comment yangu? Sasa mbona umetokwa na povu namna hii? Ngoja ni-assume hukuielewa.

Ingawa ni asubuhi ila tujifunze kusoma comments kwa utulivu. Iko hivi, Kabila la mtu siyo absolute determinant ya maamuzi ya Mahakama, ndiyo maana nikasema kuna wakati unaweza kuwa wa kabila linalo-attract maamuzi fulani Kimahakama lakini bado Mahakama ikaamua kinyume chake.

Naomba kubakia.
 
"Hii itategemea na jinsi Mahakama itakavyopima"

Mkuu, hujaona hiyo phrase hapo juu kwenye comment yangu? Sasa mbona umetokwa na povu namna hii? Ngoja ni-assume hukuielewa.

Ingawa ni asubuhi ila tujifunze kusoma comments kwa utulivu. Iko hivi, Kabila la mtu siyo absolute determinant ya maamuzi ya Mahakama, ndiyo maana nikasema kuna wakati unaweza kuwa wa kabila linalo-attract maamuzi fulani Kimahakama lakini bado Mahakama ikaamua kinyume chake.

Naomba kubakia.
Hiyo statement na maelezo yote ya chini yanazidi kubainisha kuwa kabila is no longer and shouldn't be a means to determine a ruling in any dimensions. Niliuelewa vizuri na given nilipo nimeamka masaa mengi sana yaliyopita. Kimsingi hiyo statement haina msingi wowote wa kutetea swali la kutaka kujua kabila la mtu katika mfumo wa kufanya maamuzi (mahakamani) kwa sababu nilizoeleza. Kama inafanyika ni kutokana na udhaifu wetu wa mifumo ya haki, uchumi, Siasa na uongozi. Period.
 
Habari wana JF ..

Mimi niliahidi sitamkosoa Rais Samia, kwa sababu nilishawakosoa sana ma Rais wa nchi hii hadi nachoka; lakini Kuna mambo ni mazito huwezi hata kufikiri yanaweza kufanyika kwa karne hii.
Haya si wangeyapata NIDA...ama wasubiri kwenye sensa ya watu na makazi wangejua mambo ya dini na ukabila.
 
Habari wana JF ..

Mimi niliahidi sitamkosoa Rais Samia, kwa sababu nilishawakosoa sana ma Rais wa nchi hii hadi nachoka; lakini Kuna mambo ni mazito huwezi hata kufikiri yanaweza kufanyika kwa karne hii.

Mimi niwaombe Serikali, niwaombe CCM, niwaombe washauri wa Rais, kama mmechoka, mtuachie hili Taifa.
Wengine bado tunataka kuliona Taifa letu likiwa moja.

Vyombo vya usalama, basi mshaurini mheshimiwa Rais vizuri, msijisahau sana mkaiacha nchi kwenye auto-pilot.
Niwakumbusheni Taifa hili halikujengwa kwa matofali, la hasha!
Mpitisheni Mh. Rais katika historia ndogo ndogo zile njema, zilizotufanya Watanzania japo tukawa wamoja, potelea pote na umaskini wetu.

Sasa hamuwezi amini, leo hii Hazina inaomba taarifa za watumishi (CV), na miongoni mwa taarifa wanazotakiwa kujaza hao watumishi ni:-
1. Kabila lako .....
2. Dini yako .......

Zipo taarifa zingine, za kipuuzi zinazoombwa, ila haina haja sana kuzitaja, kwani hazina athari sana kama hizi mbili.

Hivi kweli, leo mnataka DINI ya mtumishi, iwasaidie nini?
Hii taarifa mnaitumia kuboresha nini?
Udini wa nini katika Tz ya leo.
Tuna ajenda gani na Dini za watu, (watumishi). DINI, DINI.....DINI...!!!!?....,leo tunauliza DINI yako ni ipi? Kweli mh. Rais Samia.

