Watumishi wa umma wanaingia mwaka wa 6 wakiwa na mshahara ule ule uliopanda kwa mara ya mwisho mwezi July, 2015

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,011
144,371
Tuliwalaumu na kuwalaani wakoloni kwa mambo mengi mojawapo ikiwa ni kutoa ujira mdogo kwa watu weusi na tukaamini tukipata uhuru, mambo haya yataisha.

Cha ajabu, leo hii watwala ambao ni watanzania wenzetu, wanaturudisha kule kule tulikotoka sio tu kwa kutoa mishahara inayoendana na gharama halisi za maisha, bali sasa tunashududia watumishi wa umma wakiingia mwaka wa sita huku mishahara yao ikibaki ni ile ile kwa maana ya kutotoa nyongeza ya mishahara kwa miaka mitano na sasa tukiingia mwaka wa sita isipokuwa kwa wachache waliobahatika kupandishwa mishahara kutokana na kupanda vyeo.

Hakika hii si haki na sitashangaa hata mwaka huu wasipopandisha na zaidi nitashangaa iwapo watapandisha.

Miongo sita ya kujitawala mambo ndio haya!

This is very, very inhumane!
 
Tuliwalaumu na kuwalaani wakoloni kwa mambo mengi mojawapo ikiwa ni kutoa ujira mdogo kwa watu weusi na tukaamini tukipata uhuru, mambo haya yataisha....
Wenyewe watakuona wewe kuwa mtu wa ajabu sana. Tena si ajabu ukaambiwa umetumwa.

Wao wanashukuru sana kwamba wana kazi. Wanapata huo mshahara kila mwisho wa mwezi

Je, umetumwa na hao vijana wanaozurura huko mitaani ili litokee la kutokea na wao ndio wawe wa kwenda huko mitaani?

Huoni walivyotulia, kwani unadhani hawana akili za kufikiri hawa watu?

Ngoja nimalize kwa kukuambia hili: Baada ya Mkwawa na wengine wengi wa enzi hizo, nchi hii tumepata bahati sana ya ushawishi alioufanya Mwalimu Nyerere hadi tukapata uhuru wetu bila ya matatizo yoyote. Wale wakoloni wangerudi leo....! Haya basi bhwanah, kama huelewi.
 
Mm ni rais wa wanyonge!

Nasema uwongo ndugu zangu?
Kwani, wafanya kazi ni "wanyonge" au sio wanyonge?

Na hao "wanyonge" halisi, rais wao kawafanyia kitu gani hasa kwa unyonge wao, kitu ambacho tunaweza kukitaja bila wasiwasi kuwa wanyonge wamefaidika nacho!
 
Bro tusiwalaumu wafanyakazi,tuwalaumu wananchi ndo wasaliti wakubwa hasa wanawake ambao ndio wengi.wananchi wamewatwisha mzigo watumishi na mtaji wa ccm ni wananchi walalahoi ambao ndo wengi ndo JPM alisema hahitaji kura za watumishi akijua fika Ni wachache.

Hata vyama vya wafanyakazi haviwatetei tena watumishi.Wawaombe wabunge wapitishe mswada wa kuvifuta vyama vya wafanyakazi ili ijulikane kuwa hawana mtetezi.wajifunze kutoka kenya.Vyama vya wafanyakazi vinawapiga pesa yao wakati hawawatetei.
 
Back
Top Bottom