Watumishi wa Umma wamekuwa wanyonge Namba moja Nchi Hii. Tatizo idadi yao haigeuzi matokeo ya chaguzi

NewPage

JF-Expert Member
Mar 22, 2021
1,281
2,020
"Pls ninaomba huu uzi wangu usifutwe au kuunganisha, manake siku hizi JF hamnipendi nyuzi zangu nyingi mnazifreeze! WHY?"

Mwaka huu Benki zimeambiwa zipunguze riba kwa kuwaneemesha wakulima (Rais Mama Samia alienena haya akijisahaulisha kabisa kuhusu watumishi wa umma ambao ndiyo wakopaji wakuu). Punguzo la riba za mikopo ya benki hizo kwa watumishi wa umma ni HOLAAAAAA! Hawa watu walipandishiwa mshahara kwa shilingi 2,600 hivi, wakati huo huo kutuma muamala MMOJA tu wa shilingi elfu ishirini ndiyo kiasi cha shilingi 2,600 hiyo ambayo ndiyo nyongeza ya mshahara.

Huo mshahara ukiingia kwenye akaunti ya NMB gharama yake ya kuutoa kwa ATM ni kwa kila elfu 50 ni kama zaidi ya elfu moja na ushee kwa sasa. Je ni kweli mtumishi huyu anaangaliwa na Serikali ya mama huyu? Juzi Shabiby kawanenea hawa watumishi, anagalau huyu mtu kaanza kubadilika na kuona jinsi ambavyo wao kama bunge wameshindwa kabisa kuwasimamia watumishi. Hakuna mbunge kama Marehemu Bilago - huyu alikuwa mtetezi wa watumishi wa umma hakika.

Riba za benki za kukopesha hawa watumishi iwapo zingefikia hata 12% basi hawa watu wangepata nafuu na hata kuweza kukopa tena na kukidhi baadhi ya mahitaji yao. Watumishi wa umma wamekwama sana kipindi hiki, wengi waliokuwa wanajenga nyumba zao zimeishia zilipoishia tangu atoke JK. Huyo JPM hakujali na hata hayo mamiundombinu aliyoonesha kuyakamilisha ni yale yalioanzia kipindi cha JK. Mamiradi yalioanza kipindi chake hamna ulio kamili hata mmoja.

Watumishi hawa wamebanwa kila kona. Watoto wao wakipata nafasi ya chuo hawapati kabisa mikopo eti kwa kuwa hawahesabiki kutoka familia zenye hali duni. Yaani kila kona ni mashambulizi. Watumishi hawa wamenyongonyezwa kiuchumi na kifikra ndiyo maana hata ukija uchaguzi wanazongania kupata nafasi ya kusimamia chaguzi angalau wahongwe na wanasiasa. Wanasiasa wanawachezea tu hawa watumishi.

Hata wakifanya kazi nzuri ndiyo wao wa kusengenywa tu. Mwanasiasa bila hata kutathmini unashangaa tu katamka kumsimamisha mtumishi wa umma kwa kutumia majungu. Mwanasiasa kwenye jukwaa ni kuwasema tu watumishi ili wao wapate umaarufu. Watumishi wenyewe wameufyata haswaa utadhani mbwa koko anaogopa kipigo. Hawajijui kuwa wana nguvu.

Viongozi wa vyama vya wafanyakazi wanahonga chaguzi. Serikali inaingilia chaguzi zao na kuwaweka watu wao. Rais wa Chama cha Walimu kawekwa pembeni kwa sababu tu ya uswahiba wa Katibu Mkuu wake na Waziri husika na vyama. Kisa huyo Katibu Mkuu anajigamba kuishika Serikali.

Watumishi wamekuwa ndiyo tabaka la mwisho haki zao kuzingatiwa nchini. Wamekaa wanahangaika na maneno mengi na majungu mumo humo na kufanywa kama kondoo!
 
kwa nini muwe wanyonge wakati Rais Samia alitoa ahadi kuwa mwakani mambo yenu yatakuwa mazuri?!
kwa sasa chapeni kazi kwa bidii na maarifa ili nchi isonge mbele.
hayo mengine ya mikopo na riba tayari BoT ilisha toa maelekezo kwa Mabenki yote kupunguza riba, hivyo ni suala la utekelezaji tu.
 
Wewe ni Waziri nani?
 
"gharama yake ya kuutoa kwa ATM ni kwa kila elfu 50 ni kama zaidi ya elfu moja na ushee kwa sasa" sina data lakini na mashaka na statement hiyo
 
Acha wapelekeshwe TU na hao wanasiasa Hadi akili ziwakae sawa! Wafanyakazi wa nchi hii ni maamuma yasiyojua kudai haki zao na wanafikiri Kuna mwajiri atakayewajaza mapesa Kwa ridhaa yake! Haki hudaiwa, haiombwi! Tucta, cwt, et Al wakamueni TU hao wanachama wenu na tafuneni hizo ada Kwa raha zenu kwani hayupo wa kuwahoji juu ya matumizi yenu!
 