Halafu mnataka na KABILA, kabila la mtumishi litumike kuboresha nini?
Mna ajenda gani huko?
KABILA, leo mnamuuliza mtu KABILA... Kweli mh Rais Samia , ulisema wewe huna kabila, sijui ni Mzanzibar, sasa hawa watumishi, karne ya 21, mwaka 2022, wawajazie makabila yao, muyajue, myafanyie nini?!

Mh Rais Samia, hebu kataa mambo mengine.
Siku Taifa hili likiparaganyika mikononi mwako, hao unaowaona, watakukataa.

Mfumo wa CV (format) na taarifa zinazotakiwa nimeambatanisha hapa.
denooJ , MTAZAMO , barafu , Tindo , Chige , shige2 , Malcolm X5 , MALCOM LUMUMBA ,

View attachment 2095758
Mbona hizi taarifa za dini na kabila hazijaanza leo, labda kama ww ndio umeanza kuziona awamu hii ya sita ila toka muda ukienda polisi au hosipital walikua wanauliza kabila na dini yako
 
Niliajiriwa mwaka 2009, nilikutana na fomu yenye vipengele vyote hivyo. Mwaka 2019 tulitakiwa ku-update taarifa zetu kwa kutakiwa kujaza cv iliyoandaliwa serikalini na ilikuwa na vipengele vyote ninavyoviona hapo; hakukuwa na kelele wala miguno ya kidini kwa kiongozi aliyekuwepo. Kwa sasa tangu achukue nchi mama samia nimejifunza yafuatayo;

1. Samia anachukiwa sababu ya dini yake tu basi. Kila anachofanya lazima KILAZIMISHWE kuhusishwa na dini yake na kikihusishwa na dini yake basi lazima ILAZIMISHWE kuwa kapendelea dini yake. Hali haikuwa hivyo kwa mtangulizi wake aliyeleta upendeleo sio wa udini tu bali hadi ukabila.....alisifiwa na kutukuzwa huku habari ya udini wake wa wazi na ukabila hata haukusemwa! Mapungufu meeengi tunayoambiwa ya samia, ukweli uliofichika ni chuki dhidi ya dini yake tu asingekuwa dini hiyo ninaamini hata tusingesikia. Hata huyu Kikwete asiyekoma kutukanwa na kuhusishwa na utawala wa mama samia, sababu kuu ni dini yake tu. Mkapa angelikuwa hai hata usingesikia mashambulizi yoyote dhidi yake.

2. Chuki na hila za maadui kumbe huleta baraka sana; tutulie na kuwapenda tu maadui Mungu yupo na anaangalia na analipa. Nimejifunza hili kutoka kwa mwinyi, kikwete na sasa huyu mama samia. Hawa watu hukuti jema linasemwa kuhusu wao humu mitandaoni. Ni taarifa hasi tu dhidi yao kuwa hawajui kuongoza, wana udini, hawajaleta maendeleo yoyote n.k Yanasemwa hayo huku waliokuwa wadini haswa wakiachwa, wenye roho mbaya wakiachwa, wenye upendeleo wa wazi wa kikanda wakiachwa. Uungwana wao wa kuwapenda watu na kuwapa furaha kwa kuwamwagia ajira na fursa zingine unafichwa ndani huko. Lakini mwisho wa yote Mungu anawafariji kwa kuwapa umri mrefu wenye furaha na vizazi vyema vinavyochipua (sote ni mashahidi hapa).
 
mbona kama hili suala kuna watu wamepanic sana.

Mamlaka zinataka utambuzi wa watumishi wake ili zikiwapanga kuwe na usawa..

Baada ya hapo wakuu wa kila taasisi wanapewa amri kuhakikisha kunakuwa na usawa maofisini na kwenye kutoa ajira...

Zipo taasisi zimejaa Wanyakyusa, Wahaya, Wachaga, Wasukuma nk..

SIONI SHIDA HAPO..tuache kulalama
 
Back
Top Bottom