Huwezi kugeuza matokeo katika uchaguzi ambao si wa HAKI na wala si HURU. WANAIBA hao wahuni na kura zao ambazo zimeshapigwa siku nyingi kila jimbo nchini.

"Pls ninaomba huu uzi wangu usifutwe au kuunganisha, manake siku hizi JF hamnipendi nyuzi zangu nyingi mnazifreeze! WHY?"

Mwaka huu Benki zimeambiwa zipunguze riba kwa kuwaneemesha wakulima (Rais Mama Samia alienena haya akijisahaulisha kabisa kuhusu watumishi wa umma ambao ndiyo wakopaji wakuu). Punguzo la riba za mikopo ya benki hizo kwa watumishi wa umma ni HOLAAAAAA! Hawa watu walipandishiwa mshahara kwa shilingi 2,600 hivi, wakati huo huo kutuma muamala MMOJA tu wa shilingi elfu ishirini ndiyo kiasi cha shilingi 2,600 hiyo ambayo ndiyo nyongeza ya mshahara.

Huo mshahara ukiingia kwenye akaunti ya NMB gharama yake ya kuutoa kwa ATM ni kwa kila elfu 50 ni kama zaidi ya elfu moja na ushee kwa sasa. Je ni kweli mtumishi huyu anaangaliwa na Serikali ya mama huyu? Juzi Shabiby kawanenea hawa watumishi, anagalau huyu mtu kaanza kubadilika na kuona jinsi ambavyo wao kama bunge wameshindwa kabisa kuwasimamia watumishi. Hakuna mbunge kama Marehemu Bilago - huyu alikuwa mtetezi wa watumishi wa umma hakika.

Riba za benki za kukopesha hawa watumishi iwapo zingefikia hata 12% basi hawa watu wangepata nafuu na hata kuweza kukopa tena na kukidhi baadhi ya mahitaji yao. Watumishi wa umma wamekwama sana kipindi hiki, wengi waliokuwa wanajenga nyumba zao zimeishia zilipoishia tangu atoke JK. Huyo JPM hakujali na hata hayo mamiundombinu aliyoonesha kuyakamilisha ni yale yalioanzia kipindi cha JK. Mamiradi yalioanza kipindi chake hamna ulio kamili hata mmoja.

Watumishi hawa wamebanwa kila kona. Watoto wao wakipata nafasi ya chuo hawapati kabisa mikopo eti kwa kuwa hawahesabiki kutoka familia zenye hali duni. Yaani kila kona ni mashambulizi. Watumishi hawa wamenyongonyezwa kiuchumi na kifikra ndiyo maana hata ukija uchaguzi wanazongania kupata nafasi ya kusimamia chaguzi angalau wahongwe na wanasiasa. Wanasiasa wanawachezea tu hawa watumishi.

Hata wakifanya kazi nzuri ndiyo wao wa kusengenywa tu. Mwanasiasa bila hata kutathmini unashangaa tu katamka kumsimamisha mtumishi wa umma kwa kutumia majungu. Mwanasiasa kwenye jukwaa ni kuwasema tu watumishi ili wao wapate umaarufu. Watumishi wenyewe wameufyata haswaa utadhani mbwa koko anaogopa kipigo. Hawajijui kuwa wana nguvu.

Viongozi wa vyama vya wafanyakazi wanahonga chaguzi. Serikali inaingilia chaguzi zao na kuwaweka watu wao. Rais wa Chama cha Walimu kawekwa pembeni kwa sababu tu ya uswahiba wa Katibu Mkuu wake na Waziri husika na vyama. Kisa huyo Katibu Mkuu anajigamba kuishika Serikali.

Watumishi wamekuwa ndiyo tabaka la mwisho haki zao kuzingatiwa nchini. Wamekaa wanahangaika na maneno mengi na majungu mumo humo na kufanywa kama kondoo!
 
Acha wapelekeshwe TU na hao wanasiasa Hadi akili ziwakae sawa! Wafanyakazi wa nchi hii ni maamuma yasiyojua kudai haki zao na wanafikiri Kuna mwajiri atakayewajaza mapesa Kwa ridhaa yake! Haki hudaiwa, haiombwi! Tucta, cwt, et Al wakamueni TU hao wanachama wenu na tafuneni hizo ada Kwa raha zenu kwani hayupo wa kuwahoji juu ya matumizi yenu!
Sindano!
 
Back
Top Bottom